1. Kiyama kimekaribia na mwezi
utapasuka hapana hivi wala hivi.
2. Na makafiri wakiona
Ishara, yaani muujiza mkubwa, wao hupuuza wakaacha kuuamini. Bali husema: Huu ni
uchawi wa daima unaendelea!
3. Na wamewakanusha Mitume
na wakafuata yaliyo zainishwa na matamanio yao. Na kila jambo huishia mwisho
wake linapo tulia na kuthibiti.
4. Na ninaapa kuwa
zimewajia makafiri khabari za mataifa yaliyo tangulia zenye ukweli wa uumbaji
ambazo zina mikemeo ya kutosha.
5. Haya yaliyo wajia ni
hikima kubwa na lengo la kufikia mbali. Lakini maonyo yataleta faida gani kwa
wanao zipinga hikima hizo?
6. Ewe Muhammad! Waachilie
mbali hawa makafiri, nawe ngojea siku atapoita mwitaji wa Mwenyezi Mungu kuitia
jambo ambalo nafsi inalichukia mno!
7. Macho yao yatainamia
chini kwa wingi wa kitisho, wakitoka makaburini kama kwamba ni nzige walio
tawanyika, kwa wingi wao na mbio zao.
8. Wakimkimbilia huyo
mwitaji, wakimtazama kwa unyonge na unyenekevu, macho yao yanamwangalia yeye tu.
Makafiri watasema Siku ya Kiyama: Hii leo ni siku nzito, siku ya shida!
9. Kabla ya makafiri wa
Makka walikwisha kanusha kaumu ya Nuhu. Walimkadhibisha Nuhu, mja wetu na Mtume
wetu, wakamsingizia kuwa ana wazimu. Wakaingiza baina yake na kufikisha kwake
Ujumbe kila namna ya maudhi na vitisho.
10. Nuhu akamwomba Mola
wake Mlezi akisema: Hakika mimi nimeshindwa na hawa watu wangu, basi wapatilize
hawa kwa ajili yangu!
11,12. Basi tukaifungua
milango ya mbingu ikamimina maji yasiyo katika; na tukaipasua ardhi kwa chemchem
zikitibuka maji. Yakakutana maji ya mbinguni na maji ya ardhi kuwahiliki, kama
alivyo kadiria Mwenyezi Mungu Mtukufu.
11,12. Basi tukaifungua
milango ya mbingu ikamimina maji yasiyo katika; na tukaipasua ardhi kwa chemchem
zikitibuka maji. Yakakutana maji ya mbinguni na maji ya ardhi kuwahiliki, kama
alivyo kadiria Mwenyezi Mungu Mtukufu.
13,14. Tukampakia Nuhu
katika jahazi la mbao zinazo fungwa pamoja kwa kamba, kama mtepe. Likawa
linakwenda baharini chini ya hifadhi yetu, kuwa ni malipo kwa Nuhu ambaye watu
wake waliendelea kuukanya wito wake.
13,14. Tukampakia Nuhu
katika jahazi la mbao zinazo fungwa pamoja kwa kamba, kama mtepe. Likawa
linakwenda baharini chini ya hifadhi yetu, kuwa ni malipo kwa Nuhu ambaye watu
wake waliendelea kuukanya wito wake.
15. Na tumeliacha hilo
tukio na kuzamishwa makafiri na kuokolewa Waumini liwe ni mawaidha, lakini yupo
mwenye kuwaidhika?
16. Jee, vipi ilikuwa
adhabu yangu na onyo langu kwa wakhalifu.
17. Ninaapa, tumeifanya
Qur'ani iwe sahali kukumbukwa na kutoa mawaidha. Lakini je, yupo wa kuwaidhika?
18. Kina A'di
walimkadhibisha Mtume wao Hudi. Je, hali gani adhabu yangu na onyo langu
lilikuwa kwa wendao kinyume!
19,20. Sisi kwa yakini
tuliwapatiliza kwa upepo ubaridi unao vuma, katika siku ya ukorofi wa daima,
ukiwang'oa watu na kuwatupa nao wamekufa, kama vinavyo ng'olewa vigogo vya
mitende na mizizi yake.
19,20. Sisi kwa yakini
tuliwapatiliza kwa upepo ubaridi unao vuma, katika siku ya ukorofi wa daima,
ukiwang'oa watu na kuwatupa nao wamekufa, kama vinavyo ng'olewa vigogo vya
mitende na mizizi yake.
21. Hali gani adhabu
yangu na onyo langu lilikuwa kwa walio kwenda kinyume!
22. Na bila ya shaka Sisi
tumeifanya sahali Qur'ani kwa ajili ya mawaidha na mazingatio, basi je, yupo wa
kuwaidhika?
23. Thamudi
walikadhibisha maonyo ya Nabii wao, Saleh.
24. Wakasema: Hivyo aje
mtu tu katika sisi, watu wa kawaida, asiye na watu, nasi tumfuate? Tukimfuata
huyo basi bila ya shaka sisi tutakuwa mbali mno na haki, na tutakuwa tuna wazimu
basi.
25. Uteremshiwe wahyi
kwake yeye katika sisi na hali wapo wanao stahiki zaidi? Bali huyo kazikdi
katika uwongo, mwenye kukanya neema.
26. Karibu watakuja jua
siku itapo wateremkia adhabu ni nani mwongo anaye ikanya neema. Wao au Saleh,
Mtume wao?
27. Hakika Sisi
tunampelekea Mtume wetu Saleh ngamia mke, awe ni mtihani wao. Basi wangojee, na
uwatazame watafanya nini. Na subiri, uvumilie maudhi yao mpaka itapo kuja amri
ya Mwenyezi Mungu.
28. Na waambie kwamba
maji yatagawanywa baina yao na ngamia. Kila mmoja wao atakuwa na zamu yake aje
kunywa katika siku yake.
29,30. Wakamwita mtu wao
mmoja akapania kumchinja yule ngamia, akamchinja. Basi vipi ilikuwa adhabu yangu
na onyo langu kwa hao wakhalifu walio kwenda kinyume na amri.
29,30. Wakamwita mtu wao
mmoja akapania kumchinja yule ngamia, akamchinja. Basi vipi ilikuwa adhabu yangu
na onyo langu kwa hao wakhalifu walio kwenda kinyume na amri.
31. Sisi tuliwapatiliza
kwa ukelele mmoja tu, wakawa kama miti mikavu anayo ikusanya yeyote atakaye
kujengea boma la uwa wake.
32. Na bila ya shaka Sisi
tumeisahilisha Qur'ani iwe nyepesi kwa ajili ya mawaidha na kuzingatia. Lakini
je, yupo wa kuwaidhika?
33. Kaumu Lut'i nao
walikadhibisha maonyo ya Mtume wao.
34,35. Hakika Sisi
tuliwapelekea upepo mkali wa kuwatupia changarawe. Isipo kuwa watu wa Lut'i
walio amini. Hao tuliwaokoa na adhabu hii mwisho wa usiku, kwa kuwapa neema
iliyo toka kwetu. Neema kama hizo kubwa kubwa ndivyo tunavyo walipa wenye
kuishukuru neema yetu kwa imani yao na ut'iifu.
34,35. Hakika Sisi
tuliwapelekea upepo mkali wa kuwatupia changarawe. Isipo kuwa watu wa Lut'i
walio amini. Hao tuliwaokoa na adhabu hii mwisho wa usiku, kwa kuwapa neema
iliyo toka kwetu. Neema kama hizo kubwa kubwa ndivyo tunavyo walipa wenye
kuishukuru neema yetu kwa imani yao na ut'iifu.
36. Na hakika Lut'i
aliwahadharisha watu wake vipi mshiko wetu ulivyo mkali, wakatilia shaka maonyo
yake kwa kuwa wanamwona mwongo.
37. Wakamtaka awape
wageni wake wawatende fiili yao, tukayafuta macho yao kuwa ni malipo kwa hilo
walilo litaka. Basi waambie kwa kuwakejeli: Igugumieni adhabu yangu, na maonyo
yangu!
38,39. Na asubuhi mapema
ikawashitua adhabu ya kuthibiti milele. Wakaambiwa: Igugumieni adhabu yangu na
maonyo yangu!
38,39. Na asubuhi mapema
ikawashitua adhabu ya kuthibiti milele. Wakaambiwa: Igugumieni adhabu yangu na
maonyo yangu!
40. Na hakika tumeifanya
Qur'ani ni sahali kwa ajili ya mawaidha na mazingatio. Je! Yupo anaye waidhika?
41. Na watu wa Firauni
yaliwajia maonyo ya mfululizo.
42. Walikadhibisha Ishara
zetu na miujiza yetu waliyo kuja nayo Mitume wetu. Tukawaangamiza kwa maangamizo
ya nguvu yasiyo shindika, ya uwezo mkubwa.
43. Ati nyinyi, makafiri,
mna nguvu zaidi kuliko hao wa kaumu zilizo tangulia ambao wameangamizwa? Au
nyinyi mmetolewa makosani kwa ilivyo teremka katika Vitabu vya mbinguni?
44. Bali ati wanasema
hawa makafiri: Sisi ni kikundi kilicho ungana chenye nguvu juu ya maadui wake,
hakishindwi.
45. Kikundi hicho
kitashindwa, na watakimbia mbio wakifurushwa.
46. Bali Kiyama ndio
miadi ya adhabu yao. Na Kiyama ni kizito zaidi, na kichungu zaidi.
47. Hakika wakosefu
kutokana na hawa na hao watakuwa katika hilaki na Jahannamu inayo waka moto.
48. Siku watapo bururwa
kifudifudi katika Moto wakiambiwa: Hilikini kwa machungu ya Jahannamu na joto
lake!
49. Hakika Sisi tumeumba
kila kitu. Tumeviumba kwa kukadiria inavyo hitajia hikima.
50. Na haikuwa amri yetu
tukitaka kitu ila neno moja tu, nalo ni kusema: "Kuwa", nacho huwa, papo hapo
kama kupepesa kwa jicho.
51. Na bila ya shaka Sisi
tumekwisha waangamiza wengine walio fanana nanyi katika ukafiri. Je! Yupo aliye
waidihika?
52. Na kila kitu walicho
kifanya duniani kimeandikwa katika madaftari, kimeambatishwa nao.
53. Na kila dogo na kubwa
katika vitendo limeandikwa. Hakipotei kitu.
54. Hakika wachamngu
watakuwa katika Mabustani yenye shani kuu, na mito ya namna mbali mbali.
55. Katika baraza ya
Haki, hakuna porojo huko wala madhambi, kwa Mwenyewe Mfalme Mtukufu wa uweza
Copyright � 22 August 1997, Sheikh
Ali Muhsin Al Barwani