Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu namna ambavyo program inaweza kufanya maamuzi kulingana na mashart fulani.ama namna ambavyo program inaweza ku run code zaii ya mara moja kulingana na mashart. Hapa tutazingumzia flow of control statement
Ili uweze kwanza kuelewa somo hili nitakupa case hapa mbili.
Case 1: umetkiwa ktengeneza program kwa ajili ya menyu ya chakula chuleni. Unatakiwa program hiyo inapofika muda wa kula asubuhi saa 4 iseme chakula cha asubuhi kipo tayari na wakati wa mchana saa 7 iseme chakula cha mchana kipo tayari na inapofika jioni saa 1 usiku iseme chakula cha usiku kipo tayari mwisho inapofika saa 4 usiku iseme mlale salama.
Kwa hiyo hapo utaona tumeweka masharti kulingana na saa. Shari la kwanza ifike saa 4 asubuhi ndipo iseme chakula cha subuhi kipo tayari… na kuendelea masharti mengine. Hii ndio tunaita descision making
Case 2: umetakiwa kutengeneza table (zile tabo za kuzidisha katika somo la hesabu) ya 2 kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la tatu. Sasa badala ya kuandika moja moja utahitaji program yako iandike yenyewe. Hapa ndio tunaita loop .mfano mzui wa loop ni music player, kwamba unawez akuchaguwa mziki ujirudie rudie mara ngapii.
Flow statemenet zimegawanyika katika makundi makuu matatu ambayo ni:-
Hii ni sawa na neno la kiswahiki ikiwa. Kwa mfano tunasema ikiwa umri wa mtoto ni miaka 7 program iseme aende shule. Sawa ngoja tuone jinsi ya kufanya program yetu itumie sharti hili.
Jinsi ya kuandika descision making statemen
If ( weka sharti) {
Weka code
}
Kama unavyoona hapo kwanza utaanza na keyword if likifuatiwa na na mabano () ndani ya mabano hayo weka charti lako. Ambapo ni umri wa mtoto iwe miaka 7. Kisha utaweka mabano {} ambapo ndani ya mabani hayo utaweka nini kitokee kama sharti limefikiwa. Kwa mujibu wa mfano wetu hap tunataka program iseme aende shule. Sasa wacha tuone jinsi ya kuandika hizo code.
Kwanza tutaanz akuweka variable yetu ambayoiabeba umri wa mtoto. Kisha tutaweka charti letu .
void main() {
var umri = 7;
if(umri == 7){
print('aende shule');
}
}
Sasa tunataka kusema ikiwa umri wa mtoto ni zaidi ama sawasawa na miaka 7 iseme aende shule.
void main() {
var umri = 7;
if(umri >= 7){
print('aende shule');
}
}
Unaweza kutumia naoperator nyingine kama <, 1=, <= na nyinginezo kufanya mazoezi zadi.
Sasa hapo kuna tatizo kama umriutakuwa ni chini ya saba hakuna chochote program itasema . hapa sasa tutahitaji else satatement, ambayo itaangalia ikiwa umri ni miaka 7 iseme aende shule lakini ikiwa ni tofauti na miaka 7 iseme hajafikia umri. Kufanya hivi tutafuata formla hii
If (sharti) {
Code
}else{
Code
}
Ukiangalia vyeama hapo utaona kuna keyword ya esle imeongezeka. Hii ndio ambayo itatoa nini kifanyike kama sharti halikufikiwa.
void main() {
var umri = 3;
if(umri == 7){
print('aende shule');
}else{
print('hajafikia umri');
}
}
Hapo nimebadili umri sasa nimeweka mika 3. Umeona hapo program yetu imesea hajafikia umri. Ila kuna tatizo lingine hapo kama ukiweka umri mika zaidi ya saba pia itasema hajafikiaumri.
void main() {
var umri = 18;
if(umri == 7){
print('aende shule');
}else{
print('hajafikia umri');
}
}
Utaona hapo nimeweka miaka 18 lakini bado naabiwa hajafikia umri. Kutatua tatizo hili tatatakiwa tuwe na mlolongo mzuri. Kwa mfano tuseme
Ikiwa umri ni chini ya miaka 7 iseme hajafikia umri, na ikiwa ni miaka 7 iseme aende shule. Na ikiwa ni zaidi ya miaka saba iseme umri ni mubwa zaidi.ukiangalia vyema hapo kuna masharti mawili. Sasa kutekeleza hili ndipo tutahitaji kutumia else if. Kanuni yake ni hii
if(sharti la 1){
Code
}elseif(shari la 2){
Code
}else{
Code
}
void main() {
var umri = 18;
if(umri < 7){
print('hajafikia umri');
}else if(umri == 7){
print('aende shule');
}else{
print('umri ni mubwa zad');
}
}
Unaweza kuongeza masharti mengi zaid bila kikomo. Wacha tuone mfano mwingine. Hapo kwenye program yetu mwenye umri zaidi ya mika 7 inasema anaumri mkubwa zaidi. Sasa tunataka ikiwa umri ni zaidi ya kiaka 7 na ni chni ya miaka 14 basi program iseme ukaanze memkwa, vinginevyo ndipo iseme umri ni mkubwa zaidi. Tutakwenda kutest kwa umri wa miaka 10.
void main() {
var umri = 10;
if(umri < 7){
print('hajafikia umri');
}else if(umri == 7){
print('aende shule');
}else if (umri >7 && umri<= 14){
print('akaanze memkwa');
}else{
print('umri ni mubwa zad');
}
}
Endelea kufanyia kazi operator tulizozisoma kwenye haya mashari. Umeona hapo nimetumia operator <=, >, na &&. Jambo la msingi kuzingatia ni kuwa hakuna ukmo wa kutumia else if ama if yeyewe unawez akuzitumia zaidi na zaidi.
Mwisho:
Katika somo linalofuata tutakwenda kujifunza kuhusu switch case.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-11-20 Download PDF Share on facebook WhatsApp