1. Atapata adhabu kali na maangamio huyo ambaye mtindo wake ni
kuwafedhehi watu kwa kauli au kwa ishara, au kuwasengenya kuwavunjia hishima
zao.
2. Ambaye amekusanya chungu ya mali na akawa kazi yake
kuyahisabu tu, kwa kuona ladha huko kuhisabu.
3. Anadhani huyo kuwa mali yake yatamweka milele duniani, na
yatamkinga na hayo anayo yachukia?
4. Na aache dhana hiyo! Wallahi! Hapana shaka yoyote kwa
vitendo vyake viovu hivyo atakuja tumbukizwa katika Moto unao vuruga kila
kinacho tupwa humo!
5. Na kitu gani kitacho kujuvya nini ukweli wa Moto huu wa
H'ut'ama?
6. Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa kwa amri yake, na daima
unawaka!
7. Ambao unafikilia nyoyoni na kuzizunguka nyoyo.
8,9. Huo utakuwa umefungwa milango yake, na wao watakuwa wamefungwa humo ndani kwenye maguzo yaliyo nyooka. Hawawezi kutaharaki, wala kutoka.