PHP somo la 53: class inheritance kwenye PHP Object Oriented Programming


PHP somo la 53: class inheritance kwenye PHP Object Oriented Programming


imageKatika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu class inheritance kwenye object oriented programming.Inheritance ni nini?

Hiki ni kitendo kuwa class moja inarithi property na method kutoka class nyingine. Hii inayorithi itaitwa child class yaani class toto. Katika kurithi huku tutazingatia access modifier, hivyo basi tutarithi method na property ambazo ni public au  protected. Class ambayo inayorithi (inherited) huongezewa keyword extends wakati wa kuitengeneza.

 

Mfano:

<?php

class Gari {

   

}

class prado extends Gari {

    

}

?>

 

Hapo class Gari huitwa parent class na hiyo class prado huitwa child class. Sasa ngoja tuone namna ambavyo tunaweza kurithi method na property ambazo ni public ama protected.

<?php

 

class Gari

{

   public $jina;

   protected $speed;

 

   public function __construct($jina, $speed)

   {

       $this->jina = $jina;

       $this->speed = $speed;

   }

 

   protected function tangazo()

   {

       echo "Tunauza {$this->jina} yenye speed ya {$this->speed}.";

   }

}

 

class Prado extends Gari

{

   public function tangazo_jipya()

   {

//method tangazo ni protected

       $this->tangazo();

   }

}

 

$Toyota = new Prado("Toyota", "180 km/h");

$Toyota->tangazo_jipya();

?>

 

Hapo utaona method tangazo() ni protected lakini tumeweza kuitumia kwenye child class prado(). Hii ni kwa sababu class Prado() imerithi property na method kutoka kwenye parent class  Gari().

 

Kwa kutumia mfabo huo hata property ikiwa ni protected unaweza kuitumia ndani ya child class bila ya wasi wasi wowote. 

 

Hapo kuna kitu kipya umekiona {$this->jina} umeona hapo tumetumia mabano {} haya hapo yametumika ili tuweze kutumia hizo property kwenye string. Hii kitaalamu inaitwa string interpolation. Angalia mfano mmoja hapo chini

<?php

$x = 4;

$b = 6;

$z = $x +$b;

 

echo "jumala ya {$x} na {$b} ni  {$z}";

jumala ya 4 na 6 ni  10

">...Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-12-02 Download PDF Share on facebook WhatsApp

RELATED POSTS

picha

Katika somo hili utajifunza jinsi ambavyo utaweza kutengeneza mfumo wa
picha

Katika somo hili unakwenda kujifunza jinsi y kutengeneza database na
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuandika function yako
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya ku update na
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu access modifier ili kuweza
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia PHP kutengeneza
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kusoma data kutoka
picha

Katika somo hili utajifunza jinsi ya kufanya sanitization kwenye user
picha

Katika somo hili utakwenda kujifundisha kuhus matumizi ya function kwenye
picha

Katika soo hili utakwenda kujifunza umuhmu wa kutumia PDO kwenye
picha

Katika somo hili utakwenda jifunza jinsi ya kuhesabu row kwenye
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza concept ya traits kwenye OOP.
picha

Katika somo hili utajifunza jinsi ya kukusanya taarifa ambazo watu
picha

Katika somo hili utajifnza jinsi ya ku upload file kwenye
picha

katika post hii utajifunza jinsi ya kufuta post kwenye database.
picha

katika somo hili utajifunza jinsi ya ku upload multiple file