1. Naapa kwa wakati wa kupanda juu jua, na ni wakati wa
uchangamfu na kazi!
2. Na naapa kwa usiku unapo tulia na ukatanda kote kiza chake!
3. Ewe Muhammad! Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukuchukia.
4. Na matokeo ya mambo yako, mwisho wake, yatakuwa bora kuliko
mwanzo wake.
5. Na ninaapa kuwa bila ya shaka hapo Mola wako Mlezi atakupa
kheri za duniani na Akhera hata utaridhia.
6. Kwani hakukukuta wewe yatima unahitaji wa kukutunza naye
akakupa makaazi ya kukuhifadhi kwa mwenye kukuangalia vyema kwa mambo yako?
7. Na akakuona umebabaika hukukinaika na itikadi zilizo
kuzunguka, naye akakuongoa kwenye Njia ya Haki?
8. Akakukuta fakiri wa mali naye akakutajirisha kwa kukupa
riziki?
9,10,11. Ikiwa hii ndiyo hali yetu nawe, basi yatima usimdhili, na mwenye kuomba au kuuliza usimjibu kwa ukavu, na ama neema za Mola wako Mlezi zitangaze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kuwa ndio kudhihirisha neema.