1. Ewe Muhammad! Sema: Enyi makafiri, mlio shikilia juu ya
ukafiri wenu.
2. Mimi simuabudu mnaye muabudu nyinyi badala ya Mwenyezi
Mungu.
3. Wala nyinyi si wenye kumuabudu huyo ambaye mimi namuabudu,
naye ni Mwenyezi Mungu wa pekee.
4. Wala mimi si mwenye kuabudu mfano wa ibada yenu, kwani
nyinyi ni washirikina.
5. Wala nyinyi si wenye kuabudu mfano wa ibada yangu, kwani hii
ni Tawhidi, ibada ya Mungu Mmoja.
6. Nyinyi mna dini yenu mnayo itakidi, na mimi nina Dini yangu aliyo niteulia Mwenyezi Mungu niishike.