Katika somo hili utakwenda kujifundisha kuhus matumizi ya function kwenye php. Pia utajifunza jinsi ya kuandika function
PHP FUNCTIONS:
Function ni kikundi cha code ambazo huweza kutumika kwa zaidi ya mara moja. Function zipo katika aina mbi ambazo ni:-
Zile ambazo zimekuja moja kwa moja katika php yenyewe hizi huitwa built in functions
Zile ambazo unaweza kuzitengeneza wewe mwenyewe. Hizi huitwa user defined functions
Sifa za Functions:
Huweza kutumika zaidi ya mara moja
Haiload kila page inapoload
Hutumika pale tu itakapoitwa
USER DEFINED FUNCTIONS:
Sasa hebu tuone jinsi ya kutengeneza function yako mwenyewe. Ili uweze kufanya hivi itahitajika kutumia kanuni ifuatayo:-
function jina() {
//weka code hapa
}
Jinsi ya kuandika function yako:
Kwanza anza na neno keyword function likifuatiwa na jina la hiyo function. Kwa mfano tunataka function ya kujumlisha namba mbili. Hivyo tutaipa jina la jumlisha. Kwahyo itakuwa kama hivi: function jumlisha kisha utaweka mabano haya (). Pia jina la function halitakiwi lianze na namba au special character. Kama ile ya dola tulioitumia kwenye variable.Baada ya hapo utaweka mabano haya {} ambapo ndani yake ndipo kutakuwa na code za hiyo function.
Mfano 1
Function jumlisha(){
Code zinakaa hapa.
}
Hebu sasa tuone mfano halisi wa function ya kujumlisha namba mbili:
Mfano 2:
<?php
function jumlisha() {
$a = 4;
$b = 5;
$c = $a + $b;
echo "$c";
}
?>
Hapo tumeshatengeneza function kwa ajili ya kujumlisha namba mbili. Sasa endappo uta load huo ukurasa hautaonyesha chochote, ni kwa sababu function haionyeshi kitu mpaka iitwe. Ili kuiita hiyo function unatakiwa urudie kuliandika jina lake likifuatiwa na mabano (). Mfano katika code hapo juu utaandakia jumlisha () hapo utakuwa umeiita function na itakupa majibu. Hivyo basi code nzima itakuwa:-
<?php
function jumlisha() {
$a = 4;
$b = 5;
$c = $a + $b;
echo "$c";
}
jumlisha()
?>
Jinsi ya kutatua matatizo kwa kutumia PHP function
Chukulia mfano unaandika program ya kuorodhesha majina ya wanafunzi kwa jinsia zao. Sasa una jinsia mbili ya kike na ya kiume. Sasa baada ya kila inapotaja jina la mwanafunzi uandike na jinsia yake. Kwa kutumia function hatutakuwa na haja ya kutaja jinsia kila wakati.
Mfano: 3
<?php
function mv() {
echo "Mvulana <br>";
}
function ms() {
echo "Msichana <br>";
}
echo "Juma " . "jinsia "; mv() ; echo "<br>";
echo "Aisha " . "jinsia "; ms() ; echo "<br>";
echo "Baraka " . "jinsia "; mv() ; echo "<br>";
echo "Neema" . "jinsia "; ms() ; echo "<br>";
echo "Joharia" . "jinsia "; ms() ; echo "<br>"
?>
Function inaweza kuwa ni reference (kumbukumbu)
Mfano unataka test vitu vingi kwa kutumia kitu kimoja. Hicho kimoja ambacho kitatestiwa kitakuwa ndio reference. Mfano tunataka kujumlisha namba kadhaa na namba moja. Hivyo tofauti na kuiandika hiyo namba kila wakati tunapotest basi tutaifanya kuwa reference.
Mfano 4:
<?php
function saba(&$kumbukumbu) {
$kumbukumbu += 7;
}
$x = 3;
saba($x);
echo $x;
echo "<br>";
$b = 6;
saba($b);
echo $b;
?>
Function pia hutumia return statement ili kurudisha thamani fulani. Return keyword hutumika ili kusitisha function kuenelea kufanya kazi. Hii kwanza itasitisha function kisha italeta majibu kutokana na expression iliyowekwa.
Mfano 5:
<?php
function Zidisha($a, $b) {
$c = $a * $b;
return $c;
}
echo zidisha(5, 4) . "<br>";
?>
PHP function pia hubeba argument (parameter)
Hizi hutumika kama variable. Baada ya kurudia kuandika neno fulani unalifanya kuwa argument kwenye function na kupata thani yake moja kwa moja. Kwa mfano watoto wa Daudi.Baada ya kumuandika daudi kila baada ya kumuandika mtoto. Utatumia function
Mfano 6:
<?php
function jina($baba, $mwaka) {
echo "$baba Daudi. Amezaliwa mwaka $mwaka <br>";
}
jina("Saidi", "2003");
jina("Steven", "2008");
jina("Juma", "2009");
?>
Somo linalofuata tutaangalia baadhi ya function ambazo ni built in. Yaani zimetengenezwa moja kwa moja toka kwa waundaji wa PHP. Somo lijalo litakuwa rahisi endapo utakuwa umeshapitia somo la function katika php level 1.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-10-18 Download PDF Share on facebook WhatsApp