1,2. Hebu staajabuni kwa yanayo walazimu Makureshi!
Kuwalazimu safari za musimu wa baridi kwenda Yaman, na safari za musimu wa joto
kwenda Shamu, kufanya biashara na kutafuta riziki kwa utulivu na amani. (Hizo
safari za biashara za Yaman ndizo zilizo waleta Waarabu Afrika Mashariki kwa
maelfu ya miaka, na zikauleta Uislamu pande za Afrika kabla ya kuenea Arabuni.
Kwani nchi za Afrika Mashariki zilikaliwa na Waarabu kwa maelfu ya miaka. Soma
Periplus of the Erythrean Sea, na East Africa and Its Invaders ya Prof.
Coupland, na vitabu vya Sir John Gray na Dr. L.W. Hollingsworth.)
3. Basi wamtakasie ibada Mola Mlezi wa Nyumba hii aliye
wawezesha kuzifanya hizi safari mbili.
4. Ambaye anawalisha wasione njaa, na hali wao wamo katika bonde lisio na makulima, na akawalinda na khofu na watu wengine pembezoni mwao wananyakuliwa.