Katika somo hli utakwend akujifunza kuhusu loop kwenye Dart. Loop zimegawanyika katika makundi mnne ambayo ni for loop, while loop, for in loop na do while loop.
For loop
Hii ni moja katika njia ya kurun code mara nyingi zaidi kulingana na masharti husika. For loop hutumika kama unaelewa ni mara ngapi code zako zinatakiwa ku run. Tuchukulie mfano tunataka kutengeneza tebo ya 7. Hapa code zetu zita run mara 12.
Jinsi ya kuandika for loop
For (initialization ; condition; increment/decrement){
Code
}
Kama unavyoona hapo kwanza utaanza na keyword for ikifuatiwa na mabano ambayo ndani yake utaanza na initial huu ni mwnzo ambapo program yako inatakiwa kuanza ku run..
Baada ya initialization itafuata kuweka condition yaabu sharti ambalo code zako zitaliangalia. Utatenganisha initialization na condition kwa kutumia alama hii ( ; ). Kisha itafuata increment au decrement. Operator. Kisha utaweka mabano {} ambayo ndani yake ndipo utaweka hizo code zitakazofanya kazi.
void main() {
print('TEBO YA 7');
for (int x = 1; x <=12; x++){
print(7*x);
}
}
Kuna namna zaidi tunaweza kuboresha code zetu. Ni kwa kutumia ${} hii hutumika kuweza kutumia interpolation (rejea string interpolation kwenye somo la type of data).
void main() {
print('TEBO YA 7');
for (int x = 1; x <=12; x++){
print('${x}*7 =${x*7}');
}
}
For in loop
Hii hutumika kwenye list, object au map. Tofauti na for loop ambayo inawekewa condition. Hii yenyewe inafanya kinachotakiw akwenye list husika.
Kanuni ya kuandika for in loop
for (var in expression) {
code
}
Kama unavyoona hapo kwanza utaanza na keyword for ilifuatiwa na mabano () ndani yake utaanza na intializationa kama tulivyoona hapo mwanzo kisha itafuatiwa na keyword in baadaye utaweka hiyo data yako.
void main() {
print('TEBO YA 7');
var tebo = [7,14,21,28,35,42,49,56,63,70,77,84];
for(var x in tebo){
print(x);
}
}
Sio tu ku print hiyo list bali pia tunaweza kuifanyia mahesabu kama tulivyofanya kwenye for loop.
void main() {
print('TEBO YA 7');
var tebo = [1,2,3,4,5,6,7,8,9,10,11,12];
for(var x in tebo){
print(x *7);
}
}
void main() {
print('TEBO YA 7');
var tebo = [1,2,3,4,5,6,7,8,9,10,11,12];
for(var x in tebo){
print('${x} *7= x*7');
}
}
Mwisho:
Unaweza kufanyia kazi aina nyigine za data, ama kutengeneza mifano zaidi na zaidi. Somo linalofuata tutakwenda kujifunza kuhusu while loop.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-11-21 Download PDF Share on facebook WhatsApp