1. Ewe Muhammad! Hao wanao sema kwa kejeli, "Tusifie Mola wako Mlezi.": waambie: Yeye ni Mwenyezi Mungu wa pekee hapana mwenginewe, wala hana mshirika.

 

2. Mwenyezi Mungu Mwenye kukusudiwa peke yake katika haja zote, na yote yanayo takikana.

 

3,4. Hana mtoto wala hakuzaliwa na baba wala mama, wala hana yeyote aliye mshabihi, au mfano wake.