Katika somo hili utajifunza jisni ya kujuwa aina ya data iliyotumika kwenye python
Ili uweze kujuwa aina ya data iloiyotumika kwenye pytho tutatumia function ya type(). Hii hutumika kutambuwa ni aina gfani ya data iliyotumuka. Angalia mifano hii:-
Mfano 1:
mafunzo = "python, php, javascript, java"
print(type(mafunzo))
Hii itakupa majibu haya:
<class 'str'> kumanisha kuwa hiyo object hapo ni string. String hufupishwa kwa kuandika str. Kwahiyo hapo tunapata majibu kuwa "python, php, javascript, java" Ni string
Mfano 2
bei = 16500
print(type(bei))
Hii itakupa majibu <class 'int'> kumaanisha kuwa hii ni int yaani namba
Mfano 3
bei = 2.5
print(type(bei))
Hii itatupa jibu <class 'float'> kumaanisha kuwa yo ni float
Mfano 4
a = [1,2,3,4]
print(type(a))
Hii itakupa majibu <class 'list'> kumaanisha kuwa hiyo ni list
Mfano 5
a = ('Google', "Amazon", "Bongoclass" ,"Youtube")
print(type(a))
Hii itakupa majibu <class 'tuple'>
Mfano 6
wanafunzi = {15:'juma', 100:'ali', 28:'rashid', 9:'john', 12:{2:'dada', 4:'kaka', 1:'baba'}}
print(type(wanafunzi))
Hii itakupa majibu <class 'dict'>
Mfano 7
a = 2>3
print(type(a))
Hii itakupa majibu <class 'bool'>
Hivi ndvyo utaweza kujuwa aina ya data iliyotumika. Somo linlaofuata tutajifunza jinsi ya kubadili aina ya data. Kwa mfano kubadili int kuwa floaf
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-10-21 Download PDF Share on facebook WhatsApp