1,2,3. Kitakapo
tukia Kiyama haitatokea nafsi yoyote ya kukadhibisha kutukia kwake. Kiyama hicho
kitawateremsha chini walio waovu, na kitawanyanyua juu walio wema.

4,5,6. Ardhi
itakapo tikiswa, na ikatetemeshwa kwa nguvu, na milima ikavurugwa teketeke,
ikawa vumbi la kupeperushwa, Aya hizi tukufu zinaeleza hadi gani vitakuwa
vitisho vitavyo uteremkia ulimwengu kitapo fika Kiyama. Na katika vitisho hivyo
ni hayo masaibu ya dunia yatakayo athiri ardhi na mat'abaka yake. Kwani hii
ardhi tunayo ishi juu ya mgongo wake si yenye kutulia na kukaa sawa kwa
utimilivu. Kwani hiyo imeundwa kwa mat'abaka ya majabali yaliyo ingiliana ovyo.
Huenda baadhi yao yakateremka yakaachana na mengineyo yaliyo jirani nayo. Na
huwa hiyo inayo itwa kupasuka kwa mat'abaka ya ardhi, Geological cleavage kama
inavyo tokea katika maeneo kadhaa wa kadhaa. Mpasuko huu ulikuwa na ungali kuwa
ndio asili ya chini kabisa ya zilzala, mitetemeko, mikubwa kwa kuathirika na
nguvu za kudidimiza na kuvuta zinazo fuatana na mat'abaka ya ardhi yanapo
vunjika. Basi mizani ya utulivu ya nguvu hizi inapo geuka kwa kuathirika na
mambo mengineyo ya nje huenda zikafunguka nguvu za mtikiso mkubwa ndio ikatokea
mitetemeko na mitikisiko ya ardhi, ambayo hubomoa kila kitu kiliopo juu ya ardhi
karibu na ilipo anzia hiyo zilzala. Na hapo tena hutokea uharibifu mkubwa mno.
Na hayo maelezo ya kisayansi hayageuzi kitu, wala hayako mbali na nadhari ya
kidini. Kwani hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu huenda akajaalia sababu za maumbile
za kawaida zikajumuika kwa njia tusiyo izoea sisi ili zikiingiliana kwa njia ya
kutisha ndio sababu ya kuharibika dunia. Hapo maelezo ya kisayansi yanafuatana
na Aya zenye kuonya kwa vitisho hivyo vikuu. Na yote hayo yanatokana kwa
Mwenyezi Mungu. Na hutokea kwa idhini yake Mwenyezi Mungu kutimiza hukumu yake
katika dunia yetu

katika dunia yetu.

7. Na mkawa
nyote siku hiyo namna tatu kwa mujibu wa vitendo vyenu;
8,9. Basi watu
wa mkono wa kulia, watu wa cheo kilio bora, utukufu ulioje huo wa hali yao! Na
watu wa kushotoni, hao ni watu wa cheo duni, uovu ulioje wa hali yao!

10,11,12. Na
walio tangulia mbele katika mambo ya kheri duniani ndio watakuwa mbele katika
vyeo vya Akhera. Hao ndio walio karibishwa mbele kwa Mwenyezi Mungu. Mola wao
Mlezi atawatia katika Bustani zenye neema.

13,14. Hawa
walio karibishwa mbele ni kundi la wengi katika mataifa yaliyo tangulia na
Manabii wao, na wachache katika umma wa Muhammad ukiwalinganisha na hao.

15,16. Juu ya
viti au vitanda vilivyo nakishiwa kwa nakshi za vito vya thamani, wakivitegemea
kwa raha na utulivu huku wakielekezana nyuso kwa ziada ya mahaba.

17,18.
Wakiwazungukia kwa kuwakhudumia vijana watakao baki milele hivyo hivyo, nao
wamechukua vikombe na mabirika yaliyo jaa vinywaji vya Peponi, na bilauri zenye
mvinyo kutoka chemchem zinazo miminika,

19. Vinywaji
hivyo haviwaletei kuumwa kichwa wala kutokwa akili kwa ulevi.
20,21. Na
matunda ya kila namna wanayo yapenda na wanayo yaona; na nyama za ndege kama
zinavyo tamani nafsi zao.

22,23,24. Na
wanawake wenye macho ya vikombe, kama mfano wa lulu zilio hifadhiwa katika
chaza, kwa usafi wao na urembo wao. Watapewa haya kuwa ni malipo kwa mambo mema
waliyo kuwa wakiyatenda duniani.

25,26. Huko
Peponi hawatasikia maneno yasiyo kuwa na maana, wala masimulizi ya kumtia
dhambini mwenye kuyasikia. Ila watalo sikia ni kauli ya wao kwa wao:
Tunakusalimuni kwa Salama.

27. Na watu wa
mkono wa kulia, hapana ajuaye nini malipo ya watu wa kuliani.
28,29,30,31,32,33,34. Katika miti ya mikunazi iliyo katwa miba yake, na migomba
iliyo pangika na ndizi zake zimepandana juu ya mikungu, na kivuli kilicho enea
wala hakiondoki, na maji yanayo miminika karibu yao popote wayatakapo, na
matunda ya namna nyingi na kabila nyingi yasiyo tindikia wakati wowote, wala
hazuiwiliwi ayatakayo, na matandiko yaliyo nyanyuliwa ya starehe.

35,36,37,38.
Hakika Sisi tulianza kuwaumba Mahurulaini mwanzo, na tukawafanya kuwa ni vijana,
wenye kupendwa na waume zao, wenye umri ulio karibiana, wa tayari kwa neema ya
watu wa kuliani.

39,40. Watu wa
kulia ni wengi katika mataifu yaliyo kwisha tangulia, na kikundi kikubwa katika
umma wa Muhammad.

41. Na watu wa
kushoto, hapana anaye jua nini adhabu ya watu wa kushoto.
42,43,44.
Watakuwa kwenye upepo umoto utakao wazunguka, unao penya katika tundu za mwili,
na maji yaliyo chemshwa motoni wayanywe na wamiminiwe vichwani, na katika kivuli
cha kiza cheusi cha moshi umoto, hapana ubaridi wa kupunguza joto la hewa, wala
huruma ya kuwaletea nafuu wanapo vuta pumzi.

45. Hakika hao
kabla ya haya walikuwa wamepita kiasi katika kustarehea neema za duniani,
wamepumbaa hawataki kumt'ii Mwenyezi Mungu Mtukufu.
46. Na
walikuwa wameshikilia daima kufanya dhambi kubwa kabisa, kwani waliapa kwa
Mwenyezi Mungu kwamba kabisa Mwenyezi Mungu hatamfufua aliye kufa.
47. Na
walikuwa wakisema kwa kukanusha kurejea tena: Ati tutafufuliwa baada ya kwisha
kufa, na baadhi ya miili yetu ikisha kuwa udongo na mengine mifupa iliyo chakaa?
Ati sisi tutarudishwa tuwe hai mara ya pili?
48. Ati
tutafufuliwa sisi na baba zetu wa zamani walio kwisha kuwa udongo ulio tapanyika
na umepotea katika ardhi?
49,50. Waambie
kwa kuwajibu kukanusha kwao: Hakika wa zamani na wa mwisho, ambao nyinyi ni
katika jumla ya hao, nyote mtakusanywa katika wakati wa siku malumu, na wala
hamtoipita.

51,52,53.
Kisha nyinyi, enyi mnao ipinga Njia ya Uwongofu, mnao kanusha kufufuliwa, bila
ya shaka mtakula mti wa Zaqqumu katika Jahannamu, na mtayajaza matumbo yenu kwa
shida ya njaa.

54,55.
Mtakunywa juu ya mlicho kila maji yenye kutokota, yasiyo ondoa kiu, na mtakunywa
kwa wingi na pupa kama anavyo kunywa ngamia mwenye kiu kisicho katika kiu chake
kwa maji.

56. Hayo
yaliyo tajwa ya mateso mbali mbali ndio karamu yao waliyo andaliwa kwa siku ya
malipo.
57. Sisi
tulianza kukuumbeni mlipo kuwa si chochote, basi hebu hamkiri uweza wetu wa
kukurejesheni tena baada ya kukufufueni?
58,59.
Hamuangalii manii mnayo itia katika tumbo la uzazi? Ni nyinyi ndio mwenye uweza
juu yake na kuilea mpaka ikawa mtu, au ni Sisi ndio twenye makadara hayo?

60,61. Sisi
tumekuhukumieni mauti, na tumeweka wakati makhsuri wa kufa kwenu. Na wala Sisi
si wenye kushindwa kukubadilisheni sura zenu, na kuzileta nyengine, na
tukakuumbeni katika umbo jengine na sura nyengine msiyo ijua.

62. Bila ya
shaka mmekwisha yakinika kuwa Mwenyezi Mungu alikuumbeni mara ya kwanza, basi
je, hamkumbuki kwamba Mwenye kuweza hayo ni Mweza zaidi wa kufanya tena.
63,64. Je!
Hamuangalii mbegu mnayo ipanda katika ardhi? Ni nyinyi mnao ifanya imee au ni
Sisi peke yetu ndio tunaifanya imee?

65,66,67.
Tungeli taka tungeli ifanya mimea hiyo iwe mabua na mapepe yaliyo katika katika
kabla haijapevuka, mkawa mkistaajabu tu kwa uovu ulio isibu, huku mkisema:
Hakika sisi tumepata khasara baada ya juhudi yetu. Bali sisi hatuna bahati,
tumenyimwa riziki.

68,69. Je!
Hamyaoni maji matamu mnayo yanywa? Ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni,
au ni Sisi ndio Wenye kuyateremsha kuwa ni rehema juu yenu? Katika Kiarabu
limetajwa neno Almuzni. Maana yake ni mawingu yanayo leta mvua. Na kitendo cha
kunyesha mvua kinahitajia mambo yaliyo khusiana na hali ya hewa maalumu ambayo
mwanaadamu hana mamlaka nayo, au kuyaleta kwa juhudi zake. Kwa mfano
zinahitajiwa pepo zinazo kwenda kwa mkondo zilizo baridi juu ya nyengine zilizo
za joto, au hali za kuondoka utulivu katika anga. Na watu wamejaribu kuinyesha
mvua kwa mawingu yanayo pita kwa njia ya ufundi, lakini juhudi hizo mpaka sasa
ni majaribio, na lilio thibiti katika sayansi ni kufuzu kwa majaribio hayo ni
kudogo mno, na hata hivyo kunalazimu ziwepo hali maalumu za maumbile zinazo
saidia.

70. Lau
tungeli taka tungeli yafanya hayo maji yakawa ya chumvi yasiyo nyweka. Basi
mbona hamumshukuru Mwenyezi Mungu aliye yajaalia matamu yenye kunyweka?
71,72. Je!
Hamuuoni moto huo mnao uasha? Ni nyinyi ndio mlio uotesha mti wake, na mkautia
ndani ya huo mti moto, au ni Sisi ndio tulio uumbia hivyo, kadhaalika?

73. Sisi
tumeufanya huu moto uwe ni ukumbusho wa Moto wa Jahannamu mtapo uona, na uwe ni
manufaa kwa wasafiri wa msitu na nyika, wakinafiika kwa kupikia chakula chao na
kuotea moto wakati wa baridi.
74. Basi
dumisha kusabihi, kutakasa, kwa kulidhukuru jina la Mola wako Mlezi aliye
Mkubwa, kwa kumtakasa na kumshukuru kwa neema hizi nzuri.
75,76. Basi
ninaapa kweli kwa maangukio ya nyota pale zinapo tua mwisho wa usiku wakati wa
Tahajudi, ibada za usiku, na kustaghafiru. Na hakika bila ya shaka hicho ni
kiapo kikubwa chenye maana ya kufikia mbali, lau kuwa mnafikiri makusudio yake.
Aya mbili hizi zinabainisha hadi ya umuhimu wa kiapo hichi kikubwa. Kwani nyota
ni vitu vyenye kutoa mwangaza wenyewe, na nyota ya karibu mno kwetu sisi, nayo
ni jua, ni kiasi ya masafa ya miaka 500 ya mwangaza. Na nyota ifuatayo kwa
ukaribu iko mbali nasi kwa kiasi cha miaka 4 ya mwangaza takriban. Basi nguvu
tunazo zitumia kutokana na jua ndizo zinazo tuwezesha kuishi. Lau kuwa umbali wa
jua kutokana na ardhi ni duni ya hivyo au zaidi ya hivyo basi hapana shaka kuwa
maisha yangeli kuwa taabu, bali ni muhali. Kadhaalika ukubwa wa nyota
unakhitalifiana. Zipo nyota kubwa mno hata ukubwa wake unaweza kukusanya hii
ardhi na jua juu ya umbali wao. Vipo vikundi vya nyota vinavyo itwa A'naqiid
vinaogelea angani zikivuka Njia ya Maziwa The Milky Way mara kwa mara. Wakati wa
kupita kwake zikasadifiana kukutana na kikundi cha jua na zikagongana basi
hakika hapo itakuwa ndio maangamizo na kumalizika kwa kweli. Hata ikikaribia
nyota moja katika nyota zitokazo kwenye jua basi hayo pia yataleta kuharibika
mizani na kupelekea maangamizo na kumalizika ulimwengu. Kwa hivyo basi hakika
Ishara za mazingatio na uweza wa Mwenyezi Mungu zinaonekana katika ulimwengu huu
alio uumba Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala na akaupanga.

77,78. Hakika
hii bila ya shaka ni Qur'ani yenye manufaa mengi, imo katika ubao ulio hifadhiwa
Al-lauhu-lmahfudh, usio karibiwa na yeyote ila Malaika walio karibishwa kwa
Mwenyezi Mungu. (Kwa watumiaji Computer wanaweza kukisia kuwa hiyo
Al-lauhu-lmahfudh ni kama Disk iliyomo ndani ya Computer na haigusi mtu, na
Misahafu tunayo iona, na kuisoma, ni kama yapigwayo chapa kutoka hiyo Disk.)

79,80.
Hawaigusi Qur'ani Tukufu ila walio t'ahirika na najisi na hadathi, vitengua
udhu; imeteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe vyote.

81. Je!
Mnapuuza? Ni Qur'ani hii tukufu ndio nyinyi mnaidharau?
82. Na badala
ya kuishukuru riziki yenu ndio mna ikadhibisha?
83,84,85. Basi
je! Ikifika roho ya mmoja wenu kwenye mapitio ya pumzi, na nyinyi inapo fika
roho kwenye koo nanyi mnamwangalia huyo anaye kufa, na Sisi tuko karibu zaidi
kwa huyo aliye kabiliwa na mauti na tunaijua zaidi hali yake kuliko nyinyi,
lakini nyinyi hamjui hayo wala hamhisi.

86,87. Basi
je! Ikiwa nyinyi si wenye kunyenyekea kwa Ungu wetu, mrudishieni roho yake huyo
aliye kabiliwa na mauti ikiwa nyinyi mwasema kweli kwamba nyinyi mnazo nguvu na
hamshindwi.

88,89. Ama
akiwa huyo aliye kabiliwa na mauti ni katika walio tangulia walio karibishwa
basi mwisho wake ni raha, na rehema, na riziki njema, na Pepo yenye neema.

90,91. Ama
akiwa katika watu wa mkono wa kulia, basi ataambiwa kwa maamkio na takrima:
Unapewa salamu kutokana na watu wa kuliani.

92,93,94. Na
ama akiwa ni katika wa kushoto, wanao kanusha, walio wapotovu, basi atakirimiwa
maji ya moto hadi ya kuchemka, na kubabuliwa na moto wa mwisho wa ukali.

95. Hakika
haya yaliyo tajwa katika Sura hii tukufu bila ya shaka ni kiini cha yakini iliyo
thibiti, isiyo ingiliwa na shaka.
96. Tanguliza
tasbihi kwa kumdhukuru Mola wako Mlezi aliye Mkubwa, kwa kumtakasa na kumshukuru
kwa neema zake.
Copyright � 22 August 1997, Sheikh
Ali Muhsin Al Barwani