1. Ikithibiti nusura ya Mwnyezi Mungu na ushindi kwako na kwa
Waumini,
2. Na ukawaona watu wanaingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu
makundi kwa makundi,
3. Basi mshukuru Mola wako Mlezi, na Sabbih' , Mtakase kwa sifa
zake, na mtake akusamehe wewe na umma wako, kwani hakika Yeye ni Mwingi wa
kupokea toba za waja wake.
Maoni ya wataalamu juu ya Surat Annas'r:-
Sura hii tukufu inaashiria kugomboka kwa Makka. Na sababu khasa iliyo
pelekea kugomboka Makka ni Maqureshi walipo vunja mkataba wa amani wa Hudaibiya
kwa kuwashambulia kabila ya Khuzaa', ambao walikuwa wana masikilizano na Mtume
s.a.w., na wakawasaidia Bani Bakri katika hayo. Yalipo tokea hayo Mtume akaona
waliyo yafanya Maqureshi kuvunja mapatano imembidi ende kuigomboa Makka. Basi
akakusanya jeshi la nguvu lenye wapiganaji elfu kumi. Akenda mwezi wa Ramadhani
katika mwaka wa nane wa Hijra (Desemba mwaka 630 B.K.) Akawazuia watu wake
wasipigane ila wakilazimishwa. Na Mwenyezi Mungu alipenda aingie Nabii na jeshi
lake Makka bila ya vita. Na kwa hivi akapata ushindi mkubwa kabisa katika
taarikhi ya wito wa Kiislamu, bila ya vita. Na Mwenyezi Mungu akamwezesha
kusimamisha dola ya kwanza duniani bila ya vita na bila ya kumwagwa damu.
Na huo ugombozi wa Makka ulikuwa na athari za kufikia mbali kwa pande za
Dini na siyasa, kwani ilikuwa ni kuung'oa upagani, kuabudu masanamu, katika
ngome yake kubwa, kwa kuvunjwa masanamu yaliyo simamishwa katika Al-kaaba, na
yakaondolewa mapicha na masanamu yaliyo kuwemo.
Na kwa kuingia Makka
kwenye boma la Uislamu Nabii s.a.w. aliweza kuzishinda kabila zote zilizo bakia
katika Hijazi, ambazo zilizo kuwa zina kani za kijahiliya, kama Hawazan na
Thaqif. Mwenyezi Mungu akamwezesha kusimamisha dola si juu ya kabila wala nchi
bali juu ya Imani, nayo ni Imani ya Kiislamu, na bendera ya Kiislamu