Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili

36.Surat Ya-sin


image
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 0

image
1. Ya-Sin  1

image
2. Kwa Haki ya Qur'ani yenye hikima! 2

image
3. Hakika wewe ni miongoni mwa walio tumwa, 3

image
4. Juu ya Njia Iliyo Nyooka. 4

image
5. Uteremsho wa Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. 5

image
6. Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa , basi wao wamekuwa wenye kughafilika.6

image
7. Bila ya shaka kauli imekwisha thibiti juu ya wengi katika wao, kwa hivyo hawaamini.7

image
8. Tumeweka makongwa shingoni mwao, yakawafika videvuni. Kwa hivyo vichwa vyao viko juu tu. 8

image
9. Tumeweka kizuizi mbele yao, na kizuizi nyuma yao, na tumewafunika macho yao; kwa hivyo hawaoni. 9

image
10. Ni sawa sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawataamini. 10

image
11. Hakika wewe unamwonya mwenye kufuata ukumbusho, na akamcha Arrahman, Mwingi wa Rehema, kwa ghaibu. Basi mbashirie huyo msamaha na ujira mwema. 11

image
12. Hakika Sisi tunawafufua wafu, na tunayaandika wanayo yatanguliza, na wanayo yaacha nyuma. Na kila kitu tumekihifadhi katika daftari asli lenye kubainisha.12

image
13. Na wapigie mfano wa wakaazi wa mji walipo wafikia walio tumwa. 13

image
14. Tulipo watumia wawili, wakawakanusha. Basi tukawazidishia nguvu kwa mwingine wa tatu. Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwenu. 14

image
15. Wakasema: Nyinyi si chochote ila ni watu kama sisi. Na Mwingi wa Rehema hakuteremsha kitu. Nyinyi mnasema uwongo tu. 15

image
16. Wakasema: Mola wetu Mlezi anajua kwamba hakika sisi tumetumwa kwenu.16

image
17. Wala si juu yetu ila kufikisha ujumbe ulio wazi. 17

image
18. Wakasema: Sisi tumeagua kuwa nyinyi ni wakorofi. Ikiwa hamtaacha basi kwa yakini tutakupigeni mawe, na mtapata adhabu chungu kutoka kwetu. 18

image
19. Wakasema: Ukorofi wenu mnao wenyewe! Je! Ni kwa kuwa mnakumbushwa? Ama nyinyi ni watu walio pindukia mipaka. 19

image
20. Na akaja mtu mbio kutokea upande wa mbali wa mjini, akasema: Enyi watu wangu! Wafuateni hawa walio tumwa. 20

image
21. Wafuateni ambao hawakutakini ujira, hali ya kuwa wenyewe wameongoka. 21

image
22. NA KWA NINI nisimuabudu yule aliye niumba na kwake mtarejeshwa? 22

image
23. Je! Niishike miungu mingine badala yake? Arrahmani, Mwingi wa Rehema, akinitakia madhara uombezi wa hao hautanifaa kitu, wala hawataniokoa. 23

image
24. Basi hakika mimi hapo nitakuwa katika upotovu ulio dhaahiri. 24

image
25. Hakika mimi nimemuamini Mola wenu Mlezi, basi nisikilizeni! 25

image
26. Akaambiwa: Ingia Peponi! Akasema: Laiti kuwa watu wangu wangeli jua 26

image
27. Jinsi Mola wangu Mlezi alivyo nisamehe, na akanifanya miongoni mwa walio hishimiwa. 27

image
28. Na hatukuwateremshia kaumu yake baada yake jeshi kutoka mbinguni, wala si wenye kuteremsha. 28

image
29. Hakukuwa ila ukelele mmoja tu; na mara walizimwa! 29

image
30. Nawasikitikia waja wangu. Hawajii Mtume ila wao humkejeli.30

image
31. Je! Hawaoni umma ngapi tulizo ziangamiza kabla yao? Hakika hao hawarejei tena kwao.31

image
32. Na hapana mmoja ila wote watakusanywa waletwe mbele yetu. 32

image
33. Na Ishara hiyo kwao - ardhi iliyo kufa, nasi tukaifufua, na tukatoa ndani yake nafaka, wakawa wanazila! 33

image
34. Na tukafanya ndani yake mabustani ya mitende na mizabibu, na tukatimbua chemchem ndani yake, 34

image
35. Ili wale matunda yake, na hayo hayakufanywa na mikono yao! Basi je, hawashukuru?35

image
36. Subhana, Ametakasika, aliye umba dume na jike vyote katika vinavyo mea katika ardhi na katika nafsi zao, na katika wasivyo vijua. 36

image
37. Na usiku ni Ishara kwao. Tunauvua humo mchana, mara wao wanakuwa gizani. 37

image
38. Na jua linakwenda kwa kiwango chake. Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu, Mwenye kujua. 38

image
39. Na mwezi tumeupimia vituo, mpaka unakuwa kama karara kongwe. 39

image
40. Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia zao.40

image
41. Na ni Ishara kwao kwamba Sisi tuliwapakia dhuriya zao katika jahazi ilio sheheni. 41

image
42. Na tukawaumbia kutoka mfano wake wanavyo vipanda. 42

image
43. Na tukitaka tunawazamisha, wala hapana wa kuwasaidia, wala hawaokolewi, 43

image
44. Isipo kuwa kwa rehema zitokazo kwetu na starehe kwa muda. 44

image
45. Na wanapo ambiwa: Jilindeni na yalioko mbele yenu na yalioko nyuma yenu, ili mpate kurehemewa...45

image
46. Na haiwafikii Ishara yoyote katika Ishara za Mola wao Mlezi ila wao huwa ni wenye kuipuuza. 46

image
47. Na wanapo ambiwa: Toeni katika aliyo kupeni Mwenyezi Mungu, walio kufuru huwaambia walio amini: Je! Tuwalishe ambao Mwenyezi Mungu angependa angeli walisha mwenyewe? Nyinyi hammo ila katika upotofu ulio dhaahiri. 47

image
48. Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa nyinyi ni wakweli? 48

image
49. Hawangojei ila ukelele mmoja tu utakao wachukua nao wamo kuzozana. 49

image
50. Basi hawataweza kuusia, wala kwa watu wao hawarejei. 50

image
51. Na litapulizwa barugumu, mara watatoka makaburini wakikimbilia kwa Mola wao Mlezi. 51

image
52. Watasema: Ole wetu! Nani aliye tufufua kwenye malazi yetu? Haya ndiyo aliyo yaahidi Mwingi wa Rehema na wakasema kweli Mitume. 52

image
53. Haitakuwa ila ukelele mmoja tu, mara wote watahudhuruishwa mbele yetu. 53

image
54. Basi leo nafsi yoyote haitadhulumiwa kitu, wala hamtalipwa ila yale mliyo kuwa mkiyatenda. 54

image
55. Hakika watu wa Peponi leo wamo shughulini, wamefurahi. 55

image
56. Wao na wake zao wamo katika vivuli wameegemea juu ya viti vya fakhari.56

image
57. Watapata humo kila namna ya matunda na watapata kila watakacho kitaka.57

image
58. "Salama!" Hiyo ndiyo kauli itokayo kwa Mola Mlezi Mwenye kurehemu. 58

image
59. Na enyi wakosefu! Jitengeni leo! 59

image
50. Je! Sikuagana nanyi, enyi wanaadamu, kuwa msimuabudu Shet'ani? Hakika yeye ni adui dhaahiri kwenu.50

image
61. Na ya kwamba mniabudu Mimi? Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka. 61

image
62. Na bila ya shaka yeye amekwisha lipoteza kundi kubwa miongoni mwenu. Je, hamkuwa mkifikiri? 62

image
63. Hii basi ndiyo Jahannamu mliyo kuwa mkiahidiwa. 63

image
64. Ingieni leo kwa vile mlivyo kuwa mkikufuru. 64

image
65. Leo tunaviziba vinywa vyao, na iseme nasi mikono yao, na itoe ushahidi miguu yao kwa waliyo kuwa wakiyachuma. 65

image
66. Na tungeli penda tungeli yafutilia mbali macho yao, wakawa wanaiwania njia. Lakini wange ionaje? 66

image
67. Na tungeli taka tunge wageuza sura hapo hapo walipo, basi wasinge weza kwenda wala kurudi. 67

image
68. Na tunaye mzeesha tunamrudisha nyuma katika umbo. Basi je! hawazingatii? 68

image
69. Wala hatukumfundisha (Muhammad) mashairi, wala hayatakikani kwake hayo. Haukuwa huu ila ni ukumbusho na Qur'ani inayo bainisha. 69

image
70. Ili imwonye aliye hai, na neno litimie juu ya makafiri. 70

image
71. Je! Hawaoni kwamba tumewaumbia kutokana na iliyo fanya mikono yetu wanyama wa mifugo, na wao wakawa wenye kuwamiliki. 71

image
72. Na Sisi tukawadhalilishia. Basi baadhi yao wako wanao wapanda, na baadhi yao wanawala. 72

image
73. Na wao wanapata kwao manufaa na vinywaji. Basi je, hawashukuru? 73

image
74. Na wameishika miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu ili ati wapate kusaidiwa! 74

image
75. Hawataweza kuwasaidia. Bali hao ndio watakuwa askari wao watakao hudhurishwa. 75

image
76. Basi maneno yao yasikuhuzunishe. Hakika Sisi tunayajua wanayo yaweka siri na wanayo yatangaza. 76

image
77. Kwani mwanaadamu haoni ya kwamba Sisi tumemuumba yeye kutokana na tone la manii? Kisha sasa yeye ndio amekuwa ndiye mgomvi wa dhaahiri! 77

image
78. Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake, akasema: Ni nani huyo atakaye ihuisha mifupa nayo imekwisha mung'unyika? 78

image
79. Sema: Ataihuisha huyo huyo aliye iumba hapo mara ya mwanzo. Na Yeye ni Mjuzi wa kila kuumba. 79

image
80. Aliye kujaalieni kupata moto kutokana na mti wa kijani nanyi mkawa kwa huo mnawasha. 80

image
81. Kwani aliye ziumba mbingu na ardhi hawezi kuwaumba mfano wao? Kwani! Naye ndiye Muumbaji Mkuu, Mjuzi. 81

image
82. Hakika amri yake anapo taka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa. 82

image
73. Basi Ametakasika yule ambaye mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu; na kwake Yeye mtarejeshwa. 83


Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Ikiwa una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com 
Copyright � 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani