Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu array kwenye php, na jinsi zinavyoweza kufanya kazi
PHP ARRAY
Array ni kama variable, tofauti hii ni kuwa inahifathi thamani ya data nyingi ndani ya variable moja. Yaani variable moja hapa itabeba thamani nyingi tofauti na tulivyosoma hapo nyuma. Cheki mifano hapo chini:-
Array sikuzote inaaznia kuhesabu kuanzia 0 na kuendelea. Unaweza kuchaguwa list katika array ipi unataka kuionyesha na ipi hutaki utafanya hivi kwa kuiondoa namba ya array hiyo ama kuiweka.
Mfano:
<?php
$masomo = array("hisabati", "sayansi", "maarifa", "kiswahili", "uraina", "kiingereza");
echo "ninasoma" . $masomo [0] . "," . $masomo[1] . "," . $masomo[3]. "," . $masomo[4]. "," . $masomo[5]. "," . ".";
Hii itakupa matokeo
ninasomahisabati,sayansi,uraina,kiingereza,.
Hapo kwa kutumia variabl ilitakiwa tuweke kila kimoja hapo na variable yake. Mfano hapo tungepata variable 5, yaani
$masomo = “sayansiâ€;
$masomo = “kiswahiliâ€;
Na kuendelea. Hivyo kwa kutumia array tumeweza kupunguza kazi. Kwa kutumia array unaweza kuwa na list ya vitu hata 1000 kwenye array moja na ukakiweka kila kimoja unapotaka kwa kuangalia index namba ya ke kwa kuanzia 0.
KANUNI YA KUTENGENEZA ARRAY:
Kutengeneza array tunatumia function ya array (); kisha ndani yake ndipo zitafata hizo string ambazo kila moja hutenganishwa kwa kutumia , koma. String ya kwanz akatika array ndio array ya kwanza kuhesabiwa ambayo itakuwa ni namba 0, na inayofata itapewa namba 1.
Kuesabu jumla ya array
Kufanya hivi tutatumia function ya count() mfano.
<?php
$masomo = array("hisabati", "sayansi", "maarifa", "kiswahili", "uraina", "kiingereza");
echo count($masomo);
?>
Hii itakupa jibu 6, ina maana ndani yake kuna array sita ambazo zimeanza kuhesabiwa kutoka 0,1,2,3,4,5. hapa unapata jumla ya sita.
Pia unaweza kuonyesha array zote bila hata ya juzitajia nmba zao kama ilivyo kwenye mfano wa kwanza.
<?php
$masomo = array("hisabati", "sayansi", "maarifa", "kiswahili", "uraina", "kiingereza");
$arrlength = count($masomo);
for ($a = 0; $a < $arrlength; $a++){
echo $masomo [$a];
}
?>
Hii itakuletea matokeo
Hisabatisayansimaarifakiswahiliurainakiingereza
Tutajifunza zaidi juu ya kufanya hivi katika muendelezo wa masomo haya.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-10-18 Download PDF Share on facebook WhatsApp