PYTHON somo la 11: Matumizi ya comperison eperator katika python


image



Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu operator. Hasa hapa tutakwend akujifunz akuhusu comparison operaor.



Huu ni muendelezo wa somo la operator ambapo tulisha jifunza aina moja wapo ya iperator ambazo ni arthmetic operator. Hizi tuliziona wakati tunafanya mahesabu kama kujumlisha, kutoa, kugawanya na kuzdisha. Sasa katika somo hili tutakwenda kuona aina nyingine ya operator ambayo ni comparison operator.

 

Comparison eperator hizi ni operator ambazo hulinganisha na huleta majibu ya kweli ama si kweli yaani True au False. Kwa mfano nikisema 1 == 1 hii ni kweli yaani moja ni sawa na moja. Kwa hiyo hapo comparison eperator ni ==

 

Comperative objective inaweza kutumika kwa ajili ya kulinganisha namba, object, boolean ama string. Na katika python operator hizi zimegawanyika kama:-

  1. == Sawa sawa
  2. !=  si sawa sawa
  3. > kubwa kuliko
  4. < ndogo kuliko
  5. >= kubwa kuliko au sawasawa
  6. <= ndogo kuliko au sawasawa.

 

 

.

Kwa kuwa tulishajifunza baadhi ya izo alama kwenye masomo yaliopita hap nitatuma mifano micache ili kujazia maarifa.

 

  1. Alama ya (==)

Hii hutumika pale unapolinganisha vitu ili kujuwa kama ni sawa sawa. Kwa mfano 5 na 6. Sio sawa hivyo tukitumia alama hiyo ya == jibu litakuwa false yaani sio kweli.

print(5==6)

 

  1. Alama ya (!= )

Hii hutumika  pale unapolingalisha vitu kwa kutafuta kama sio sawa. Kama tutatumia mfano wa hapo juu jibu litakuwa true yaani kweli kuwa 6 na 5 sio sawa.

print(5!=6)

 

  1. Alama ya ( >)

Hii hutumika pale unapoangalia kama je kitu kimoja ni kikubwa kuliko kingine. Kwa mfano kama tutaangalia je 5 ni kubwa kuliko sita. Jibu litakuwa false kumaanisha sio kweli.

print(5 > 6)

 

  1. Alama ya (<)

Hii hutumka pale tunapoangalia kuwa je hiyo item ni ndogo kuliko nyingine. Kama tutatumia mfano wetu hapo juu kuangalia je 5 ni ndogo kuliko 6 jibu litakuwa true kumaanisha ni kweli kuwa 5 ni ndogo kuliko 6.

print(5 < 6)

  1. Alama ya (>=)

Hii hutumika kuangalia je hiyo item ni kubwa kuliko au ni sawa sawa na item flani. Kwa mfano wetu wa hapo juu 6 ni kubwa kuliko tatu. Hivyo kama tutatumia alama hiyo kuangalia kuwa je 6 ni kubwa kuliko ama ni sawasawa na 5 jibu liyatupa true. Kwani hapo kitaangaliwa kimoja wapo. Eidha iwe ni kubwa kuliko ama iwe ni sawa sawa.

print(6 >= 5)

 

 

Alama ya (<=)

Hii ni kinyume na hiyo hapo juu. Yenyewe huangalia kama ni ndogo kuliko ama ni sawa sawa.

print(6 <= 5)

 

 

Mwisho

Somo linalofuata tutakwenda kujifunza zaidi kuhusu assignment operator.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-11-16 Download PDF Share on facebook WhatsApp

RELATED POSTS

picha

Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu string indexing. Kama tulivyojifunza
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu number method yaani function
picha

Katika somo hili utajifunza kuhusu maana ya python na kazi
picha

Katika soo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kubaduli aina moja
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza syntaxy za python yaani sheria
picha

Katika somo hili tunakwenda kujifunza aina nyingine za data ambazo
picha

Katika somo hili utakwenda kujfnza kuhusu string method nyinginezo. Katika
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza aina za data ambazo hutumika
picha

Katika somo hili utajifunza maana ya variable, na sheria za
picha

Katika somo hili utajifunza jisni ya kujuwa aina ya data