1. Hakika, ewe Muhammad, unajua kwa ujuzi usio ingiliwa na
shaka yoyote, alivyo fanya Mola wako Mlezi kuwafanyia wale watu wenye tembo
(ndovu), wakataka kuishambulia Nyumba takatifu ya Al-Kaaba.
2. Unajua ya kwamba hakika Mwenyezi Mungu amejaalia
juhudi yao kutaka kuibomoa Al-Kaaba ivize na ipotelee mbali. Juhudi yao
ikapeperuka, na wao wasipate makusudio yao.
3. Na Mwenyezi Mungu aliwasalitisha na majeshi ya ndege yaliyo
watokea makundi kwa makundi yakifuatana, na yakawazunguka kila upande.
4. Wakiwatupia mawe kutoka Jahannamu.
5. Akawafanya kama majani ya mimea yaliyo sibiwa yakatilifu.