PHP -somo la 31: Matumizi ya include() na require() function kwenye php


imageKatika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuandika function za PHP kama require() na iclude()INCLUDE, REQUIRE,  INCLUDE_ONCE na REQUIRE_ONCE

Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu matumizi ya hizi function 3 ambazo kwa pamoja zinahusika na kuhusisha kuhusisha mafaili ya code kwenye mafaili mengi, bila ya kuziandika kila wakati.

 

include()

Incdude hutumika kama unataka kutumia code za faili falni kwenye faili lingine. Kwa mfano unataka kuunganisha database. Sasa kuna mafaili 10 ambayo yanahitaji kutumia database. Hivyo katika hali ya kawaida itakubidi uandike code za kuunganisha database kwenye mafaili yote hayo. Hivyo basi kwa kutumia include tutaandika code hizo kwenye faili moja. Kisha tutatumia function hii ili kuweza kuzitumia kwenye mafaili yote hayo.

Kwa mfano tunataka kuweka menu yetu kwenye kurasa zetu. Hivyo tofauti na kuziandika menu hizo kila ukurasa basi tutatumia include() ili kuweza kuzifikia. Wacha tuone mifano halizi.Hapo chini tutatengeneza mafaili mawili. Moja ni kwa ajili ya menu na lingine tutatumia include ili kuweza kuzitumia menu kwenye file lingine.

 

Faili ambalo tutali include tutaliita menu.php na faili ambalo ltakuwa linatumia hizo code tutaliita home.php. Sasa endapo tutafunguwa faili la home.php litaonesha menu ambazo zipo kwenye file lingine.

 

Menu.php

 

 

 

 

   Android

   Html

   Video

   Contact

 

 

 

 


 

Sasa tunakwenda kuzi include code hizi kwenye ukurasa wetu wa home.php. Na tupate matokeo sawa ya menu hii kwenye ikurasa huo.

 

home.php

 

include 'menu.php';

?>

 

Kwa kutumia mfano kama huu unaweza ku include block nyingi za code. Kufanya hivi kutakupubguzia sana kazi. Baada ya kuandika code hizohizo kila wakati sasa utatumia function hiyo na kuzi include.

 

INCLUDE_ONE()

Function hii hufanana na hiyo iliyotangulia. Utofauti ni kuwa include siku zote itakapotumika ina include code hizo bila hata ya kujali kama zilisha kuwepo ama tayari faili hilo umesha li include. Angalia mfano huu

include 'menu.php';

include 'menu.php';

?>

 

Hapo utaona faili tume li include mara mbili hivy linatupa matokeo mara mbili. Lakini sasa ukitumia include_once() kwanza itaangalia kama hilo faili tayari lipo, itainclude mara moja tu.Kwa fano hapo juu kama tutatumia include_once() tutapata matokeo mara moja tu.

 

Wacha nitumie lugha nyingine kukuelewesha. Yaani once ni neno la kiingereza linalomaanisha mara moja tu. Hivyo basi ukisema include_once yaani include hilo faili mara moja tu. Hivyo hata kama uta include mara mbtatu au zaidi zote hazitafanya kazi. Mara moja tu ndio itakayotumiwa. Angalia mfano hapo chini.

 

include_once 'menu.php';

include_once 'menu.php';

?>

 

Tumepata matokeo mara moja tu wakati tumeinclude mara mbili.

 

Hivyo basi katika mafaili muhimu kama database, ama class au yanayohusika kwenye login mara nyingi hapa tunatumia include_once na kwenye code za kawaida kama style na zile static file huwa tunatumia include.

 

REQUIRE() na REQUIRE_ONCE()

Katika php require() na require_once() hufanya kazi sawa na include() na include-once(). Utofauti wao ni kuwa endapo iclude faili ambalo limetakiwa kuwa katika include halipo code zinatoa warning lakini zinafanya kazi. Lakini endapo require imetumika na kama faili hakipo italeta error na hutoweza kuendelea na program.

 

Hapa chini nitakupa mifano 2 ambapo mafaili hayapo. Yaani nitatumia include kwa faili ambalo halipo uone inavyokuwa. Kisha nitatumia require kwa faili ambalo halipo na itakavyokuwa.

include 'head.php';

//ujumbe huu huwezi kuuona kama tungetumia reuire

echo "Haloo hapo juu faili halipo lakini php imeendelea kutoa matokeo ya code nyingine."

?>


 

Sasa tuone mfano wa require kama faili halipo

require 'head.php';

//ujumbe huu huwezi kuuona kama tungetumia reuire

echo "Haloo hapo juu faili halipo lakini php imeendelea kutoa matokeo ya code nyingine."

?>

 

 

Require hutumika kwenye mafaili ya lazima sana. Kwa mfano mafaili yote yanayohitaji login utatumia require ili kuhakikisha kuwa mtu hatoweza kuingia mpaka alogin. Endapo mtandao lamda utasumbuwa na require faili halikupatikana code zitastop kufanya kazi.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-10-18 Download PDF Share on facebook WhatsApp

RELATED POSTS

picha

Katika somo hili utakwenda kujifundisha jinsi ya kutafuta taarifa maalumu
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuzungumza na server
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kusoma data kutoka
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kufanya encryption na
picha

Katika somo hili unakwenda kujifunza jinsi y kutengeneza database na
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu access modifier ili kuweza
picha

Katika somo hili utajifunza kuhusu syntax za PHP
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza kazi na matumizi ya construct
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuandika function yako
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza aina kuu 3 za variable
picha

Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuingiza data kwenye dtabase
picha

Hapa utajifunza jinsi ya kutengeneza table ambayo tutaitumia kwenye blog
picha

Katika somo hili utajifunza jinsi ambavyo utaweza kutengeneza mfumo wa
picha

Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuandika while loop kwenye
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza kujusu PHP variable, maana yake
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia PHP kutengeneza