PHP - somo la 12: Jinsi ya kufanyia kazi taarifa zilizokusanywa kutoka kwa mtumiaji


imageKatika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia taarifa ambazo zimekusanywa kutoka kwa mtumiaji ili kuweka kutatuwa hoja mbalimbaliPROJECT KULINGANA NA COURSE HII.
Kama ulivyokwiisha kutambuwa kuwa katika kila baada ya kumaliza course tunaleta poject. Project hizi zitakusaidia mshiriki wa mafunzo haya kuweza kuelewa zaidi na kufanyia kazi kile ambacho kime fundhishwa. Hapa nitakuletea project tano ambazo ni:-

1.Kikokotoo cha hesabu (Simple calculator with php and html)
2.Kikokotoo cha umri (age calculator with php)
3.Code playground (HTML, CSS and JAVASCRIPT code playground with php)
4.Dodoso la usajili (databaseless registration form).
5.Kuhesabu idadi ya maneno kwenye sentensi ama paragraph

Project hizi ni program fupifupi ambazo zina msingi mzuri kwa mwenye kuanza. Uzuri wa project hizi zote ni za level ya chini ssana kiasi kwamba kama ulishiriki kwenye mafunzo yetu hazitakushinda. Kama ukipata ugumu tafadhali rudia somo lililotangulia la 11 katika mafunzo haya.

1.KIKOKOTOO CHA HESABU
Program hii itakuwa inafanya kaz ka ma kikokotozi yaani calculator. Yenyewe itahusika na matendo manne ya hesabu yaani kujumlisha, kuzidisha na kugawanya. Mtumiaji atahitajika kuingiza namba, tendo (+, *, - au /) kisha ataingiza namba nyingine, atabofya submit kisha atapata majibu.

Program itakusanya data zake kwa kutumia HTML form kisha itatuma namba atakazoingiza mtu kwenye variable za php. Kwa kutumia switch case utaweza kuchaguw tendo. Tafadhali pitia somo la 10 kwenye mafunzo haya upate kujifunza zaidi kama hujaelewa kuhusu switch case.

CODE ZA PROGRAM NI HIZI:-
<html>
<form method="post" action="">
<label>KIKOKOTOZI:</label><br>
<input type="number" name="a" placeholder="0"><br>
<input type="text" name="b" placeholder=""><br>
<input type="number" name="c" placeholder="0"><br>
<br><br><input type="submit">
</form></html>
<?php
$a=$_POST['a'];
$b=$_POST['b'];
$c=$_POST['c'];
$result = "";

 

 

switch ($b) {
case "+":
$result = $a + $c;
break;
case "-":
$result = $a - $c;
break;
case "*":
$result = $a * $c;
break;
case "/":
$result = $a / $c;
}
?>
<p>
<input readonly="readonly" name="result" value="<?php echo $result; ?>">
</p>

 


2.DODOSO LA USAJILI
Katika program hii mtumiaji ataweza taarifa zake kisha zitakuja kama alivyoziweka. Program hii itakusaidia utakapokuja kujifunza namna ya kudisplay taarifa kutoka kwenye database. Kwa sasa hatutatumia database ila somo litakalofata taarifa hizi moja kwa moja zitatola kwenye database baada ya mtu kujiajili.

Program hii itatumia mafaili mawili. Moja ni la HTML kwa ajili ya kukusanya madodoso. Kisha faili lingine litakuwa ni kwa ajili ya kudisplay taarifa zilizojazwa. Katika faili la HTML kwenye action utakuta kuna link ya faili linalofata ambalo ndilo litakalopelekewa taarifa zilizojazwa kwa ajili ya kuchakatwa.

Ijapokuwa unaweza kuchanganya mafaili haya sehemu moja ;akini nimependelea kuyatengenisha kwa ajili ya kujifunza zaidi. Hivyo kama ndio na wewe unaanza weka mafaili mawili. Kisha faili m,oja ni la htm;l code na la pili ni kwa ajili ya php code.

Katika program hii faili la kwanza nimeliita p2.php ambalo litabeba php code na la pili p.php ambalo litabeba hyml code


P.pph
<html>
<form method="post" action="p2.php">
<label>Sensa ya watu na makazi</label><br>
<input type="text" name="a" placeholder="Weka jina lako hapa"><br>
<input type="text" name="b" placeholder="Umri"><br>
<input type="text" name="c" placeholder="Jinsia"><br>
<input type="text" name="d" placeholder="Unapoishi"><br>
<input type="text" name="e" placeholder="Hali ya ndoa"><br>
<input type="text" name="f" placeholder="Elimu"><br>
<br><br><input type="submit">
</form></html>


P2.php

<?php

$a=$_POST['a'];
$b=$_POST['b'];
$c=$_POST['c'];
$d=$_POST['d'];
$e=$_POST['e'];
$f=$_POST['f'];
$t = date("Y/m/d/l");
echo "<p>Karibu sana <b>$a</b></p> <br><br> <u><b>Na hizi ndio Taarifa zako ulizojaza kwenye Sensa hii:-</b></u><br>";
echo "Jina: $a <br>";
echo "Umri: $b <br>";
echo "Jinsia: $c <br>";
echo "Unapoishi $d <br>";
echo "Hali ya Ndoa: $e <br>";
echo "Elimu: $f <br>";
echo "Siku ya kuandikishwa: $t"

?>

 

3.KIKOKOTOZI CHA UMRI
Katika program hii mtumiaji atatakiwa kuwka mwaka wake aliozaliwa kisha program itamtajia idadi ya miaka yake. Program imetengenezwa kwa kutumia kwaka 2021. yaani mtu akiingiza mwaka aliozaliwa program itachukuwa mwaka 2021 kisha itatoa huo mwaka na kupata miaka ya hiyo mtu.

Kwa mfano mtu akiingiza mwaka 2000 program itafanya 2021 - 200 = 21 hivyo idadi ya miaka ni 21. unaweza kimodify program hii kwa kutumia function date() ili iweze kuendana na muda, yaani itakuwa inachukuwa muda wa sasa. Mfano ifikapo 2022 program hii haitasema ukweli lakini kwa kutumia function date() haina aja ya kubadili 2021 kuweka 2022.

Code
<html>
<form method="post" action="">
<label>KIKOKOTOZI CHA UMRI:</label><br>
<br><br>
<label>Weka mwaka uliozaliwa</label><br>
<input type="number" name="a" placeholder="0"><br>
<br><br><input type="submit">
</form></html>
<?php
$a = $_POST['a'];
$c= "2021";
$b = $c - $a;
echo "Una miaka $b";


4.CODE PLAGROUND
Kwa kutumia program hii utaweza kuandika code za html, css na javascript kwenye program hii na kupata matokeo yake yaani preview. Program hii itakusaidia katika kufanya preview ya code zako kujuwa kama umepatia ama laa. Chukulia mfano unaandika <h1>hi</h1> program hii itaonyehsha hi yaani kile ambacho kitapatikana baada ya hizo code za html

Kwa kutumia html form <textarea> mtu ataweza kuandika code zake kwenye uwanja huo. Kisha akibofya submit anapata matokeo. Tafadhali kama hujaelewa kwenye fomu za html ana text area rejea course ya kwanza na pili za html.

<html>
<h1>Code playground</h1>
<form method="post" action="">
<textarea name="a" placeholder="weka code za html hapa"
style="width: 350px;height: 200px;">
</textarea> <br><br><input type="submit">
</form></html>
<?php
$a = $_POST['a'];

echo $a;


5.PROGRAM YA KUHESABU MANENO
Fikiria kwa mfano umetoa interview kwa watu 100, na umewataka wajieleze kwa maneno yasiyopunguwa 300. na wote wameandika, hivi utaweza kweli kuhesabu watu wote kuhakikisha kuwa wameandika maneno mangapi?. hapa utahitaji program itakayokuwezesha kuhesabu maneno walioandika.

Kwa kutumia program hii utaingiza sentensi ama paragraph au ahabari kisha ukibofya submit unaletewa idadi ya maneno yaliyokuwemo. Hapa nimetumia functino str_word_count() ni php function ambayo tumejifunza katika somo la 5. tafadhali kama utapata ugumu rejea somo la tano.

<html>
<h1>HESABU IDADI YA MANENO</h1>
<form method="post" action="">
<textarea name="a" placeholder="sentensi ama paragraph hapa"
style="width: 350px;height: 200px;">
</textarea> <br><br><input type="submit">
</form></html>
<?php
$a = $_POST['a'];
echo "Idadi ya maneno ni:-";
echo str_word_count("$a");
?>


MWISHO WA COURSE
Mpaka kufikia hapa course ya php level 1 ndio nimeifunga. Tafadhalituachie maoni yako ili kuweza kuboresha masomoyetu zaidi na utoaji wa masomo haya. Usiwache kuwa nami kwenye level 2 ya php ambapo tutajifunza zaidi katika yale ambayo tumeyawacha na tutakwenda kuyaona.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-10-18 Download PDF Share on facebook WhatsApp

RELATED POSTS

picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya ktumia baadhi ya
picha

Katika somo hili utakwendakujifunza concept ya namespaces na jinsi inavyosaidi
picha

Katika somo hili utajifunza jinsi ambavyo unaweza kutengeneza blog ambayo
picha

Katika somo hili utajifnza jinsi ya kufanya prepared statement kama
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu aina za loop DO,
picha

Katika somo hili utajifunza jinsi ambavyo utaweza kutengeneza mfumo wa
picha

Katika somo hili utajifunza jinsi ya kutumia filter_var() function kwa
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kusoma data kutoka
picha

katika post hii utajifunza jinsi ya kufuta post kwenye database.
picha

Katika somo hili utajifunza kupangilia data wakati wa kuzisoma kwenye
picha

Katika somo hili utajifnza jinsi ya ku upload file kwenye
picha

Katika somo hil utawenda kujifunza jinsi ya ku edit post
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuzungumza na server
picha

Katika somo hilibutajifunza maana ya cURL pamoja na matumini yake
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza concept mpya ya abstract class
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza kujusu PHP variable, maana yake