Katika somo hili utakwenda kujifunza aina za data zinazotumika kwenye Dart.
Dart ni kama lugha nyinginezo za kompyuta, karibia aina za data zinazotumuka kwenye dart ni sawa katika language nyinginezo. Aina hizo za data ni :-
Namaba zinaweza kuwa ni int yaani namba nzima ama double yaani namba zenye desimali.
void main(){
print(2);
print(1.5);
}
Hizi ni data zilizo katika mfumo wa mchanganyiko wa herufi, namba, na alama za uandishi. String huandikwa ndani ya alama za funga na fungua semi mbili (“) ama moja (‘). Jambo la kuzingatia ni kuwa utakayoa anza nayo ndio umalizie nayo. Yaani ukitumia (“) mwanzo basi na mwisho utumie (“)
void main(){
print("bongoclass");
print('info@example.com');
print("#@?");
}
Pia unaweza kuunganisha string zaidi ya moja yaani kufanya concatnation. Kuna njia 3 ambazo hutumika kuunganisa string zaidi ya moja. Njia hizo ni kama
void main(){
//concatnation kwa kutumia +
print("karibu "+"Bongoclass");
//kwa kucha nafasi kati ya string mbili
print('karibu ' 'Bongoclass');
//kufanya interpolation
//x ni variable. Tutajifunza zaidi kwenye somo lijalo
var x = 'bongoclass';
print('karibu ${x}');
}
Kwenye string unaweza ku break line kwa kutumia back slash () ikifuatiwa na herufi n hii ni sawa na matumizi ya <br> kwenye html
void main(){
print(' karibu bongoclass upate kujifunza');
}
Kuna changamoto nyingine angalia mfano huu
void main(){
print("mama anauza ng'ombe");
}
Hapa utaona hakuna error. Ila sasa wacha tutumia single quotation mark (‘)
void main(){
print('mama anauza ng'ombe');
}
Hapo kwenye neno ng’ombe hiyo alama ya apostroph (‘) haiwezi kuendana na hizo funga semi. Hivyo kutatua tatizo hilo tutatumia back slash ().
void main(){
print('mama anauza ng'ombe');
}
3. List
Hizi ni data zilizo katika orodha ya vitu vingi. List huandikwa kwenye mabano [ ]. Tunaweza kuitumia kila data iliyo ndani ya list kivyake kwa kutumia indexing. Tutakuja kujifunza zaidi kuhusu undexing.
void main(){
print([1,2,3,4,5]);
print(['bongoclass', 'google', 'facebook']);
var x = ['Tanzania', 'Kenya', 'Uganda'];
print(x);
print(x[1]);
}
4. Boolean
Hizi ni data zenye majibu mawili tu yaani True na False. Ni sawa na kusema On na off.
Mfano 2 ni kubwa kuliko 1 hivyo jibu ni kweli.
void main(){
print(2 >1);
}
5. Map
Data hizi zinafanana kidogo na list. Tofauti ni kuwa zenyewe zipo kama na pea kuna key na value. Ila key haitakiwi kufanana na nyingine. Data hizi zinakuwa kwenye mabano haya {} tofauti na list ambazo zilitumia mabani haya ().
Ili uweze kuandika map utaanz ana mabano {} kisha utaweka key ya hiyodata. Kama ni string itakaa ndani ya zile alama za finga na funguwa semi. Kisha itafuatiwa na nukta pacha (:) kisha utaandika value yaani thamani ya hiyo data. Kutenganisha itemmoja na nyingine utatumia alama ya koma (,)
Unapotaka kuitumia item yeyote kwenye list tutatumia key yake. Kwa mfano angalia jinsi nilivyo display jina la juma kmwey mfano hapo chini.
void main(){
print({'jina':'Bongoclass','umri':6, "status":'live' });
var x = {'jina': 'juma', 'umri': 35, 'uraia': 'Tanzania'};
print(x['jina']);
}
6. Runes
Hii hutumika pale unapotaka ku display symbol kwa mfano zile emoj. Hapa tutatumia alama ya back slash.
void main(){
print('u2665');
print('u{1f600}');
}
Jinsi ya kujuwa aina ya data iliyotumika
Kufanya hivi tutatumia runtimeType Angalia mfano hapo chini.
void main() {
print(2.runtimeType);
print("haloo".runtimeType);
print(2.9.runtimeType);
print(true.runtimeType);
print([2,'tatu', 4].runtimeType);
print({'jina':'bongoclass'}.runtimeType);
}
Mwisho
Tukutane somo linalofuata titakwenda kujifunza kuhusu variable.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-11-18 Download PDF Share on facebook WhatsApp