Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu condition statements if, ifelse na switch case. Hata utajifunza jnsi ya kuziandika na zinavyofanya kazi
PHP CONDITION STATEMENTS
Hizi ni logic statement ambazo zitaangalia kukidhi kwa vifezo ndipo code ziweze kufanya kazi. Kwa mfano ikiwa asubuhi kompyuta itasalimia umeamkaje, na ikiwa mchana itasema umeshindaje na ikiwa jioni utasema habari za jioni. Hivyo hapa kwanz kompyuta itabidi iangalie saa, kama saa itasoma ni asubuhi ndipo code zinazotaka iseme habari za asubuhi zitafanya kazi.
Kwa pamoja code hivi tunaziita condition statement, yaani kwanza huangalia vogezo vinavyotakiwa kama vimetimia ndipo huleta matokeo na kama havijatimia huenda hatuwa nyingine. Statatement hizi kwenye php zipo nne ambazo ni:-
1.If statement
2.If..else statement
3.If..elseif..else statement
4.Switch statement
1.If statement
Hii itaangalia condition moja (yaani kigezo kimoja) kanuni yake ni
If (condition) {
Code
}
Condition ni kigezo ambavyo unataka kiangaliwe kabla ya code kufanya kazi. Kwa mfano tunataka mfunguaji wa ukurasa huu kama ni asubuhi ukrasa uandike habari za asubuhi. Kufanya hivi itabidi tuweke saa. Saa itakuwa inaangalia kama ni asubuhi ita peleka taarifa kuwa ni asubuhi kisha code ndipo hufanya kazi.
Jivyo tutatumia function ya kuonyesha time kama tulivyojifunza hapo nyuma. Ila hapa tutatumia masaa 24. na kwa masaa 24 asubuhi ni kunania 5 mpaka 11. itabidi tuwe na variable ya kuwakikilisha time. Hivyo tutatumia t kama variable na function ya time kwa ajili ya kusoma muda.
Mfano:
<?php
$t = date("H");
if ($t < ="11") {
echo "habari ya asubuhi";
}
?>
Hii itaangalia kama masaa ni sawa na 11 ama chini ya 11, code zetu zitasoma habari za asubuhi. Saba hapa kuna shida moja, ni kuwa kama itakuwa sio asubuhi hakuna chichite kitakachisoma. Hivyo basi tunatakiwa pia kusema na endapo sio asubuhi inatakiwa iseme nini.
2.If.. else
Ili kufanya hivyo ndipo tunahtaji else statement. Hivyo hapa tutatumia if else statement. Yaani kama itakuwa ni chini ya saa 11 iseme habari za asubhuhi laikini kama sio muda huo iseme mambo vipi. Agalia mfano wa if else statement hapo chini.
Mfano
<?php
$t = date("H");
if ($t < "11") {
echo "habari ya asubuhi";
}else {
echo "mabo vipi";
}
?>
Hapa kama haitakuwa asubuhi itasema mambo vipi
Kanuni ni kama ile ya mwanza
If (condition) {
Code} else{
Code}
Sasa kwa kuwa siku imegawanyika kama asubuhi, mchana na jioni sasa tunataka ikiwa ni asubuhi iseme, habari za asubuhi na ikiwa ni mchana iseme habari za mchana na ikiwa ni usiku iseme habari za usiku.
3.If..elseif…
Kufanya hivi tutahitaji kutumia if elseif else statement. Hapa tutaendelea kutumia function ya kuonyesha time.kwa masaa 25 ambayo ni date(H). kwa masaa 24 asubuhi ni chini ya 11, mchana ni kunzia 12, jioni ni 16 na usiku 19 na kuendelea.
Kanuni ya kutumia if elseif else
If (condition){
Code} elseif (condition) {
Code} else {code
}
Chekki mfano hapoc hini
<?php
$t = date("H");
if ($t < "11") {
echo "habari ya asubuhi";
}elseif ($t >= "19") {
echo "habari za usiku";
} else{
echo "habari za mchana";
}
?>
Unaweza kutumia elseif kadiri ya unavyo taka. Kwa mfano mfano hapo chini nitatumia elseif zaidi ili kuboresha code zetu. Sasa nataka isalimie asubuhi, mchana, jioni, na usiku, na alfajiri.
4.Switch satatemnet
Hii hutumika kana una condition zaidi ya tatu. Switch case ipo fasta kuliko elseif sataament. Ijapokuwa kazi ambazo switch case inafanya pia unaweza kuzifanya kwa elseif ila ufanisi wake hautakuwa mzuri ukilinganisha n switch case.
Kanuni
switch (x) {
case label1:
code ;
break;
case label2:
code;
break;
case label3:
code;
break;
default:
code;
}
Kwanza unatakiwa uwe na thamani ambayo inatakiwa ifikiwe ili code ziweze kufanya kazi. Kama inavyoonekana hapo juu. Utaanza na neno switch kisha inafata thamani inayotakiwa kufikiwa na hii mara nyingi huwa ni variable. Kisha thamani hii ndipo hulinganishwa kwenye code ili kama itafikiwa code ziweze kufanya jazi.
Kila statement au code block hutenganishwa na neno break. Hii hufanya program yako kuishia pale ambapo thamani itafikiwa na kutoa matokeo. Kisha mwisho utaweka default statement. Hii ni statement ambayo endapo thamani haitafikiwa kwa case zote za kwenye cose basi itumike hii thamani ya kwnye default.
Mfano
<?php
$kiti = "mbao";
switch ($kiti) {
case "mbao":
echo "kiti chako ni cha mbao";
break;
case "bati":
echo "kiti chako ni cha bati";
break;
case "chuma":
echo "kiti chako ni cha chuma";
break;
default:
echo "kiti chacho sio cha chuma, bati wala mbao";
}
?>
Katika mfano huu kwanzo code zitaangalia kama kiti ni cha aina gani, kama ni cha mbao condition ya kwanza itakuwa imefikiwa. Hivyoo itafanyia kazi code za kwanza na kupata matokep kiti chako ni cha mbao.
Mfano huu unaweza usielewe utafanya vipi kazi. Chukulia mfano, una website na unataka watu kulingana na umri wao kila mmoja aone maudhui fulani kulingna na umri wake. Hivyo unaweza tumia code hizi, kwamba ikiwa umri ni miaka 18, atapelekwa kwenye ukurasa fulani, ikiwa ni 60 hivyo hivyo na zaidi.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-10-18 Download PDF Share on facebook WhatsApp