Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu switch case na jinsi inavyofanya kazi kwenye Dart.
Katika somo hili tutakwenda kutumia mifano yetu ya somo lililotangulia ili kuweza kujienga uelewa zaidi.
Jinsi ya kuandika switch case
switch(expression){
Case value:
Code
break
}
Ukiangalia hapo ni kuwa utaanza na keyword switch utaweka mabano () kama kawaid ndani yake ni value tunayotaka ku test ikufuatiwa na mabano {}. Kisha utaweka keyword case ikifuatiwa na sharti unayotaka ku test kisha utawka nukta pacha ( : ). Baad aya hapo ni code ambazo zita run kisa utaweka keyword break kwa akiji ya ku stop code zisiendelee ku run
Wacha tuone mambo yanavyokuwa:
Tunataka ikiwa umri wa mtoto ni miaka 7 aambiwe aende shule.
void main() {
var umri = 7;
switch(umri){
case 7:
print('aende shule');
break;
}
}
Sasa tunataka kama ni chini ya kiaka 7 aambwe hajafika umri, na kama miaka 7 aambiwe aende shule, na kama ni miaka 13 au zaidi aambiwe aende mmemkwa. Tutakwenda ku test miaka 10
void main() {
var umri = 10;
switch(umri){
case <7:
print('aende chekechea');
break;
case ==7:
print('aende shule');
break;
case >=13:
print('aende memkwa');
break;
}
}
Hapo utaona hakuna matokeo yeyote. Ni kwa sababu 10 haopo kwenye test zetu. Kwahiyo hapo tunatakiwa kuweka default yaani tuweke code ambazo zitafanya kazi ikiwa sharti hata moja halijafikiwa.
Sasa tunataka ikiwa hakuna sharti lolote lililofikiwa basi iseme umesha je umesoma?
void main() {
var umri = 10;
switch(umri){
case <7:
print('aende chekechea');
case ==7:
print('aende shule');
break;
case >=13:
print('aende memkwa');
break;
default:
print('je umesoma?');
}
}
Hakuna ukomo wa kutumia switch case unaweza kutumia zaidi na zaidi. Miongoni mwa fgaida zake ni kuwa ni rahisi kuitumia, na inapunguza mrundikano wa code nyingi kuliko kwenye if else else if.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-11-21 Download PDF Share on facebook WhatsApp