1. Unamjua anaye kanusha malipo na hisabu ya Akhera?

 

2,3. Ukitaka kumjua basi ni huyo ambaye anaye msukuma yatima kwa nguvu, na anamtumilia mabavu, na anamdhulumu, na wala hahimizi kulishwa masikini.

 

4,5. Maangamio yatawashukia wanao sali na wakasifika kwa sifa hizi, na wakaghafilika na Sala zao wasinafiike nazo.

 

6. Ambao huonyesha kwa watu vitendo vyao, ili wapate cheo katika nyoyo za hao watu, na wasifiwe.

 

7. Na huku wanazuia hisani zao na msaada wao kwa watu.