Katika somo lililopita tumejifunza kuhusu sintaksia za dart. Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutengeneza variable kwenye Dart.
Nini maana ya variable?
Variable ni jina ambalo hutumika kuhifadhia data kwenye program. Jina la variable huitwa identifier. Kwa mfano ukisema x = 6 yaani x ni sawa na 6. Hivyo tunasema x ni variable ambayo inahifadhi 6
Sheria za variable:
Jinsi ya kuandika variable:
Kwanza utaanza na jina la variable (identifier) ikifuatiwa na alama ya (=) ikifuatiwa na value ya hiyo variable. Wakati mwingine utaanza na kutaja aina ya data ikifuatiwa na jina la vaiable likifuatiwa na alama ya (=) ikifuatiwa na value
Kwenye Dart kuna njia njingi za kuandika variable kuliko baadhi ya luga nyinginezo:-
Mfano
void main(){
var web = 'bongoclass';
print(web);
}
Wakati mwingine kwa sababu za ki usalama utahitaji aina maalumu ya data kwenye variable yako. Hapa utataja aina ya data moja kwa moja
void main() {
String web = 'bongoclass';
print(web);
}
Kama ukiweka aina nyingine iliyo tofauti, na ambayo umeitaja itakuletea error. Angalia mfano hapo chini
import 'dart:ffi';
void main() {
Int web = 'bongoclass';
print(web);
}
Hapo kuna error kwa sababu aina ya data nilio target ni int yaani namba lakini value nilioweka ni string.
Pia unaweza kutengeneza variable zaidi ya moja kwenye mstari mmoja kwa kutumia aina ya data moja. Angalia mfano hapo chini variable a, b na c ni int yaani namba. Zote nimezitengeneza kwa pamoja.
void main() {
int a, b, c;
a = 5;
b = 10;
c = 2;
print(a +b +c);
}
Hapo jibu ni 17
Pia unaweza kubadili value ya variable kwa kuitumia tena. Ila hakikisha type of data inabakia ile ile kama umetumia var.
void main() {
var x = 3;
x = 4;
print(x);
}
Wakati mwingine unahitaji variable iweze kutumika zaidi ya mara moja kwa value tofauti tofauti na aina tofauti tofauti za data Hapa tutatumia dynamic. Tofauti iliyopo kati ya dynamic na var ni kuwa unapotumia jina la variable kwenye var huhusiwi kubadili aina ya data. Ila unapotumia dynamic hilo jina linaweza kutumiwa tena na kubadili value.
void main() {
dynamic x = 'haloo';
print(x);
x = ['hi', 'hujambo'];
print(x[1]);
x = {'salamu':'habari'};
print(x);
}
Mfano kama huo ukitumia var hauwezi kuleta matokei hayo.
void main() {
var x = 'haloo';
print(x);
x = ['hi', 'hujambo'];
print(x[1]);
x = {'salamu':'habari'};
print(x);
}
Final na const
Hizi ni keyword nyingine ambazo utumika katika kutengenezea (declare) constant. Contant ni kama variable zilivyo ila utofauti wake mkubwa ni kuwa constst haiwezi kubadilika. Yaani unapotumia jina kuwakilisha value huwezi kulitumia tena jina hilo. Yaani jina la hiyo variable haliwezi kutumika tena.
void main() {
const web = 'bongoclass';
final site = 'google';
print(web);
print(site);
}
Huwezi tena kufanya kama ambavyo tulifanya kwenye var na dynamic. Itakupa error.
void main() {
const web = 'bongoclass';
web = 'youtube';
final site = 'google';
site = 'microsoft';
print(web);
print(site);
}
Hapo utagundua kuwa final na const maana zao zinakaribiana sana. Ila utofauti ni kuwa const value yake una uhakika nayo kuwa haitabadilika wakati wa ku run code. Kwa mfano unajuwa kuwa unga kipishori kimoja ni kilo 25. Una uhakika na vlue na unaijuwa hapo tutatumia const.
Ila kama hauijui value hapa utatumia final. Kwa mfano kama data zinatoka kwenye API hapa kua uwezekano mkubwa wa data kuwa na mabadiliko muda wowote kwa kuwa huwenda wewe so mmiliki wa hizo data. Ama mfano mzuri ni muda, unaweza kubadilika kila wakati. Hivyo hapa utatumia final.
Mwisho:
Somo linalofuata tutakwenda kujifunza kuhusu Dart keywords
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-11-18 Download PDF Share on facebook WhatsApp