DART - somo la 1: Kazi za dart programming na historia yake


imageKatika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu kazi za dart language. Pia nimekuandalia istoria fupi ya lugha ya DART.DART

Dart ni miongoni mwa general purpose programming language. Hizi ni lugha za kikompyuta ambazo hufanyabkazi maneno mengi kwa mfano kwenye web app, software, na maneno mengineyo. 

 

Hii ni course ya dart yenye lengo la kukupa ufahamu Ili iwe rahisi kuelewa matumizi ya flutter. Katika course hii tutakwenda kujifunza lugha hii pamoja na kufanyia mazoezi.

 

Maandalizi ya somo:

  1. Kwa wanaotumia kompyuta
  1. Download software ya visual studio ya Microsoft ama webstorm ya jetbrainin
  2. Nenda kwenye sehemu ya kionstall extensions tafuta dart Kisha download. Hakikisha una bando lisilopunguwa MB 500
  3. Kisha download dart sdk  hapa kisha fuata maelekezo 
  4. Baada ya hapo utaanza project mpya ya dart.

2. Kwa watumiaji wa simu

Download App ya dart compiler hapa 

Baada ya hapo utaifunguwa na kuanza kuandika code.

 

Online compiler

Kama ukiona ni changamoto ku install dart sdk unaweza kufanya majaribio online kwenye dart compiler. Cheki hapa

 

Matumizi ya dart

Dart inaweza kutumia kwa ajili ya:-

  1.  Kutengeneza website
  2. Kutengeneza web App
  3. Kutengeneza mobile app
  4. Hutumika kwenye server
  5. Kutengeneza desktop software

 

Kwa kuwa ni general purpose inaweza kufanya mambo mengi zaidi.

 

Historia fupi Dart

Dart language ikianza kudizainiwa na Lars Bak na luendelezwa na kampuni ya Google. Kwa mara ya kwanza ilitambulishwa mwaka 2011.

 

Mwaka 2013 toleo la kwanza la dart lilitambulishwa kama Dart 1.0 wakati huu kulitokea malalamiko mengi kuhusu lugha hii. Hivyo mwaka 2015 toleo la Dart 1.9 likiwa limejikita sana katika ku compile dart kuwa JavaScript. Mwaka 2018 mabadiliko zaidi yakaongezwa hasa kwenye type system na toleo hili lilitwa Dart 2.0 yaani toleo la pili. 

 

Baada ya mabadiliko zaidi toleo la 2.6 lilikuja na extension ya dart2native ambayo iliwezesha ku compile dart kwenye linux, macOS na window. Katika kipindi hiki mahusiano ya flutter na dart yakazidi kuimarika.

 

Mpaka kufikia leo 24/10/2023 tupo toleo la 3.1.4 ambalo lilitolewa mwaka 2023 tarehe 18 mwenye wa 10.

 

Mwisho:

Tukutane somo linalofuata tutajifunza kuhusu sytax za dart.

 Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Imeandikwa na Rajabu Terehe 2023-10-27 Download PDF Share on facebook WhatsApp

ZOEZI

Jaza maswali yote ama baadhi kisha bofya kitufe za kutuma majibu hapo chini.1 : Dart ilitambulishwa kwa mara ya kwanza mwaka ________

2 : Ni nani alianzisha Dart langauge ?__________

3 : Moja kati ya framework zifutatayo zinatuia Dart language _______

4 : Kampuni gani imehusika katika kuiendeleza lugha ya dart_____

5 : Moja ya yafuatayo sio matumizi ya Dart __________RELATED POSTS

picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu switch case na jinsi
picha

Katika soo hili utakwenda kujifunza kuhusu reserved keywords katika Dart
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu operator kwenye Dart, kazi
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza method yhinginge zinazofanya kazi kwenye
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kusoma na kuandika
picha

Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu while loop na do
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu function kwenye dart, jisni
picha

Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu method ambazo hutumika kwenye
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu break na continue kwenye
picha

Katika somo hli utakwend akujifunza kuhusu loop kwenye Dart. Loop
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu namna ambavyo program inaweza
picha

Katika somo hili tutakwenda kuingia ndani zaidi kwenye somo la
picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza aina za data zinazotumika kwenye
picha

Jinsi ya kuchukuwa user input kwenye Dart kwa ajili ya
picha

Katika somo hili utakwenda kuziona method za dart zinazotumika kwenye
picha

Katika somo hili tutatkwenda kuziona baadhi ya xyntax yaani kanunu