1. Sema: Najikinga na Mola Mlezi wa wanaadamu, Mwenye kuendesha
mambo yao.
2. Mfalme wa wanaadamu, kwa ufalme ulio timia, kuwamiliki wote
wafalme wao na maraia.
3. Mungu wa wanaadamu, Mwenye uweza kwa kuwasarifu kwa
ukamilifu atakavyo.
4. Na shari ya mwenye kutia wasiwasi watu, ambaye hurudi nyuma
ukiomba msaada kwa Mwenyezi Mungu dhidi yake.
5. Ambaye hutia kwa kificho katika vifua vya watu ya
kuwaachisha wasende kwenye njia ya uwongofu.
6. Kutokana na majini na wanaadamu.