Katika post hii utakwenda kujifunza jinsi ya kutuma email kwa kutumia php function ya email()
KUTUMA EMAIL:
Katika somo hili tunakqenda kujifunza jinsi ya kutuma email kwa kutumia php. Kuna njia kama tatu za kutuma email kwa kutumia php. Ila katika somo hili .nitakufundisha njia moja ambayo ni kwa kutumai mail().
Njia hii ni nyepesi, ila itahitaji uwe umeshahost. Haifanyikazi kwenye localhost. Hivyo hakikisha unahost faili lako live ndipo liweze kufanya kazi.
Function hii ina sehemu kuu tano yaani parameta 5 ambazo ni:-
To
From
Header
Message
Subject
To hii itabeba email ya mpokeaji wa hiyo email. From hutumika kubeba email ya mtumaji. Header hii hubeba meta information.kama wapi ukumbe umetoka, na wapi utaweza ku reply. Massage hapa ndipo ambapo utaandika meseji yako. Subject hubeba kicha cha habari.
Mfano:
mail($to,$subject,$message, $headers)
Wacha tuone jinsi ya kutuma plain text email:
<?php
$from = "non-reply@bongoclass.com";
$to = "josh@example.com";
$subject = "greetings from Bongoclass";
$message = "haloo karibu bongoclass";
$headers = "From:" . $from;
if(mail($to,$subject,$message, $headers)) {
echo "Email imetumwa";
} else {
echo "Email imeshindwa kwenda";
}
?>
Hapo kwenye josh@example.com utaweka emaili ya unayemtumia na hapo kwenye non-reply@bongoclass.com utaweka emaili ya mtumaji. Nimrtumia if() ili kcheki kama ujumbe umetumwa ama laa. Kama umetumwa basi italeta ujumbe kuwa email imetuwa.
Soma post nzima hapa
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-11-14 Download PDF Share on facebook WhatsApp