Katika somo hili tunakwenda kujifunza aina nyingine za data ambazo hutumika kwenye python.
AINA ZA DATA KWENYE PYTHON SEHEMU YA PILI
Hapa tutakwenda kujifunza aina nyingine za data ambazo hutumika kwenye python. Aina hizi zina mfanano kidogo na array lakini ni tofauti.
Hii ji aina ya data ambazo huwasilishwa kwa njia ya list yaani orodha. Aina hii ya data inaweza kukusanya data zilizo katika makundu tofautootofauti. Kwa mfano inaweza kuwa na namba tupu, ama hstring tupu amna ikachanganya string, float na namba.
Katika aina hii ya data tutatumia mabano ya bracket ambayo ni [] ili kutengeneza list yetu. Kila data moja hutenganisha na nyingine kwa kutumia alama ya koma (,). Jambo la kuzingatia ni kuwa data hizi husomwa kwa kupuata kanuni za array, yaani tunaanza 0. Kw amfano kwenye lista hii [1,2,3,4,5] hapo tukitaka kujuwa 5 ni yangapi tutasema ni ya 3 kwenye orodha kwa kuwa tunahesabu kuanzia sifuri. Kwahiyo orodha hiyo ina data 4 tu na sio 5. Angalia mifano hiyohapo chini:-
Mfano 1: kwa namba tupu
a = [1,2,3,4]
print(a)
Hapo itakupa matokeo haya
Mafano 2: kwa string tupu
b = ['Google', "Amazon", "Bongoclass" ,"Youtube"]
print(b)
Code hizo zitakupa matokeo haya
Mfano wa 3: kwa mchanganyiko
c = [2023, "python", 2011, "java", 16.5]
print(c)
Code hizo zitakupa matokeo haya
Pia unaweza kuweka list ndani ya list nyingine (nested list). Mfano
b = ['Google', "Amazon", "Bongoclass" ,"Youtube", ["blog", "web", "app"]]
print(b)
Hapo utapata matokeo haya:-
Jinsi ya ku display value mahususi ndani ya list data:
Kwa mfano kwenye list hii ['Google', "Amazon" "Bongoclass" "Youtube"] Na unataka ku display Bongoclass kutoka kwenye hiyo lista hapo. Kwa nza itakupasa kujuwa hiyo bongoclass ni ya ngapi kwenye list. Kumbuka utatakiwa kuhesabu kuanzia 0. Hivyo basi hapo bongoclass itakuwa ni ya 2. Sasa endapo utataka ku display hiyo tu itakubidi utumie hiyo index yake ambayo ni 2.
Mfano:
b = ['Google', "Amazon", "Bongoclass" ,"Youtube"]
print(b[2])
Hii itadisplay Bongoclass
Sasa tuseme kuwa tunataka ku display Bongoclass na Google kwanza tutatakiwa kuzijuwa index namba zao. Kumbuka kuanzia 0. Hivyo kwenye list hiyo Google ina index 0 na Bongoclass ina index 2. Kwa maana hiyo sasa tutatumia index hizo ku display kama tulivyofanya hapo juu
b = ['Google', "Amazon", "Bongoclass" ,"Youtube"]
print(b[2],b[0])
Hizo zita display Bongoclass Google
Na endapo utahitaji ku display list iliyo ndani ya list
Hapa utafanya vilevile kwa ja ujuwe index ya hiyo lista. Mfano tuna hii lista
Hapo list iliyoyopo ndani ya list ina index ya 4. Hivyo tutatumia index ya 4 ku rint hiyo list. Mfano
b = ['Google', "Amazon", "Bongoclass" ,"Youtube", ["blog", "web", "app"]]
print(b[4])
Hiyo itatupatia matokeo haya
Na endapo tunataka ku display data maalumu, kwa mfano tunataka ku display app hapo kwanza tutatakiw akujuwa index ya list yote ambayo ni 4 kisha tujuwe index ya hilo neno app kwenye list ndogo ambayo ni 2. Hivyo tutatsena print(b[4][2])
b = ['Google', "Amazon", "Bongoclass" ,"Youtube", ["blog", "web", "app"]]
print(b[4][2])
Hapo utapata app
Utaweza kutumia mifano hiyo kwenye list nyingine zaidi.
2. Ana nyingine ni turple
Aina hii ya data ni sawa na list mabayi tumeiona hapo juu, isipokuwa ii ni static yaani haibadiliki badiliki. Tofauti na list ambayo inawez kubadilika muda wote. Katika uandishi utofauti wao ni matuminzi ya mabano. Hii ya turple inatumia mabano haya () yaani parenthesis
Mfano
a = ('Google', "Amazon", "Bongoclass" ,"Youtube")
print(a)
Pia unaweza kuweka list nyingine ndani yake (nested turple)
Mfano
b = ('Google', "Amazon", "Bongoclass" ,"Youtube", ("blog", "web", "app"))
print(b)
Ili ku display data maalmuu kwenye list utafanya kama ulivyofanya lwenye list data type. Kwanza unatakiw aujuwe index ya hiyo data unayoitaka. Kwa mfano tunataka ku display Bongoclass na web kutoka kwenye nested turple. Index ya bongoclass ni 2 na index ya web ni 1 na index ya nested turle ni 4
b = ('Google', "Amazon", "Bongoclass" ,"Youtube", ("blog", "web", "app"))
print(b[2], b[4][1])
3. dictionary
Aina ya mwisho ni python dictionary. Aina hii inahifadhi data kwa mtindo wa key na value yake. Mfano tuna orodha hii
1 juma
2 ali
3 rashidi
4 john
Sasa hizo namba hapo kutoka 1 hadi 4 tunaziita key na hayo majina tunaita value hivyo data zitahifandhi kwa key na value zake. Hapa katikauandishi tutaingiza data zetu kwenye mabano curly yaani {} na seti moja ya data itatenganishwa na nyingine kwa alama ya koma (,) Kwa mfano list hiyo utaweza kuw ahivi :=
watoto = {1:'juma', 2:'ali', 3:'rashid', 4:'john'}
print(watoto)
Sasa kama utahitaji ku display value ya data moja moja kama kawaida kwanza utatakiw akujuwa index ya hiyo value. Kwatika aina hii ya data tunatumia key zao na sio index. Kwa mfano una list hii watoto = {15:'juma', 100:'ali', 28:'rashid', 9:'john'}
Na hapo unahitaki ku display jina rashidi hapo utaangalia je rashidi key yake ni ngapi. Kwa kuangalia hapo key ya rashidi ni 28 hivyo tutasema print(watoto[28])
Kuweka lista ndani ya dictionary data (nested dictionary)
Ili uweke dictionary nyingine ndani ya dictionary utatakiw akwanz akuipa key hiyo dictionary kisha ndipo utaandika value zake ndani. Mfano 12:{2:'dada', 4:'kaka', 1:'baba'}
Angalia mfano huu
watoto = {15:'juma', 100:'ali', 28:'rashid', 9:'john', 12:{2:'dada', 4:'kaka', 1:'baba'}}
print(watoto)
Na ukihitaji ku display nested dictionary peke yake basi utaiita kwa key yake. Mfano
watoto = {15:'juma', 100:'ali', 28:'rashid', 9:'john', 12:{2:'dada', 4:'kaka', 1:'baba'}}
print(watoto[12])
Au kama unahitaji ku display data baamulu kwenye hiyo nested dictionary nayo utaiita kwa key yake. Mfano tunahitaji ku display neno kaka. Hivyo tutatumia key ya 4. Hivyo code zitakuwa hivi
watoto = {15:'juma', 100:'ali', 28:'rashid', 9:'john', 12:{2:'dada', 4:'kaka', 1:'baba'}}
print(watoto[12][4])
Hapo utapata jibu kaka
5. Boolean
Hii ni aina nyingine ya data ambayo nataka nimalizeie nayo. Hii ni data ambayo ina majibu mawili tu yaani TRUE au FALSE kenye programming true ni namba 1 na false ni namba 0. Hii ni kwa kuwa kompyuta inaelewa 1 na 0 tu.
Angalia mfano huu:
a = 5 >8 print(a)
hapa utapatiwa majibu ya FALSE kwani namba 5 haiwezi kuwa kubwa kuliko 8. ili iwe TRUE yaani kweli inatakiwa namba nane iwe kubwa kuliko namba tano. hivyo inatakiwa iandikwe hivi
a = 8 > 5 print(a)
hii itakupatia majibu ya TRUE kwani 8 ni kubwa uliko 5.
Pia unaweza kutumia mfano huu kwenye string.
a = "a" > "b" print(a)
Hapo ni FALSE kwani a inatangulia kuliko b
a = "A" > "a" print(a)
hapa pia ni FALSE kwani herufi ndogo hutangulia kuliko kubwa.
.
Mwisho
Katika somo linalofuata tutakwenda kuona jinsi ya kujuwa aina za data na jinsi ya kubadili aina ya data.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-10-21 Download PDF Share on facebook WhatsApp