1. Sema najikinga na Mola Mlezi wa asubuhi inapo pambazuka
kutokana na usiku.
2. Na shari ya kila chenye shari katika viumbe, ambavyo hapana
wa kuzuia shari yao ila Mwenye kumiliki amri yao.
3. Na shari ya usiku unapo kuwa totoro.
4. Na shari ya anaye pita baina ya watu kwa sababu ya
kuwafisidi.
5. Na shari ya hasidi anaye tamani iondoke neema kwa wengine.