DART somo la 6: Dart operator na jinsi zinavyofanya kazi.
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu operator kwenye Dart, kazi zake na jinsi ya kuzitumia.
Operator ni nini?
Operator hizi ni aalama ambazo hutumikakwa ajili ya kubadili value ama kufanya mahesabu mbalimbali. Ukisha elewa maana ya operator itakubidi uelewe maana ya operand. Sasa ili uelewe vyema viwili hivi nitakupa mfano:
2 + 3 = 5 katika mfano huu namda 2 na 3 ni operand na namba alama ya kujumlisha (+) ni operator. Operator zimegawanyika katika makundi mbalimbali ambayo ni
Arithmetic operator
Assignment operator
Relational operator
Type test operator
Logical operator
Bitwise operator
Conditional operator
Casecade notational operator
Katika somo hili tutakwenda kuiangalia aina moja ya operator ambayo ni arithmetic operator.
ARITHMETIC OPERATOR
Operator hizi ni zile ambazo tumezoea katika matendo ya hesabu. Ambazo ni
Substruction ( - ) Hutumika kutoa mfano 10 - 4 = 6
Divide ( / ) hutumika kugawanya mfano 10 / 5 = 2
Multiplication ( * ) hii hutumika kuzidisha mfano 3 * 6 = 18
Modulus ( % ) hii ni sawa na kugawanya ila badala ya kutoa jibu itatoa namba iliyobaki. Mfano 10 % 3 jibu ni 1. Hii inakupa namba iliyobaki.
Division ( ~/) hii hutumika kugawanya ila yenyewe itakupa jibu tu pila ya kuleta desimali kama kuna kilichobaki. Mfano 10 ~/3 hapa jibu ni 3. Bila ya kuleta desiali
Urinary minus ( -() ). Hii hutumika kubadili alama iliyopo kwenye operand. Kama ni negative inakuwa positive na kama ni positive inakuwa negative. Mfano - (10 - 4) = -6 utaona hapo jibu ni - 6 kwa kuwa tumebadli 10 kutoka positive kuwa negative. Kisha tukatoa negative 10 kutoa negative 4 jibu negative 6.
Agalia mfano hapo chini
void main() {
print(5 + 6);
print(7 - 5);
print(10 / 3);
print(10 ~/ 3);
print(10 % 3);
print(-8 - 4);
print(3 * 4);
}
URINARY OPERATOR
Hizi ni operator ambazo zinafanya kazi ya incrementon ( ++ ) na decrementation ( – - ) kwenye value. Kufanya increment ni kuongeza namba moja kwenye value. Mfano ++20 inakuwa 21. Na decrement ni kutoa namba moja kwenye value. Mfano - - 20 inakuwa 19.
Sasa kwenye Dart kuna post na pre. Unaposema post maana yake hizi alama zinakaa mbele ya value na kazi yake ni kutuma namba halisi kabla ya increment ama decrement mfano 20++ hapa itakupa jibu 20 kwa kuwa ndio namba halisi kabla ya increment. Na 10 - - itakupa jibu 10 kwa kuwa ndio namba halisi kabla ya decrement.
void main() {
var a, b, c, d;
a = 10;
b= 20;
c = 30;
d = 14;
print(a++);
print(++b);
print(c--);
print(--d);
}
ASSIGNMENT OPERATOR
Hizi ni operator ambazo hutumika kwa ajili ya kuipa variable thamani yaani value. Hapo awali tuisha jifunza alama ya ( = ) katika kuipa variable value yake. Sasa hapa tutakwend akuchanganya na operator nyingine ili kuweza ku assign value kwenye variable:-
Miongoni kwa assignment opetaror ni kama :-
Assignment operator ( =) hiitumesha izungumzia
Add and assign ( +=) hii kari yake ni kuongeza value operand ya kulia kwenye value ya operand ya kushoto. Mfano a = 3 na b = 4 sasa kama nitaandika hivi a += b hap a ndio operand ya kushoto na b ndio operand ya kulia ina maana sawa na kuandika hivi a = b + a. Ambapo sasa a itapata value mpya ambayo ni 7.
Substract and assign (- =). Hii yenyewe itatoa value kwenye operant ya kushto na kurudisha value kwenye operand ya kushoto. Mfano a 10, b = 4 hivyo nikiandika x - = y ni sawana kuandiak x = x - y hivyo value mpya ya variable x ni 6
Multiplay and assign ( * =) mfano k = 10, j = 2 hivyo nikiandika k * = j ni sawa na kuandiaka k = k *j hivyovalue mpya ya variable k itakuwa 20
Divide and assign ( /=) mfano c = 8, d = 4 hivyo c/=d ni sawa na kuandika c = c/d abapo value mpya ya variable d itakuwa 2.
Divide and assign ( ~/=) e = 10, f = 3 hivyo e ~/=f ni sawa na kuandiiak e = e~/f ambapo value mpya ya variable e itakuwa ni 3
Mod and assign ( %=) g = 10, h = 3 hivyo g %=f ni sawa na kuandika g = g %f ambapo value mpya ya variable g ni 1
void main() {
var a = 4;
var b = 3;
a +=b;
print(a);
var x = 10;
var y = 4;
x -=y;
print(x);
var k = 10;
var j = 2;
k *=j;
print(k);
dynamic c = 8;
var d = 4;
c /=d;
print(c);
var e = 10;
var f = 3;
e ~/=f;
print(e);
var g = 10;
var h = 3;
g %=h;
print(g);
}
RELATIONAL OPERATOR
Hizi ni operator ambazo zinaonyesha mahusiano yaliyopo kwenye item katia program. Hizi zinatupa true ama false. Operator hizi zinaweza kuwa:-
Kubwa kuliko ( > ) mfano 5 > 4 ina maana 5 ni kubw akuliko 4. Hapa ni true
Ndogo kuliko ( < ) mfano 5 < 4 ina maana 4 ni ndogo kuliko 4. Hapa ni false
Kubwa kuliko ama sawasawa (>=) mfano 5 >= 4 hii ina maana 5 ni kubwa kulio 4 au ni sawasawa. Hapa ni true
Ndogo kuliko ama sawasawa (<=) mfano 5 <= 4 hii ni false
Sawasawa ( ==) hii huonesha kuwa item 2 zipo sawasawa. Mfano 5 == 5 hii ina 5 ni sawasawa na 5 hii ni true
Si sawasawa ( != ) mfano 5 != 5 hii ina maana 5 sio sawasawa na 5 hii false
void main() {
print(5 > 4);
print(5 < 4);
print(5 >= 5);
print(5 <= 5);
print(5 == 5);
print(5 != 5);
}
LOGICAL OPERATOR
Hizi hutumika kwenye bool data type.
AND ( &&)
OR ( || )
NOT ( ! )
void main() {
print(true || false);
print(true && false);
print(false || true);
print(false && true);
print(true && true);
print(false && false);
}
Operator nyinginezo tutazisoma kidogo kidogo kadiri somo linavyoendelea.
Mwisho:
Katika somo linalofuata tutakwenda kujifunzakuhusu control flow tutakwend akujifunz akuhusu kuweka mashart kwenye program.