Katika somo hili utajifunza maana ya variable, na sheria za kutengeneza variable kwenye python. Pia utajifunza maneno ambayo hayafai kutumiwa kama variable
Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya variable na jinsi ya kuandika variable.
Variable tunaweza sema ni kitu ambacho kinabeba thamani ya kitu fulani, ama huwakilisha kitu fulani. Kwa mfano unaposena x ni sawa na 7 hapo hiyo x ni variable na hiyo saba ni thamani.
Jinai ya kuandika variable na kuipa thamani (value).
Kwanza utaandka jina la variable yako. Mfano jina
Kisha itafuata alama ya sawasawa (=) alama hii kazi yake ni ku declare varibale yaani kuipa thamani varibale
Kisha ndipo utaandika hiyo thamani ya variable yako. Mfano “juma” kumaanisha kuwa variable jina ilioajw aapo kipengene a, thamani yake ni juma. Kwenye python variable hiiitaonakena hivi jina = "juma"
Angalia mfano huu:
jina_la_kwanza = "juma"
jinalapili = "saidi"
umri = 34
print(jina_la_kwanza)
print(jinalapili)
print(umri)
Variable hizi zitakupa matokeo haya:-
.
Sifa za variable kwenye python:
Kwanza haitakiwi kuanza na special character kama @, #, $, %, ? na nyinginezo. Mfano #jina = ali hii sio sawa. Usawa wake ni jina =” ali”
Unaweza kutumia underscore (_) mwanzoni mwa varibale badala ya kuanza na namba mfano _2023
Pili variable haitakiwi kuanza na namba. Mfan 2023 = “mwaka” hii sio sawa. Usawa wake iwe _2023
Zingati herufi yaani neno “Jina” na neno “jina” haya ni maneno mawili tofauti mfanoVariable hizi ni mbili tofauti jina = "juma" ; JinA = "juma"
Vyema kama variable yako ina maneno zaidi ya moja nganisha kwa kutumia underscore yaani (_) mfano jina_la_baba
Ikiwa thamani ya variable ni neno ama maneneo ama herufi au alama basi zungushia kwa (“) au kwa (‘) b mfano jina = “bongoclass” au jina = ‘tarzan’
Endao variable ni namba basi hautaweka hizo alama za kuninuu. Endapo utaziweka hiyo variable yako haitahesabika kuwa ni namba.
Mfano:
mwaka = 2023
print(mwaka)
Hiyo itakupa matokeo ya 2023
8. Unaweza ku update thamani ya variable baada ya kui declare kwa kutumia thamni mpya.
jina = "bongoclass"
jina = "Tanzania"
print(jina)
Code hizo zitakupa matokeo Tanzania na sio bongoclass kwa sababu variable umebadilishwa baada ya kui declare kwa mara nyingine kwa thamani toauti
9. Unaweza kuunganisha variable zaidi ya moja kwa kutumia alama ya jumlisha (+) hii hujulikana kama concatnation
Mfano:
mafunzo = "python"
darasa = "bongoclass"
gharama = "bure"
print("Jifunze" + mafunzo + "kutoka"+darasa + "kwa gharama ya "+gharama)
Hii itakupa matokeo
Pia unaweza kufanya mahesabu kwa kutumia variable. Angalia mfano huu
a = 5
b = 6
print(a *b)
Hi itakupa jibu la 30
10. MANENO HAYA HAYATAKIWI KUTUMIKA KWENYE VARIABLE:
False def if raise
None del import return
True elif in try
and else is while
as except lambda with
assert finally nonlocal yield
break for not
class form or
continue global pass
Mwisho:
Katika somo linalofuata tutakwenda kujifunza aina za data kwenye python. Katika somo hilo tutakwenda kufanyia kazi somo hili la variable kwa vitendo hatuwa kwa hatuwa.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-10-20 Download PDF Share on facebook WhatsApp