1,2,3,4,5,6.
Ninaapa kwa mlima wa T'ur ulioko katika Sinai. Kwenye mlima huo ndio Nabii Musa
a.s. alisemezwa. Na naapa kwa Kitabu kilicho teremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu
kilicho andikwa katika kurasa zilio nyepesi kuzisoma, na kwa Nyumba iliyo jengwa
kwa sababu ya wenye kuizunguka kwa ibada na wenye kusimama na kurukuu na
kusujudu kwa Sala, na naapa kwa mbingu iliyo nyanyuliwa bila ya nguzo, na bahari
iliyo jaa.

7,8. Hakika
adhabu ya Mola wako Mlezi waliyo ahidiwa makafiri bila ya shaka itawateremkia
hapana hivi wala hivi. Hapana wa kuizuia isiwafikilie.
7,8. Hakika
adhabu ya Mola wako Mlezi waliyo ahidiwa makafiri bila ya shaka itawateremkia
hapana hivi wala hivi. Hapana wa kuizuia isiwafikilie.
9,10. Siku
mbingu itapo tikisika kwa mtikiso mkubwa, na milima itapo ng'oka kutoka hapo
ilipo kwa kuonekana khasa.
9,10. Siku
mbingu itapo tikisika kwa mtikiso mkubwa, na milima itapo ng'oka kutoka hapo
ilipo kwa kuonekana khasa.
11,12.
Maangamio makubwa yatawapata siku hiyo hao wanao kadhibisha Haki, ambao katika
upotovu ndio mchezo wao wanapo chezea.
11,12.
Maangamio makubwa yatawapata siku hiyo hao wanao kadhibisha Haki, ambao katika
upotovu ndio mchezo wao wanapo chezea.
13. Siku
watakapo sukumwa kuingizwa Motoni kwa nguvu.
14.
Wataambiwa: Huu ndio Moto mlio kuwa mkiukanusha duniani.
15. Je! Bado
mnaendelea kuukanya. Huu Moto mnao uona ni uchawi, au hamwoni tu?
16. Uingieni,
mpate kuonja vukuto lake. Mkivumilia shida zake, au mkitovumilia, kwenu ni
mamoja. Hakika leo mtayakuta mliyo kuwa mkiyatenda duniani.
17. Hakika
wachamngu watakuwa katika Mabustani yenye wasaa, hapana awezae kuyaeleza
yalivyo, na neema kubwa kadhaalika.
18.
Wakistarehe na neema alizo wapa Mola wao Mlezi, na Mola wao Mlezi akawalinda na
adhabu ya Moto.
19.
Wataambiwa: Kuleni chakula mpendacho, na kunyweni kwa raha, kuwa ni malipo ya
vitendo mlivyo vitenda duniani.
20. Wakikaa
nao wameegema juu ya makochi yaliyo pangwa kwa safu. Na tutawaoza wake weupe
wenye macho ya vikombe wazuri.
21. Na walio
amini, na wakastahiki vyeo vya juu, na vizazi vyao wakawafuata katika Imani, na
wao hawajafikia daraja zile za baba zao, tutawakutanisha nao hao dhuriya zao,
wapate kutulia nyoyo zao. Na wala hatuwapunguzii chochote katika thawabu za
vitendo vyao. Wala wazazi hawatobeba chembe katika makosa ya dhuriya zao. Kwa
sababu kila mtu amefungamana kwa rahani na vitendo vyake visio bebwa na
mwenginewe.
22. Na
tutawazidishia matunda mengi, na nyama kama waipendayo.
23. Huko
Peponi watakuwa wakipeana kwa mapenzi bilauri zilio jaa vinywaji visio leta
maneno yasiyo na maana wala vitendo vya dhambi, yaani havilevi na kuondoa akili.
24. Na
watakuwa wakiwapitia vijana walio wekwa kwa kuwatumikia, kwa weupe wao na usafi
wao kama lulu iliomo ndani ya chaza.
25. Na watu wa
Peponi watakabiliana wakiulizana wao kwa wao khabari za hayo mambo makuu wanayo
yapata na sababu zake.
26,27. Kabla
ya neema hizi sisi tulikuwa pamoja na ahali zetu tukiiogopa adhabu ya Mwenyezi
Mungu. Mwenyezi Mungu akatufadhili kwa rehema yake, na akatukinga na adhabu ya
Moto.
26,27. Kabla
ya neema hizi sisi tulikuwa pamoja na ahali zetu tukiiogopa adhabu ya Mwenyezi
Mungu. Mwenyezi Mungu akatufadhili kwa rehema yake, na akatukinga na adhabu ya
Moto.
28. Hakika
sisi kabla ya haya tulikuwa duniani tukimuabudu Yeye tu. Yeye peke yake ndiye
Mhisani Mkunjufu wa rehema.
29. Wewe
endelea na kukumbusha kama unavyo fanya. Kwani wewe, kwa neema ya Mwenyezi Mungu
aliyo kuneemesha kukupa Unabii na akili iliyo timia, si kuhani anaye toa khabari
za ghaibu bila ya ilimu, wala si mwendawazimu unaye sema usiyo yasadiki.
30,31. Bali
ati wanasema huyu ni mtunga mashairi, tunaye mngojea afikiwe na mauti! Waambie
kwa kuwatisha: Ngojeeni, na mimi nami ni katika wanao ngojea mwisho wa hali
yangu na hali yenu!
30,31. Bali
ati wanasema huyu ni mtunga mashairi, tunaye mngojea afikiwe na mauti! Waambie
kwa kuwatisha: Ngojeeni, na mimi nami ni katika wanao ngojea mwisho wa hali
yangu na hali yenu!
32. Bali ndio
akili zao zinawaamrisha waseme maneno hayo yanayo gongana. Kwani kohani na
mtunga mashairi ni watu wenye fahamu na akili; na mwendawazimu hana akili.
Lakini hawa ni watu walio pita mipaka katika inadi zao.
33. Bali ati
wanasema: Muhammad ameizua hii Qur'ani! Bali hawa kwa ukaidi wao hawaamini tu.
34. Basi
nawalete masimulizi kama haya ya Qur'ani, ikiwa wao ni wasema kweli kuwa
Muhammad kaizua.
35. Kwani wao
wameumbwa bila ya kuweko Muumbaji, au wao wamejiumba wenyewe, basi kwa hivyo ati
ndio hawamtambui Muumbaji wa kumuabudu?
36. Kwani wao
ndio walio ziumba mbingu na ardhi kwa uumbaji mzuri wa pekee wa namna hii? Bali
wao hawana na yakini na lolote lilio mwajibikia Muumbaji. Na kwa hivyo ndio
wanamshirikisha.
37. Kwani wao
wanazo khazina za Mola wako Mlezi wanazo zisarifu watakavyo? Au wana nguvu za
kutenda watakavyo, na kupanga mambo kama wapendavyo?
38. Bali
wanacho kipandio cha kupandia mpaka mbinguni wakasikiliza anayo yahukumia
Mwenyezi Mungu? Kama hivyo, basi nawamlete huyo mtu wao anaye sikiliza atoe hoja
iliyo wazi kuthibitisha madai yake.
39. Ati
Mwenyezi Mungu ndiye mwenye mabinti, kama mnavyo zua, na nyinyi ndio mna watoto
wa kiume kama ndio mnavyo penda?
40. Kwani wewe
unawaomba chochote kuwa ni ujira wa kuwafikishia Ujumbe wako, ndio wamethakilika
na hizo gharama wakalalimika?
41. Bali kwani
wao wanao ujuzi kujua mambo ya ghaibu, yaliyo fichikana, na hivyo wanaandika
kutoka hayo wayatakayo?
42. Au
wanataka kukufanyia vitimbi tu na kuuharibu Ujumbe wako? Basi hao walio kufuru
ndio wanao stahiki kutumbukia katika vitimbi vyao.
43. Au wao
wanae mungu wa kuabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu atakae walinda na adhabu ya
Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu ametakasika na hayo wanayo mshirikisha naye!
44. Na wakiona
kipande cha mbingu kinwaangukia kuwaadhibu wao husema, kwa inda tu: Ni mawingu
yaliyo bebana!
45. Waache
bila ya kuwajali mpaka watakapo ikuta siku yao watapo angamizwa.
46. Siku
ambayo hila zao hazitawakinga hata na chembe ya adhabu, wala hawatapata wa
kuwanusuru.
47. Na hakika
hao walio dhulumu watapata adhabu mbali na hii waliyo teseka nayo hapa duniani,
lakini wengi wao hawajui hayo.
48. Wewe
isubirie hukumu ya Mola wako Mlezi ya kuwapa muhula hao, na wewe kupata maudhi
yao. Kwani hakika wewe umo katika hifadhi yetu na ulinzi wetu. Basi vitimbi vyao
havitokudhuru wewe. Na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi unapo amka.
49. Na tafuta
usiku usiku nafasi ya kumsabihi, yaani kumtakasa, Mwenyezi Mungu, na mtakase pia
wakati zinapo kuchwa nyota, yaani alfajiri.
Rudi kwenye
sura
Copyright � 22 August 1997, Sheikh
Ali Muhsin Al Barwani