PYTHON - somo la 10: string method na zinavyofanya kazi


image



Katika somo hili utakwenda kujfnza kuhusu string method nyinginezo. Katika somo lililopita tulijifunza kuhusu string indexing.



1. Kubadili herufi ya kwanza ya string kuwa katika herufi kubwa

Kufanya hivi tutatumia function ya capitalize(). Mafano tuna neno bongoclass lote limeandikwa kwa herufi ndogo. Sasa tunataka kufanya herufi b kuwa B ili kisomeke Bongoclass

 

string = 'bongoclass'

capitalized_string = string.capitalize()

print(capitalized_string)

 

 

 

2. Kubadili string yote kuwa katika herufi kubwa. Kufanya hivi tunatumia function ya upper(). Mfano neno letu la awali bongoclass tutalibadilisha kuwa BONGOCLASS. 

 

string = 'bongoclass'

upper_string = string.upper()

print(upper_string)

 

 

3. Kujuwa idadi ya character kwenye string. Kufanya hivi tutatumia funvtion ya len(). Mfano neno letu bongoclass hapo tutakwenda kuhesabu ina character ngapi?

 

string = 'bongoclass'

print(len(string))

 

4. Kubadilisha sehemu ya string. Kufanya hivi tutatumia replace(). Kwa mfano hapo leno letu bongoclass tunataka liwe bongocare. Sasa function hii ina sehemu kuu 2 yaani parameter 2, ya kwanza ni kipande cha string ambacho unataka kukitoa. Na sehemu ya pili ni kipande cha string ambacho unakwenda kukiweka.

Kipande cha kwanza hapo tutawea class na kipande cha pili tutaweka care

 

string = 'bongoclass'

replace_string = string.replace('class', 'care')

print(replace_string)

 

 

5. Kubadili string kuwa katika herufi ndogo tupu. Kufanya hivi tutatumia function ya lower() . Kwa neno BONGOCLASS tunataka tulibasili kuwa bongoclass.

 

string = 'BONGOCLASS'

small_string = string.lower()

print(small_string)

 

 

6. Kuangalia kifungu cha character kama kipo  kwenye string. Kufanya hivi tutatumia keyword in  au not in. Kwa mfano katika sentensi hii tunatoa mafunzo ya php, html, css na java . Sasa hapa tunataka kuangalia kwenye list hii je html ipo ama haipo.

 

Ikiwa itakupa jibu true maana yake hiyo string ipo na ikikupa jibu false maana yake haipo. 

 

string = 'tunatoa mafunzo ya php, html, css na java'

check_string = 'html' in string

print(check_string)

 

Hapo kama utaangalia javascript itakupa jibu false. Kwa sababu javascript haipo kwenye hiyo string yetu.

string = 'tunatoa mafunzo ya php, html, css na java'

check_string = 'javascript' in string

print(check_string)

 

Sasa kama ukitumia key word not in  ni kinyume ca in  kwa maana kama kifungu cha string kipo itakuambia false na kama hakipo itakuambia true. Mfano huo hapo juu tukiugeuza badala ya false itakuwa true.

 

string = 'tunatoa mafunzo ya php, html, css na java'

check_string = 'javascript' not in string

print(check_string)

 

 

Mwisho

Katika somo linalofuata tutakwenda kujifunza kuhusu logical oparator

 



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-11-15 Download PDF Share on facebook WhatsApp

RELATED POSTS

picha

Katika somo hili tunakwenda kujifunza aina nyingine za data ambazo
picha

Katika soo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kubaduli aina moja
picha

Katika somo hili utajifunza jisni ya kujuwa aina ya data
picha

Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu string indexing. Kama tulivyojifunza
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu operator. Hasa hapa tutakwend
picha

Katika somo hili utajifunza kuhusu maana ya python na kazi
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu number method yaani function
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza aina za data ambazo hutumika
picha

Katika somo hili utajifunza maana ya variable, na sheria za
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza syntaxy za python yaani sheria