PHP - somo la 16: Jinsi ya kufuta tabale na database kwa kutumia php


image



Katika somo hili utajifunza jinsi ya kufuta table ya databse kwa kutumia PHP. Pia utajifunza jinsi ya kututa database yeto



Tumesha jifunza namna ya kutengenezadatabase na table kwa kutumia PHP. Sasa somo hili tutajifunza namna ya kufuta database na table. Unaweza kufuta vyote kwa pamoja ama kufuta kimoja kimoja. Endapo utachaguwa kufuta table tu, basi database itabakia lakini ukifuta database, na table pia itafutika na data zilizomo.

 

Maandalizi makubwa hapa ni kama yaliotangulia Andaa variable zote zinazohitajika kama vile server name, database name, username, na password. Tutakwenda kufuta table yenye jina menu kwenye databse inayoitwa hotel. Hivyo database name yetu itakuwa hotel

$servername = "localhost";

$username = "root";

$password = "";

$dbname = "hotel";

 

Katika mafunzo ya database hakuwahi kusoma namna ya kufuta table kwa kutumia SQL. Sasa hapa nitakwenda kukujuza jinsi ya kufanya hivyo. SQL inayotumiaka ni DROP TABLE kisha unaweka jina la database yenye hiyo table kisha utaweka kidoto kati kisha ndipo utaweka jina la hiyo database. mfano DROP DATABASE hotel . menu. Hivyo variable ya statement hii itakuwa  $sql = "DROP TABLE `hotel`.`menu`";

 

Baada ya hapo utaandaa if else kwa ajili ya kukupa mrejesho kama umefanikiwa ama umefeli. Kama tulivyoona katika masomo yliyopita kufanya hivyo tutatumia function hii mysqli_query($conn, $sql)

 

CODE ZA KUFUTA TABLE ZITAONEKANA HIVI    

$servername = "localhost";

$username = "root";

$password = "";

$dbname = "hotel";

 

// Create connection

$conn = mysqli_connect($servername, $username, $password, $dbname);

// Check connection

if (!$conn) {

   die("Connection failed: " mysqli_connect_error());

}

 

// delete database

$sql = "DROP TABLE `hotel`.`menu`";

if (mysqli_query($conn, $sql)) {

   echo "table DELETED successfully";

else {

   echo "Error DELETING table: " mysqli_error($conn);

}

 

mysqli_close($conn);

?>


 

JINSI YA KUFUTA DATABASE

Hakuna tofauti kubwa sana kati ya kufuta table na kufuta database. Kinachobaldilika hopo ni SQL statement baada ya DROP TABLE hotel.menu itakuwa DROP DATABASE hotel. baada ya hapo utafunguwa faili lako kwenye browser na majibu utayapata. ila hakikisha umebadili alert message za kujulisaha kuwa table imefutwa kuwa zikujulishe kuwa database imefutwa.

 

$servername = "localhost";

$username = "root";

$password = "";

$dbname = "hotel";

 

// Create connection

$conn = mysqli_connect($servername, $username, $password, $dbname);

// Check connection

if (!$conn) {

   die("Connection failed: " mysqli_connect_error());

}

 

// delete database

$sql = "DROP database `hotel`";

if (mysqli_query($conn, $sql)) {

   echo "Database DELETED successfully";

else {

   echo "Error DELETING database: " mysqli_error($conn);

}

 

mysqli_close($conn);

?>

 

Mwisho

Tukutane somo la 6 tutajifunza jinsi ya kuweka data kwenye databse kwa kutumia PHP. Pia tutajifunza kuedit data hizo. Somo hili litakuwa chachu ya kujifunza matumizi ya html form katika kukusanaya madodoso.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-10-18 Download PDF Share on facebook WhatsApp

RELATED POSTS

picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu aina za loop DO,
picha

Katika somo hili utakwendakujifunza concept ya namespaces na jinsi inavyosaidi
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutengeneza class na
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya ku update na
picha

Katika ukurasa huu utakwenda kujifunz jinsi ya kuandika code za
picha

Katika somo hili utakwenda kuona namna ya kutuia if else
picha

Katika somo hili utajifunza jinsi ya kutengeneza system ambayo mta
picha

Katika somo hili utajifunza jinsi ya kufanya sanitization kwenye user
picha

Huu ni mwendelezo wa mafunzo ya PHP na hapa tunaaza
picha

Katika somo hili utajifnza jinsi ya kufanya prepared statement kama
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kusoma data kutoka
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kukusanya taarifa za
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza aina kuu 3 za variable
picha

Katika somo hilibutajifunza maana ya cURL pamoja na matumini yake
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza concept mpya ya abstract class
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu condition statements if, ifelse