Katika course hii utakwenda kujifundisha jinsi ya lutengeneza blog kutoka mwanzo hadi mwisho.
Hii ni course mpya inayotarajiwa kufundishwa kwenye mafunzo yetu. Lengo la course hii ni kukufundisha jinsi ya kutengeneza blog yako kwa kutumia PHP, HTML, CSS, SQL na MySQL databae.
Course hii ni rahisi na imetokana na mafunzo ya php level 3 pamoja na mafunzo ya database level 1. Kkabla hujaianza course hii hakikisha umepata mafunzo ya HTML, PHP na SQL kutoka kwenye mfaunzo yetu ya ICT.
Course hii itajikita kwenye mambo kadha kama:-
Course hii itapatikana kwa njia ya text pia utaweza kuangaia video moja kwa moja kwenye channel yetu ya youtube tehama-tz
Mahitaji ya kujifunzia
Utahitajika kuwa na kifaa kama simu ama komputa ambayo imesha andaliwa kwa ajili ya kutumia php na database. Tunashauri utumie moja katika software hizi zifuatazo:
1. Kwa watumiaji wa Simu
Kama wewe unatumia simu basi fuata maelekezo haya ili kuweza kuandaa simu yako kwa ajili ya mafunzo. Hapa nitakuletea list za App ambazo inatakiwa uwe nazo. List hii nimeiweka katiuka vifungu viwili ambavyo ni:-
A. Text editor: Hakikisha una moja kati ya App hizi, kama si u yako itagoma utacheki nyingine.
1. Acode - code editor | FOSS (nakushauri uchukuwe hii)
2. DroidEdit (free code editor)
3. Code Editor- Program on Mobile
B. Local host server Hakikisha una moja kati ya server zifuatazo:- Ila ninakushauri uwe na hiyi ya kwanza hapo.
1. AWebServer ( Http Web Server (nakushauri uchukuwe hii)
3. Web Server PHP/MyAdmin/MySQL
2. kwa watumiaji wa Kompyuta:
kama unatumia kompyuta basi nakushauri utumie moja kati ya software zifuatazo:-
A. Local host server
1. xamp (Nakushauri uchukuwe hii)
2. wampserver
B: Text editor
1. Sublime text (Nakushauri uchukuwe hii)
2. Notepad ++
Pia unaweza kutumia IDE kama PHPSTORM kutoka jetbrain kwa ajili ya kurahisisha uandishi wa code.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-10-20 Download PDF Share on facebook WhatsApp