PHP - somo la 1: Maana ya PHP na jinsi inavyofanya kazi


imageKatika somo hili utakwenda kujifunza maana ya PHP na jinsi inavyofanya kaziMAFUNZO YA PHP SOMO LA KWANZA

Mahitaji ya course:
1.Uwe na kompyuta ama smartphone
2.Uwe na uelewa wa html
3.Uwe mjanga, wa kuweza kutumia simu ama kompyuta yako vyema
4.Ujuwe kusoma na kuandika
5.Kuwa na hamu ya kutaka kujuwa.


Utangulizi:
PHP ni katika lugha za kikompyuta inayotumika kwenye server. Php hutumika katika kutengeneza kurasa za wavuti kama ilivyo html. Php pia inaweza kutumika katika kutengeneza software. Php ni moja katika lugha zinazotumika sana katika blog kama wordpress na katika social media kama facebook. Php ni free kibiashara na hata binafsi.

Php ilianzishwa mwaka 1994 na mmarekani aliyejulikana kwa jina la Rasmus Lerdorf, ikiwa kama home project. Nika katika luga za kikompuata zilizo rahisi kujifunza, hata hivyo syntax yake inaweza kuwa ngumu kuliko javascript na lugha nyingine.

PHP ni nini?
Php ni kifupisho cha maneno Hypertext Preprocessor. Php hutengeneza kurasa za wavuti kama html, pia huweza kutumiwa ndani ya html ama html ikatumiwa ndani ya php. Kwa pamoja tukaweza kuhama kutokakurasa kwenda kurasa ndio maana php ikawa nayo ipo katika hypertext kama ilivyo html. Tofauti ni kuwa php kwanza code hufanyiwa processing kwenye server, kisha ndipo server hutuma matokeo kwenye browser kama html code ama plain text kwa maana hii ndipo tunapata preprocessor kwa maana kwana code zinachakatwa kwenye server kisha matokeo ndipo hutolewa kama html ama plain text kwenye browser.

 

NINI PHP HUFANYA:
1.Hutengeneza dynamic web page
2.Hutengeneza static webpage
3.Huwengeneza web App

 

Kwa ufupi php ina uweza kufanya mambo haya:-
1.Inaweza kuedit data kwenye database
2.Kuongeza na kupunguza data kwenye database
3.Kujaza fomu za madodoso
4.Kupokea taarifa kutoka katika madodoso (form)
5.Kufunga na kufunguwa database
6.Kufunguwa na kufunga mafaili
7.Kutengeneza dynamic na static web page
8.Kutengeneza system za web App

 

PHP inafanyaje kazi?
Kwanza browser inapokutana na code za php, code hizi hutumwa kwenda kwenye server. Server inachakata code za php na kurudisha matokeo kwenye browser kama plain text, na hapo html huchukuwa nafasi yake, hatimaye maudhui yanaonekana kwenye browser kama html.

Server ni nini?
Server ni kompyuta inayohudumia kompyuta nyingine. Zipo kompyuta maalumu zinafanya kazi ya kuhudumia kompyuta nyingine, lakini kompyuta yako mwenyewe pia unaweza kuifanya iwe server na kuhudumia kompyuta nyingine. Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia sikuhisi hata simu inaweza kuwa server na kuhudumia kompyuta.

Browseer yako kama chrome, firefox na opera zinaelewa html, javascript, xml, css lakini haziwezi kuelewa php. Hivyo ili code za php uweze kuzirun kwenye browser ni lazima uwe na server ambayo inachakata php na kurudisha majibu kama plain text.

 

KUIANDAA SIMU NA KOMPYUTA YAKO KUTUMIA PHP
Kama nilivyokueleza kuwa php inahitaji server. Hivyo unatakiwa uwe na App ambazo zitaweza kufanya simu yako iwe localhost server. Fuata hatuwa zifuatazo:-

1. Kwa watumiaji wa Simu

Kama wewe unatumia simu basi fuata maelekezo haya ili kuweza kuandaa simu yako kwa ajili ya mafunzo. Hapa nitakuletea list za App ambazo inatakiwa uwe nazo. List hii nimeiweka katiuka vifungu viwili ambavyo ni:-

A. Text editor: Hakikisha una moja kati ya App hizi, kama si u yako itagoma utacheki nyingine.

1. Acode - code editor | FOSS (nakushauri uchukuwe hii)

2. DroidEdit (free code editor)

3. Code Editor- Program on Mobile

 

B. Local host server Hakikisha una moja kati ya server zifuatazo:- Ila ninakushauri uwe na hiyi ya kwanza hapo.

1. AWebServer ( Http Web Server  (nakushauri uchukuwe hii)

2. KSWEB: web developer kit

3. Web Server PHP/MyAdmin/MySQL

 

JINSI YA KUANZA KUTUMIA:

1. Kwenye simu yako tengeneza fola kisha lipe jina unalotaka. kwa mfano utaliita web.

2. kati ya moja ya App hizo za kwanza kwenye kundi la text editor funguwa App kisha tengeneza faili jipya kisha weka code hizi hapa chini. Kama utahitajika kuweka jina la faili kabla ya kuendelea andika web.php:-

<?php echo "Haloo Bongoclass" ;?>

3. Kisa sevu faili lako kwenye folda ulio itengeneza. Yaani wakati wa ku sevu chaguwa folda hilo uliotengeneza hapo juu tulioliita web. Kisha sevu hapo ndani ya hilo fpolda. Utakapokuwa unaandika jina la faili andika web.php kisha sevu.

4. baada ya kusevu funguwa moja kati ya App hizo zilizopo kundi la pili, local host server.

5. Hatuwa inayofuata ni kuchaguwa folda ambalo lina mafaili yako ama faili letu tulioandika hapo mwanzo. Kama unatumia awebserver kwenye palipoandika Document root kulia kuna batani imeandika select. Bofya hapo kisha kisha bofya Internal kisha bofya OK. Utaona mafolda ya simu yako. Weka tiki lile folda ambalo tumeweka faili letu. Jina la folda ni web ama kama uliweka jina lako mwenyewe ok weka tiki hapo kisha bofya selwct utaiona kulia upande wa chini.

6. Kisha palupoandikwa Service bofya start. Hapo server yako itakuwa On yaani itakuwa tayari kufanya kazi.

7. kisha kwa juu hapo palipoandikwa Anddress kulia kwake kuna link ipo hivi http://0.0.0.0:8080 bofya hapo utaona ukurasa umefunguka kwenye browser yako.

8. Hapo utaona orodha ya mafaili ambayo yapo hapo. Kwa kuwa mpaka sasa kuna faili moja utaliona hapo. Bofya hilo faili utaona kwenye brower yako maneno haya yatatokea haloo Bongoclass.

9. kama umefikia hapo basi upo tayari kuendelea na somo la pili.

10. Kama utatumia hizo App nyingine maelezo ni kama haya yanafanana.

.

2. kwa watumiaji wa Kompyuta:

kama unatumia kompyuta basi nakushauri utumie moja kati ya software zifuatazo:-

A. Local host server

1. xamp  (Nakushauri uchukuwe hii)

2. wampserver

 

B: Text editor

1. Sublime text  (Nakushauri uchukuwe hii)

2. Notepad ++

 

Jinsi ya kutumia

1. Kama umedownload xamp basi nenda disk C kisha bofya folda lililoandikwa xamp  kisha bofya folda lililoandikwa htdocs ndani ya folda hilo tengeneza folda liite web.

2. Kama ume download wampserver nenda disk c bofya folda lililoitwa wampserver, kisha bofya folda lililoandikwa www kisha ndani ya folda hilo tengeneza folda liite web.

3. Funguwa text editor moja kati ya hizo hapo juu kisha pest code hizi 

<?php echo "haloo Bongoclass" ;?>

4. Kisha sevu faili lako katika kuandika jina chaguwa All files kisha liite web.php halafu nenda ukalisevu kwenye lile folda la web tuliolitengeneza hapo awali.

5. baada ya hapo ni kuwasha server.

Kama unatumia xamp utaiona icon yake kwenye desktop ama start app. Bofya hiyo icon kisha kwenye app angalia palipoandikwa Apache kulia kwake kuna palipoandikwa start. bofya hapo kisha bofya palipoandikwa Admin utaona ukurasa umefunguka. kwenye ubao wa kuandikia link kwenye browser yako link itasomeka hivi http://localhost/dashboard/ kitu cha kufanya kuondoa neno dashboard kisha  kuongeza jina la folda letu pamoja na jina la faili tuliolitengeneza. hivyo link itakuwa hivi http://localhost/web/web.php kisha bofya enter. Hapo utaona maneno haya haloo Bongoclass .

6. kama umefika hapo upotayari kuendelea na somo.

 

7. Kwa wale mliodownload wampserver kwanza bofya icon ya App ya wamserver ulio install, kisha utaiona itakaa kwenye kaji tray ka app upande wa kulia ndani pale . Right click kisha bofya start. Kisha nenda kwenye browser andika http://localhost/web/web.php

 8. Kisha bofya enter utaona maeneo haya haloo Bongoclass

9. Mpaka kufikia hapo utakuwa tayari kuendelea na somo la pili. Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-10-17 Download PDF Share on facebook WhatsApp

RELATED POSTS

picha

Katika somo hili utajifunza kuhusu cronjob na matumizi yake kwenye
picha

Katika somo hili uatakwenda kujifunza jinsi ya kutumia htaccess ili
picha

Katika somo hili utajifunza jinsi ya kufanya sanitization kwenye user
picha

Katika somo hilibutajifunza maana ya cURL pamoja na matumini yake
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutengeneza class na
picha

Katika somo hili utajifnza jinsi ya kufanya prepared statement kama
picha

Katika somo hili unakwenda kujifunza jinsi y kutengeneza database na
picha

Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuingiza data kwenye dtabase
picha

katika somo hili utajfunza kukusanya taarifa za mafaili. kisha ku
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza aina za data ambazo hutumika
picha

Katika post hii utakwenda kujifunza jinsi ya kutuma email kwa
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza concept ya iteration kwenye PHP
picha

Katika post hii utajifunza jinsi ya kupata taarifa muhimu za
picha

Hapa utajifunza jinsi ya kutengeneza table ambayo tutaitumia kwenye blog
picha

Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuandika while loop kwenye
picha

katika post hii utajifunza jinsi ya kutengeneza ukurasa wa dashboard