1. Hakika tumekukunjulia kifua chako kwa kuwa tulitia ndani
yake Uwongofu na Imani.
2. Na tumekupunguzia mizigo iliyo kuwa mizito juu ya mgongo
wako, kwa kukuunga mkono na kukusahilishia mambo yako,
3. Ambayo yalikuwa ni mazito juu ya mgongo wako.
4. Na tumelitukuza jina lako, tukalifanya linatajwa na ulimi wa
kila Muumini pamoja na jina letu.
5. Hizo ni baadhi ya neema zetu juu yako. Basi kuwa na yakini
na uweza wa Mwenyezi Mtukufu, kwani pamoja na uzito upo wepesi mwingi unao kuja
nao.
6. Hakika pamoja na uzito (wakati huo huo ijapo kuwa wewe
hujui), upo wepesi mwingi vile vile.
7. Basi ukipata nafasi katika kazi ya kuwalingania watu, na
mambo yaliyo khusiana na Jihadi, endelea na jitihada ya ibada na jishughulishe
nafsi yako katika hayo.
8. Kwa Mola wako Mlezi tu ndio uelekee kwa kumwomba na kumhitajia.