Katika somo hili utajifunza kuhusu syntax za PHP
Katika somo hili utajifunza TAG za PHP na jinsi zinavyofanya kazi
Tulishaona katika somo lililopita namna ya kuandaa kompyuta yako na simu yako kwa ajili ya kufunguwa php. Kwa maelezo yaliotangulia katika somo la kwanza uliweza kuandaa simu ama kompyuta yako kuwa server. Katika somo hili tutakwenda kujifunza tag za php na jinsi zinavyofanya kazi.
Php ni tofauti sana na html huwenda ni kwa sababu ni lugha mbili tofauti. Hata hivyo html ina mamia ya tag kama tulivyojifunza katika mafunzo ya html level ya kwanza na pili. Php ina tag chache. Katika mafunzo ya HTML pia tulijifunza kuwa kuna tag za kufungulia na kufungia.
TAG ZA PHP
Php hufunguliwa na tag <?php na hufungwa na ?>. huwenda hizi ndio tag pekee za php zinazotumika katika kucode php. Tag hizi pia unaweza kuzifupisha kwa <? na ?> mfano
<?php
?>
Au
<?
?>
ECHO na PRINT
Ili kuweza kuandika kitu na kionekane kama tulivyotumia kwenye html, basi php inatumia echo na print. Hizi ni statement mbili za php ambazo hutumika ili kuweza kuleta matokeo kwenye browser. Yaani unapoandika code za php zinachakatwa kwenye server, kisha matokeo yake hutolewa kwenye browser kama plain teext (maandishi ya kawaida) kisha html hufanya kazi yake ya kupangilia. Sasa ili kupata haya matokeo ya code za php ambapo mtumiaji wa mtandao ataona ndipo tunatumia hizi echo na print.
Mfano katika html unapotaka kuandika neno “hallo” ili lionekane na mtumiaji wa ukurasa huo utatumia tag mfano <h1>hallo</h1>. sasa katika php utaanza tag za php ya kufunga na kufunguwa ambazo ni <?php kisha unaweka echo ama print utaweka alama ya funga semi na funguwa semi kisha ndani ndipo utaandika huo ujumbe mfano
<?php
echo “hello”;
?>
Kwa kutumia print
<?php
print “hello”;
?>
Echo na print sio tag, katika php hizi zinaitwa statement. Tutajifunza zaidi kuhusu statement katika masomo mengine. Kwa ufupi ni kuwa echo na print zinafanya kazi sawa ijapokuwa utofauti wao ni mdogo. Kwa mfano echo ipo fasta katika kuleta matokeo kuliko print. Echo pia inatumika katika kuleta matokeo kutoka katika parameta zaidi ya moja. Hivyo ijapokuwa zote zinafanana ila zina utofauti mdogo.kama huna uhakika ipi utumie vyema kutumia echo.tutajifunza utofauti wao zaidi katika masomo yajayo.
HTML NA PHP
Php na html zote hutumika katika kutengeneza ukurasa wa wavuti. Katika faili ya html unaweza kutumia php na katika faili la php pia unaweza kutumia html. Ipo hivi browser yako inapokutana na tag za html itachakata na kuleta matokeo na ikikutana na tag ya php inapeleka mchakato kwenye server kisha server ikirudisha text ndipo inatoa matokeo. Mfano:-
Html ndani ya php
<?php
echo “<h1>hello”>
?>
Au unaweza kutumia hii:-
<?php
print “<h1>hallo<h1>”
Pia unaweza kuandika code za html nje ya tag za php katika faili la php mfano
<?php
echo “hello”
?>
<p>hello</p>
PHP NDANI YA HTML
Kama ilivyo ndani ya php file unaweza kuandika html hivyo hivyo unaweza kuandika php ndabi ya faili la html. Unaweza kueka code za php kwenye html tag ama nje ya html tag. Mfano
<h1 style="color:red">
<?php echo "hello" ?>
</h1>
Kwa mfano huu code zote za php zilizopo ndani ya <h1> zitafuata style hiyo. Unaweza pia kutumia php kwenye faili la html nje nje ya tag za html na ikaleta matokeo.
NAMNA YA KUWEKA COMMENT KWENYE PHP
Tumejifunza kwenye html kuwa kukoment ni kwamba unaandika kumbukumbu zako katika code kwamba ili uweze kukumbuka amba mtu mwingine aweze kujuwa kwa urahisi kuwa msitari huo wa code unahusu nini. Komenti hazionekani kwa mtumiaji ijapokuwa zipo kwenye code.
Katika html tulujifunza kuwa ukitaka kukoment unatumia <!-- kisha unaweka koment halafy unamalizia na -->
Ila katika php utatumia // kisha utakomeny. Ama utatumia # kisha itakoment. Namna hii ya kukoment ni pale unapokoment kwa maneno yasiozidi msitari mmoja. Na kama unataka kukoment sana utatumia /* kisha utakomenta halafu utafunga kwa */ mfano:
<?php
//hallo
#hallo
?>
Au kama unataka kukoment misitari mingi
<?php
/* hello
Hii ni
Koment
*/
?>
Endelea kufanyika kazi zaidi somo hili, kwani somo linalofata litakuhitaji uwe umeweza angalau kujuwa tag za php.
Somo linalokuja tutakuja kuangalia namna ya kutumia variable, na kuonyesha matokeo.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-10-17 Download PDF Share on facebook WhatsApp