1. Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika usiku wa Cheo na Utukufu.

 

2. Na kitu gani kitakufunza ni nini usiku huo wa Cheo na Utukufu?

 

3. Usiku wa Qadr na Sharaf, Cheo na Utukufu,  ni bora kuliko miezi elfu, kwa kuwa umekhusika kwa kuteremka ndani yake Qur'ani tukufu.

 

4. Huteremka Malaika na Jibrili katika usiku huo mpaka kwenye ardhi kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa sababu ya kila jambo.

 

5. Na wameaminika na maudhi na uovu. Hali inabaki  hivyo mpaka mapambazuko ya alfajiri.