Katika somo hili utakwenda kujifunza aina za data ambazo hutumika kwenye python. hapa utajifunza aina kuu 3 za data.
AINA ZA DATA KWENYE PYTHON
Python inatambuwa aina zifuatazo za data:
String ni mkusanyiko wa herufi,namba na herufi, herufi na alama ama alama peke yake. Mara nyingi pythoni hukusanya alphanumerical character. Yaani herufi na namba. Katika python string itafahamika kwa kuzungurukwa na alama za kunukuu yaani (“) aua (‘) Mfano wa string
Matumizi ya backlash kwenye string
Katika string zingatia sana matumizi ya alama za kunukuu. Kama umeanza na single quote (‘) basi unatakiwa umalize na single quote. Na kama umeanza na double quote (“) basi hivyo hivyo umalize nayo. Mfano print(‘bongoclass”) hii haitakiwi inatakiwa iwe hivi print(‘bongoclass’) au print(“bongoclass”)
Sasa endapo umeanza na single quote (‘) na ukataka kuandika neno lenye single quote kwa mfano ng’ombe hapa utatumia backlash (/). Bila kufanya hivyo utapata error.
Mfano:
Mfano huu sio sahihi print('ng'ombe')
Ili kutatuwa tatizo hili tutatumia backlash print('ng'ombe') Au tutatumia double quote print("ng'ombe").
2. Namba za integer
Kwenye python tukisema namba tunakusudia namba nzima. Hizi ni namba ambazo sio za desimali au sehemu. Mfano wa namba hizi ni 0,1,2,3,4. Unapoandika namba hizi huna haja ya kuweka alama za kunukuu (quote). Na endapo utatumia ala hizo kwenye nmba hapo namba itabadilika kuwa string.
Mfano:
print(5 +4) Hii itakupa jibu la 9 kwa kuwa nimejumlisha namba 5 na 4. Lakini hii print('5' + '4')Itakupa jibu la 54 yaani tano na nne hapo imefanya concatnation. Hapo 5 na 4 sio namba ni string.
Kwenye python hairuhusiwi kufanya concatnation yaani kujumlisha kati ya namba na herufi. Mfano print('5' + 5)Hii hairuhusiwi na uki run hapo utapata error. Au hii print('bongoclass' + 5) Pia hairuhusiwi wa sababu ni string na nmba huwezi kuzijumlisha kwa pamoja.
3. Float
Hizi ni namba ambazo zinakuwa na desimali au sehemu. Mfano 3.2, 1.5, ½, ⅕ . kwenye python ukigawanya mbambo zozote mbili jibu utakaopata ni float na sio integer. Mfano 10/2 jibu ni 5.0 na sio 5.
print(10/2) Jibu hapo linakuja 5.0 hii ni float na sio integer.
Mwisho:
Zipo aina nyingine za data ambazo tutakuja ziona katika somo linalofuata. Aina hizo hazipo tofauti na hizi tulizozisoma, ila muinkano wake utakuwa na wa utofauti.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-10-21 Download PDF Share on facebook WhatsApp