Katika somo hili utajifunza kuhusu maana ya python na kazi zake. pia jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya somo.
Python ni moja katika lugha za kikompyuta zilizo maarufu. Ilianzishwa mwaka 1991 na Guido van Rossum. Python ni moja katika high level programming language ambayo ni general programming language yaani inatumika kwenye field nyingi.
Python imekuwa ikifanyiwa marekebisho mengi toka ilipoanzishwa na sasa tupo katika toleo la 3 yaani python 3. Katika course hii tutakwenda kutumia toleo la 3 la python.
Matumizi ya python
Python file extension:
Kama ilivyo kuwa language zote zina extension kama ilivyo hatml ni .html, php ni .php, basi na python ni .py. Mfano main.py
Maandalizi kwa ajili ya course hii:
Kwa watumiaji wa kompyuta:
Course zinazopatikana bongoclass zinalenga wanafunzi wa aina zote. Kwa wale wanaotumia kompyuta na wale waotumia simu janja. Sasa kwa wale wanaotumia kompyuta fuata maelekezo haya:-
Hapo bofya palipoandika New Project.kisha utakuja ukurasa mwingine ambao ni huu
Kama ndio mara yako ya kwanza hapo usiset kitu chochote zaidi ya jina la project yako tu. hapo mwanzoni kabisha kuna palipoandikwa pythonProject
Badili jina la project yako kutoka pythonProject kuwa jina unalotaka wewe. Kwa mfano mimi nitasema pythonMafunzo
Baada ya hapo bofya create kwa chini upande wa kulia. Itaanza kuload ili kuandaa mazngira ya hiyo project yako. Baada ya kumaliza utakutana na ukurasa mkubwa ambao ndio uwanja wa kuanzika code zako.
Kwa upande wa kushoto kuna project root. Ambapo kuna faili linaonekana limefungka kwa upande wa kulia na kuna code utaziona. Faili hilo linaita main.py hilo ndio faili la kwanza la project yako.
Sasa fanuya hivi. Kwenye huo ukurasa uliofunguka upande wa kulia futa kila kitu kisha weka code hizi:
print("haloo bongoclass")
Baada ya hapo run hizo code kwa kubofya kialama cha ku play kilicho upande wa kulia kwa juu
Angalia kwa chini kuna ukurasa umefunguka. Ukurasa huo utaochesha vitu vitatu:-
Hiyo namba 1 inaonyesha hilo faili linapatikana wapi kwenye kompyuta yako. Hiyo namba 2 ndio matokeo ya code zetu. Kwa mfano hapo utaona haloo bongoclass hayo ni matokeo ya code ambayo tumeandika hapo juu. Ha hiyo namba tatu utaona kuwa code 0 kumaanisa kuwa hakuna tatizo. Kama umefiika hapo basi kompyuta yako ipo tayari kuendelea ku code python.
Location ya project yako:
Ili kujuwa mahali ilipo project yako utakwenda kwenye local disc c, kisha user kisha jina la user wa kompyuta yako, kisha shuka mpaka chini utakuta folder limeandika pycharmProject. Hapo ndipo project yako utaikuta.
Kwa watumiaji wa kompyuta somo letu limeishia hapa. Tkutane somo la pili ambapo tutakwenda kuzungumzsia sheria za kuandika code ya python.
Kwa watumiaji wa simu:
Baada ya kubofya alama hiyo utapata matokeo ya code zako kama inavyoonekana hapo chini. Utaona hapo neno haloo bongoclass na chini yake kuna maneno yanasomeka kama program finished. Angalia hizo picha hapo chini.
Sasa ni wakati wa ku save faili letu. Angalia kwa juu kuna icon ya folda bofya hiyo. Kisha bofya save . utafunguka ukurasa wa kuchaguwa wapi u save, wewe cjhaguwa hapo mwanzo kama inavyoonekana kwenye picha. Program itatengeneza folder lake na utaona maandishi chini yanasema use this folder bofya hapo. Utatakiwa ku ruhusu app iweze ku access mafaili kwenye simu yako. Itakubidi uruhusu hapo.
Baada ya kumaliza hatuwa hiyo utarudishwa tena kwenye app yako kwa ajili ya ku save jina la faili lako. Futa jina lililokuwepo kisha weka main.py. Hiyo main ndio jina la faili na .py ndio extension ya faili kama ilivyo .php, au .html au .css.
LOCATION YA PROJECT YAKO:
Kama unataka sasa kulona fplder lenye project yako, nenda kwenye file maneger kisha ingia kwenye document. Hapo utakutana na folder la python 3 ukifunguwa ndani ya folder hilo utakutana na faili lako la main.py.
Kama umefika hatuwa hiyo basi simu yako ipo tayari kuendelea na masomo yanayofuata. Tukutane somo la pili tutakwenda kuzungumzia sheria ya kuandika code za python.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-10-20 Download PDF Share on facebook WhatsApp