PHP - somo la 30: Baadhi function za PHP


imageKatika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya ktumia baadhi ya function za phpBUILT IN FUNCTIONS

Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu functions ambazo zimetengenezwa moja kwa moja kutoka kwa watengenezaji wa PHP. Hapa nitakuchagulia baadhi tu ya function ambazo hatukuziona kwenye level 1. Hivyo kama utahitaji kujuwa functions zaidi rudi kwenye PHP level 1.

 

pi()

Function hii hutumika kwa ajili ya kupata tyhamani ya pi (pai) kwa wale wa hesabu wanaelewa pi ni nini kwenye kutafuta eneo la duara, nusu duara n.k

 

Mfano 1:

<?php

echo(pi());

?>

 

 

min() na max()

Hizi kwa pamoja hutumika kutafuta namba kubwa na ndogo. max() ni kwa ajili ya kutafuta nmab kubwa kwenye orodha ya namba. Na min() kazi yake ni kutafuta namba ndogo kwenye orodha ya namba.

 

Mfano2:

<?php

echo(min(16, 450, 70, 20, 18, 35) . "<br>");

echo(max(67, 210, 51, 20, -16, -12));

?>

 

 

sqrt()

Function hii hutumika katika kutafuta square root ya namba. Wale wa hesabau wanafaham vyema hii function.

Mfano 4

<?php

echo(sqrt(9) . "<br>");

echo(sqrt(50) . "<br>");

echo(sqrt(16) . "<br>");

echo(sqrt(81));

?>

 

 

5. rand()

Function hii hutumika kwa ajili ya kutengeneza random namba. Hii inaweza kutumika kama kutengeneza unique id. Japo tutaona function nyinginezo zitakazotumika sawa na hii.

 

Mfano 5:

<?php

echo(rand());

?>

 


 

Sasa endapo kwa mfano unahitaji random namba hizi zitokee katika mpangilio fulani. Kwa mfano unataka random namba ziwe kati ya 18 na 67. Yaani namba ndogo iwe ni 18 na namba kubwa iwe ni 67. Hivyo random namba zicheze humo. Kufanya hivi itakubiidi utumie parameter ndani ya functuin. Kwa mfano kwenye maelezo hayo itakuwa hivi:

 

Mfano 6:

<?php

echo(rand(18, 67));

?> 

6. uniqid()

Function hii hutumika kuzalisha namba ambazo ni unique yaani haziwezi kufanana. Hii ni muhimu katika ktengeneza id za item kwenye database.

 

Mfano 6:

<?php

echo uniqid();

?>


 

7. session_start()

Function hii hutumika kwa ajili ya kuanzisha session ama kupata taarifa za session. Kwanza tuanze na kutambuwa je session ni kitu gani? Kivinjari chako ya internet (browser) huweza kukutambuwa kwa kutumia session. 

 

Pindi tu unapofunguwa ukurasa kwenye internet browser inakutengenea id yako yaani utambulisho wa kuwez akukutabua kwa muda ule. Utambulisho huu utajilikana kwa jina la session na utambulisho huu katika hali ya kawaida hufutwa punde tu unapofunga browser yako.

 

Ipo hivi unapofunguwa internet hiyo huitwa session. Kisha kila ukifunguwa website session mpya inaanzaishwa. Yaani kila unapokingia website nyingine unakuwa na session yako. 

 

Katika website taarifa ya session inatumika kwenye kurasa zote. Yaani kama session yako imepewa thamani ya zy373ndgdngd8 basi haitoweza kubadilika kwenye website hiyo bila kujali ni kurasa ngapi utatembekea kwenye website hiyo, mpaka pale utakapokunga browser yako, ama session iwe ime expire.

 

Sasa tuone namna ya kuipata session

Endapo sasa unataka kupata session za watumiaji itakubidi utumie variable ili kupata thamani hiyo. Kwanza kabisa uta start session kwa kutumia function hii session_start() kisha baada ya hapo utatumia global variable kwenye function hii session_id()

 

Mfano: 7

<?php

//anzisha session

session_start();

 

//session variable

$id = session_id();

 

//onyesha session Id

print("Session Id: ".$id);

?> 

Kazi za Session

Session itakuwezeha kujuwa ni watu wangapi wapo online, ama ama unawea kujuwa jinsi watumiaji wa web yako walivyo interact. Yaani kwa kutumia session unaweza kujuwa ameingia saa ngapi, na maefanya nini na ni page ngapi amepitia na kila page amekaa kwa muda gani. Session ina kazi nyingi zaidi.

 

8. time()

Function hii hutumika kwa ajili ya kupata muda kwa kutumia format ya unix time. Ipo hivi, unix time ni mfumo wa kuhesabu muda tokea mwaka 1970 kwa sekunde. Yaani hivi, toka mwaka 1970 mpaka sasa ni sekunde ngapo zimefika. Hivyo sekunde hizo utajuwa wewe uzifanyie nini. Kama unataka kujuwa katika dakika tano zilizopita ni watu wangapi walikuwa online kwenye website yako, unaweza kutumia unix time.

 

Mfano8:

<?php

echo time()

?>

 Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-10-18 Download PDF Share on facebook WhatsApp

RELATED POSTS

picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuzungumza na server
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia taarifa ambazo
picha

katika somo hili utajfunza kukusanya taarifa za mafaili. kisha ku
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza concept ya iteration kwenye PHP
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu condition statements if, ifelse
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kusoma data kutoka
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya ku update na
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuandika constant kwenye
picha

Katika somo hili utakwenda kuona namna ya kutuia if else
picha

Katika somo hili utajwenda kujifunza jinsi ya kuzuia hacking kwenye
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza aina za data ambazo hutumika
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuandika function za
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza concept ya traits kwenye OOP.
picha

Katika somo hili tutakwenda kutumia prepared ststement kwenye ku fetch
picha

Katika somo hili unakwenda kujifunza jinsi y kutengeneza database na
picha

Katika somo hil utawenda kujifunza jinsi ya ku edit post