Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu aina za loop DO, FOR, FOREACH LOOPS kwenye PHP
DO, FOR, FOREACH LOOPS
Kama tulivyojifunza katika somo la 7 hivyo somo hili ni muendelezo ya tulipoishia. Hivyo tutatumia mifano inayolingana.
DO LOOP:
Hii inafanana sana na while loop ila utofauti wake ni kuwa kwenye do kwanza code zitaleta matokeo kisha ndipo zitaanza kutest sharti zilizopewa. Yaani kwanza utapata matokeoa ya code halafu ndipo ianze kutest conditions.
Mfano
Unataka kuorodhesha namba zilizo chini ama sawa na 14. Hapa kama condition yetu ni 17 kwa tulivyojifunza kwenye while hapo huwezi pata matokeo lakini kwenye do kwanza italeta matokeo kwa ku display 17 kisha itastop baada ya kuwa test hazijafikiwa.
Jinsi ya kuandika do loops
Utaweka keyword do likifuatiwa na mabano {} kisha utafanye increment sura decrement ili kupata matokeo kwanza kisha ndipo utatest condition kwa kuweka while(). Code zitaoneka hivi.
Mfano huu ni endapo variable ni ndogo kuliko test yetu.
$x = 1;
do{echo $x++, "
";}
while($x<=14);
?>
Sasa endapo variable ni kubwa kuliko test yetu pia tutapata matokeo kwa kuwa kwanza itadisplay hiyo variable yetu kisha ndipo itaendelea kutest.
$x = 20;
do{echo $x++, "
";}
while($x<=14);
?>
Hapo itadisplay namba 20.
FOR LOOP
For loop hutumika utakuwa unajuwa idadi ya code zako unataka zitest mara ngapi. Kwa mfano tuna list ya array array("muembe", "mnazi", "mpapai") sasa tunataka kupata list hii. Hapa tunajuwa fika kuwa listvyetu ina item tatu hivyo code sita run mara 3. Pia unaweza kupata list ya hizo item ndani ya array kwa kutumia count function.
Kuweka for loop
For loop ipo tofauti kidogo na loop tulizojifunza. Yenyewe ina sehemu kuu tatu ambazo ni: -
Initiative counter haa nibpale ambapo unakwenda kuweka mwanzo wa test yako. Mfano unataka itest kuanzia 0 ama 2.
Test counter hapa ndipo ambapo utaanza ku test condition yao
Increment counter hapa ni pale ambapo unakwenda kufanya increment ama decrement.
Kanuni
fo(initiate counter; test counter; increment counter).
Mfano
Sasa tutumie mfano wetu wa hapo juu wa array yetu yenye item 3. Ili tuweze kupata list ya hizo items.
$x = array("muembe", "mnazi", "mpapai");
$b =count($x);
for($c=0; $c<$b; $c++){
echo $x[$c] ." "."";
}
?>
Tofauti na kutumia variable ya areay length unaweza kutumia namba. Kwa kuwa unajuwa kuwa code zako unataka zi run mara ngapi na kupata matokeo hayo hayo. Mfano sasa tunakwenda kutumia namba 3 kwa kuwa tunajuwa kuwa item zetu ni tatu hivyo.
$x = array("muembe", "mnazi", "mpapai");
for($c=0; $c<3; $c++){
echo $x[$c] ." "."";
}
?>
FOREACH LOOP:
Hii ni loop ambayo hutumika kwenye array tu. Tunaweza kupata orotha ya item kwenye arry kwa urahisi zaidi tunapotumia foreach.
Unachotakiwa kufanya ni kuipa variable array yako. Kisha weka Foreach ndani ya mabano weka variable yako kisha weka neno as likiguatiwa na value variable ambayo itakwenda kuitumia wakati wa ku fetch hizo data. Mfano Foreach($x as $j).
$x = array("muembe", "mnazi", "mpapai");
foreach ($x as $j){
echo $j ." "."";
}
?>
Pia unaweza kutumia foreach kwenye associative array. Hii ni array ambayo ina dimension. Inaweza kuwakilisha item na sifa zake. Kwa mfano hapo katika muenbe unaweza kuongeza na sifa ya aina yake inasema embe => dodo au unasema muembe : dodo. Kisha wakati wa ku output na hizo associated value ukazifa weka kwenye statement yako.
$x = array("muembe " =>"dodo", "mnazi" =>"kitamli", "mpapai" =>"bwabwa");
foreach ($x as $j => $k){
echo "$j = $k", "
";
}
?>
Unaweza kuchukuwa mfano huo ukaweka lamda majina ya watu na umri wao, ama unaweza kufikiria kingine.
Mwisho
Tukutane somo la 9 tutakwenda kujifunza kuhusu ku upload mafaili kwa kutumia php. Pia tutajifunza namna ya kudaka taarifa za faili kwa kutumia php.
Pia tutajifunza jinsi za kuingiza taarifa hizo kwenye database. Hivyo basi hakikisha unafahamu jinsi ya kutumia database
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-10-18 Download PDF Share on facebook WhatsApp