1. Naapa kwa Zama kwa sababu ya maajabu mengi na mazingatio yaliomo ndani yake.

 

2. Hakika kila binaadamu bila ya shaka yumo katika namna fulani au fulani ya kukhasiri, kwa mujibu wa anavyo ghilibiwa na pumbao na matamanio.

 

3. Isipo kuwa wale walio muamini Mwenyezi Mungu na wakatenda mema, na wakadumu juu ya ut'iifu, na wakasemezana na kuusiana kwa kushikamana na Haki, kwa itikadi, na maneno, na vitendo. Na wakausiana wasubiri na wavumilie mashaka yanayo wapata wenye kushikamana na Dini. Basi hao ndio wenye kusalimika na hiyo khasara, wenye kufanikiwa duniani na Akhera.