Aina za Hadith
Kuna aina kuu mbili za Hadith
- (a) Hadith Nabawiyyi.
(b) Hadith Qudusiyyi.
(a)Hadith an-Nabawiyyi
Ni usemi au habari aliyoitoa Mtume (s.a.w) kwa watu kwa maneno yake. Utazikuta Hadith za aina hii zikianza na: Amesema Mtume (s.a.w) "
Mfano wa Hadith an-Nabawiyyi:
Aysha (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah (Rehema na amani iwe juu yake) amesema: "Yoyote atakayeingiza jambo jipya katika mambo yetu (dini yetu) lisilokuwa la humu, litakataliwa." (Wamekubaliana Bukhari na Muslim)
(b)Hadith Qudusiyyi:
Ni usemi au habari aliyoitoa Mtume (s.a.w) kama alivyoipokea kutoka kwa Allah (s.w) lakini iliyo nje ya Qur-an. Hadith hizi huanza na: Amesema Mtume (s.a.w) kuwa Allah (s.w) kasema: "……."
Mfano wa Hadith Qudusiyyi:
Abu Huraira (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah (rehema na amani iwe juu yake) amesema: Allah (s.w) amesema: "Ni mwingi wa kujitosheleza kwa kiasi kwamba sihitaji mshiriki yeyote. Kwa hiyo yeyote yule atakaye fanya amali (atakayefanya jambo) kwa ajili ya mtu mwingine pamoja na Mimi Nitaikataa hiyo amali na kuipeleka kwa yule aliyenishirikisha naye." (Imesimuliwa na Muslim, hali kadhalika Ibn Majah).
Hadith Qudusiyyi ni chache sana ukizilinganisha na Hadith Nabawiyyi. Idadi yake ni Hadith mia mbili na kidogo tu.