Katika somo hili tutatkwenda kuziona baadhi ya xyntax yaani kanunu za uandishi wa code za dart.
Somo letu litakwenda kuanzia kwenye program ya kwanza kabisa ya Hello World copi code hapo chini kisa zi pest kwenye dart editor inayotumia kisha bofya batani ya ku excute code ama ku run code.
Void main(){
print('Hello World');
}
Kama uta run code hizo utapata majibu haya Hello World
Sasa somo letu linaanzia hapa.
File extension ya dart ni .dart.
Dart inatumia mfumo kama baadhi ya programming lnaguage nyingine kama java. Kwamba mwanzo wa program ni kwenye function ya main(). Hapa ndipo panapoanziwa program ya dart. Kwa kuwa function yetu hai return data ndio maana hapo mwanzo kumeanza na meno void kama linavyosomeka hapo void main(){}. Hata hivyo unaweza kuondoa neno void na bado program yetu ika run vyema.
Ukiangalia vyema hao utaona kuna mabano {} baada ya neno main(). Ipo hivi neno main ni jina la function na ndani ya badno () hapo kutakaa parameter nyingine zo za function na ndani ya mabano {} kutakaa code abazo zinatakiwa zifanye kazi endapo program ita run.
Utaona hapo ndani ya mabano ya {} kuna code zinasomeka print('Hello World');
Hizi ni code ambazo zitatakiwa kufanya kazi wakati program yetu ina run. Sasa hapo kuna function nyingine ya print(). Hii ni kwa ajili ya ku print text kwenye screen. Wacha nikupe mfano mwingine.
main(){
print(3 + 6);
}
Hapo umeona tumetumia mahesabu sasa tume jumlisha 3 na 6. Pia tumeondoa neno void. Katika mifano yetu hiyo miwili neno print, main, void hufahamika kama keyword.
Dart hutumia semicolon ili kutenganisha statement moja na nyingine. Kama ilivyo kwenye lugha nyingine. Angalia mfano huu
main(){
print('Karibu Bongoclass')
}
Hapo uki run hizo code utapata error kwa sababu hakuna semicolon kwenye function ya print. Ilitakiwa iwe print('Karibu Bongoclass');
Hivyo basi ni muhimu kuzingatia matumizi ya semicolon kwenye Dart kama ilivyo kwenye lugha nyingine.
Dart haiangalii mistari ilioachwa wazi. Unaweza kuruka nafasi kadiri unavyotaka hakuna tatizo. Program yenyewe itakwenda kuangalia code na sio nafasi. Dart inazingatia bnafasi moja tu ili kuppisha keyword na keyword nyingine. Kwa mfano hapo kama hutaacha nafasi kutoka kwenye neno void na neno main program yako itakuwa na shida
voidmain(){
print('Karibu Bongoclass');
}
Hiyo program hapo haiwezi ku run kwa kuwa ina matatizo.
Ili kuweka comment dart inatumia alama ya backslash mbili yaani (//) kwa ajili ya comment ya mstari mmoja. Na kama comment yako ni paragraph yaani mistari zaidi ya mmoja utatumia /* */.
Comment hutumuka kuweka kumbukumbu kwenye code ama kutoa maelekezo kwa watakaokuja kutumia hizo code. Comment hazihusiki kwenye kufanya program ifanye kazi. Comment hazitokei kwenye screen.
Mfano wa comment za single line
//mwanzo wa program
void main(){
//print text kwenye screen
print('Karibu Bongoclass');
}
Mfano wa comment za mistari zaidi ya mmoja
//mwanzo wa program
void main(){
/*huu ni mfano wa
comment ambazo zina mistari
zaidi ya mmoja
*/
print('Karibu Bongoclass');
}
Pia kuan aina nyingine za comment ambazo hutumia ///. Hizi utumika kwenye kufanya documentation ya program. Mara nyingi hizi hutumika kama unatengeneza kibrary.
7. Case sensitivity
Dart ni case sensitivity kwa maana kuwa husingatia matumizi ya herufi ndogo na kubwa. Kwa mfano neno Print na neno print ni tofauti. Kwa sababu hilo la kwanza limeanzwa na herufi kubwa na hilo la pili ni ndogo.
Mfano
void main(){
Print('Karibu Bongoclass');
}
Hizo code hapa zitakupa error kwa sababu nimetumoia P badala ya p
Mwisho
Katika somo linalofuata tutakwenda kujifunza jinsi ya kutengeneza variable na kuziwekea value zake.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-11-16 Download PDF Share on facebook WhatsApp
Jaza maswali yote ama baadhi kisha bofya kitufe za kutuma majibu hapo chini.