* 1,2. Qaaf. Hii
ni harufi katika harufi za alifbete iliyo fungulia Sura hii kama ilivyo ada ya
Qur'ani katika kufungulia Sura kadhaa wa kadhaa kwa harufi kama hii, ili
kuwakabili makafiri kama wanaweza kuleta mfano wake, na pia kuwazindua watu
wasikilize yanayo somwa. Ninaapa kwa Qur'ani yenye ubora, na utukufu, na hishima
kwamba hakika Sisi tumekutuma wewe, ewe Muhammad, ili uwaonye watu kwa hii. Na
watu wa Makka hawakuamini, bali walistaajabu kutokea Mtume miongoni mwa jinsi
yao akiwaonya kuwa watafufuliwa. Makafiri wakasema: Jambo hili hatulijui, na la
ajabu!
1,2. Qaaf. Hii

3. Ati baada ya
kwisha kufa na tukawa udongo, tutafufuliwa tena? Huko kufufuliwa baada ya kufa
ni marejeo yaliyo mbali, hayawi.
4. Sisi hakika
tunajua vipi ardhi inavyo vimeza viwiliwili vyao baada ya kufa. Na Sisi tunacho
Kitabu kinacho dhibiti na kuhifadhi kila kitu hata kidogo.
5. Wao
hawayazingatii aliyo kuja nayo Mtume, bali walimkadhibisha mara tu bila ya
kuzingatia na kufikiri. Basi wao wamo katika hali ya kubabaika, hawana utulivu.
6.
Wameghafilika hata hawaitazami mbingu ilivyo nyanyuliwa juu yao bila ya nguzo?
Vipi tumetengeneza ujenzi wake, na tukaipamba kwa nyota, na haina nyufa za
kuitia kombo! Mbingu ni kote kulio juu yetu, na ndani yake vimo vitu vya namna
mbali mbali, vinaogelea katika njia zao, nyota na sayari. Na hayo ni kwa nidhamu
ya uangalizi mkubwa, na mshikamano ulio timia, na vilevile zinafuata kwa mpango
wake kuwafikiana na kanuni za mvutano, basi hazitelezi.
7. Na ardhi
tumeikunjua na tukaisimamisha milima iliyo kaa imara na kuthibiti kwenda chini.
Na tukaijaalia kumea kila namna ya mimea mizuri ya kuwafurahisha watazamao.
Gamba lilio funika ardhi katika mwahali maalumu limetuna, ndio hiyo milima. Na
pengine limedidimia ndio sakafu ya chini ya bahari. Na uzani wa vitu hivi vizito
vinalingana wenyewe kwa wenyewe. Na ni katika uwezo wa Mwenyezi Mungu na hikima
yake kupatikana kulingana huku kwa uzani, na ukawa umethibiti kwa kupenya madda
za ardhi zilizo fanyika hilo gamba jembamba chini ya mat'abaka ya juu juu. Na
hayo ni kutoka kuliko kuwa kuzito kwendea kuliko kwepesi.
8. Tumejaalia
hayo aone na akumbuke kila mja mwenye kurejea kwa Mola wake Mlezi, akafikiri
Ishara za uwezo wake.
9. Na kutoka
mbinguni tukateremsha maji yenye kheri nyingi na baraka, na kwa hayo tukaotesha
mabustani yenye miti, na mauwa, na matunda, na tukatoa kwa hayo nafaka za
makulima ya kuvunwa.
10. Na mitende
mirefu mirefu, yenye makole ya tende yaliyo pandana kwa wingi.
11. Tumeotesha
hiyo ili iwe ni riziki kwa waja wetu, na tukaihuisha kwa maji ardhi iliyo kauka
mimea yake. Hali kadhaalika ndivyo kufufuliwa wafu kutoka makaburini.
12,13,14.
Kabla ya hawa, kaumu nyingi ziliwakadhibisha Mitume- kaumu ya Nuhu, na kaumu
nyengine iliyo kuwa ikiitwa "Watu wa Rassi", na wa Thamudi, na wa A'di, na wa
Firauni, na kaumu Lut'i, na kaumu iliyo kuwa maarufu kwa jina la "Watu wa
Machakani", na kaumu ya Tubbaa' - wote hao waliwakadhibisha Mitume wao. Kwa
hivyo wakastahiki maangamizo niliyo waahidi.

15. Kwani
kutaka kwetu kulipungua, au uwezo wetu ulitetereka, hata tukashindwa kwa kule
kuumba kwa mara ya kwanza, tusiweze tena kuwarejeza? Hasha! Hatukushindwa, nao
wanatambua hayo. Bali wao wana shaka tu na wanadanganyikiwa na huku kuumbwa
kupya baada ya kufa.
16. Ninaapa:
Bila ya shaka tumemuumba mtu, na Sisi tunajua hata anayo semezwa na nafsi yake.
Na Sisi kwa kuzijua hali zake zote, ni karibu kuliko mshipa wake wa damu ulioko
shingoni mwake. Na hicho ndicho kitu kilicho karibu mno naye.
17. Watakapo
kutana Malaika wawili walinzi, mmoja anakaa kuliani, na mwingine anakaa upande
wa kushoto, wakiviandika vitendo vyake.
18. Halimtoki
neno ila yuko karibu naye Malaika tayari kuandika neno lake.
19. Na yatapo
kuja machungu ya kukata roho, kwa haki isiyo na shaka ndani yake, hilo ni jambo
la kweli ulilo kuwa ukilikimbia.
20. Na
baragumu litapulizwa kwa mpulizo wa kuwafufua watu. Kupulizwa huko kutakuwa siku
hiyo ya kuteremka adhabu waliyo ahidiwa.
21. Na kila
nafsi njema na mbaya, itakuja na pamoja nayo wa kuichunga kuipeleka kwenye
mkusanyo, na wenye kuwatolea ushahidi wa vitendo vyao
22.
Wataambiwa, kumtisha huyo mwenye kukadhibisha: Hakika wewe huko duniani ulikuwa
umeghafilika kabisa na haya unayo sononeka nayo hivi sasa. Basi Sisi
tumekuondolea pazia lilio kuwa likikuzuia usiyaone mambo ya Akhera. Basi jicho
lako hii leo linaona kwa nguvu.
23. Na Shetani
wake aliye kuwa mwongozi wake duniani, atasema: Kafiri huyu alioko kwangu yuko
tayari kuingia Jahannamu kwa kupotezwa nami.
24,25. Malaika
wawili wataambiwa: Watieni katika Jahannamu kila aliye pita mipaka kwa ukafiri,
na aliye pita mipaka kwa inadi, na akaacha kuifuata Haki, na akapita mipaka
kuzuia kheri, mwenye kudhulumu akaipindukia Haki, mwenye kumtilia shaka Mwenyezi
Mungu Mtukufu na aliyo yateremsha.

26. Aliye
mfanya mungu mwengine wa kumuabudu pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi mtupeni huyo
katika adhabu yenye mwisho wa ukali.
27. Shetani
atasema kumrudi yule kafiri: Ewe Mola wangu Mlezi! Mimi siye niliye mfanya awe
mwenye kua'si, lakini yeye mwenyewe alikuwa katika upotovu wa mbali na haki. Na
mimi nilimsaidia tu kwa kumpotoa.
28. Mwenyezi
Mungu Mtukufu atawaambia makafiri na wenzi wao: Msigombane mbele yangu hapa
pahala pa hisabu na malipo. Na Mimi nilikuleteeni mbele duniani onyo juu ya
kukufuru kwenu kuukataa Ujumbe wangu niliyo utuma kwenu. Nanyi hamkuamini.
29. Hapana la
kugeuza kauli ilioko kwangu na onyo langu kuwatia makafiri Motoni, wala Mimi si
Mwenye kuwadhulumu waja. Kwani simuadhibu mja yeyote bila ya makosa.
30. Siku
tutapo iambia Jahannamu kwa kuwatia kiwewe makafiri: Je! Umejaa? Nayo Jahannamu
iseme kwa kuwaghadhibikia: Wapo wengine zaidi wa kuwaongeza katika hawa wenye
kudhulumu?
31. Na Pepo
iliyo pambwa italetwa karibu kwa ajili ya wenye kumcha Mola wao Mlezi, kwa
kufuata amri zake na kuyaepuka makatazo yake, iletwe pahala pasipo kuwa mbali
nao.
32. Haya ndiyo
malipo ya kila mwenye kurejea kwa Mwenyezi Mungu, aliye mwingi wa kuhifadhi
sharia zake.
33. Mwenye
kukhofu adhabu ya Mwenyezi Mungu ambaye rehema yake imeenea juu ya kila kitu, na
Yeye haonekani, na akaja Akhera na moyo wa aliye kwisha rejea kwa Mwenyezi Mungu
Mtukufu.
34. Itasemwa
kwa hishima yao: Ingieni Peponi kwa amani. Hiyo siku mtakapo ingia Peponi ndiyo
siku ya kubakia milele isiyo na mwisho.
35. Hao
wachamngu watapata kila wakitakacho huko Peponi. Na Sisi tunazo neema za kuzidi
kuliko yanayo mpitikia mtu kuyawaza.
36. Na wengi
tumekwisha wateketeza kabla ya hawa wanao kadhibisha katika mataifa yaliyo
kwisha pita. Wao walikuwa na nguvu na madaraka zaidi kuliko hawa. Wakaizunguka
miji wakishughulika kuchungua na kutafuta. Je! Walipata pa kukimbilia
wasiangamizwe?
37. Hakika kwa
waliyo tendewa hao wa kaumu zilizo kwisha pita ni mawaidha kwa mwenye moyo wa
kufahamu hakika ya mambo, au akasikiliza uwongofu naye akili zake anazo.
38. Ninaapa:
Hakika tumeziumba mbingu na ardhi na viumbe viliomo baina yao katika siku sita.
Na hatukupata kuchoka. Rejea mambo yaliyo khusu maana ya neno "Siku" za uumbaji
katika maelezo ya kitaalamu juu ya Aya za idadi 9 mpaka 12 katika Sura ya
"Fuss'ilat". 41:9-12
39,40. Ikiwa
haya yamebainika, basi, ewe Mtume, yastahamilie hayo wayasemayo hao wanao
kanusha, ya uwongo na uzushi kukhusu Utume wako. Nawe mtakasishe, Msabbih,
Muumba wako na Mlezi wako na kila upungufu, ukimhimidi wakati wa alfajiri, na
wakati wa alasiri, kwani ibada nyakati hizo ni jambo kuu. Na pia mtakasishe,
Msabbih, katika saa za usiku, na baada ya Sala.

41,42. Na
sikiliza khabari ninazo kwambia katika hadithi za Kiyama kwani shani yake ni
kubwa. Siku atapo nadi Malaika wa kunadi kutoka pahala pa karibu na hao wanao
itwa. Siku watapo sikia mpulizo wa pili wa Haki, nao ni wa kufufuliwa watu. Hiyo
ndiyo siku ya kutoka kwenye makaburi.

43. Hakika
Sisi, peke yetu, ndio tunao huisha viumbe vyote, na tunavifisha duniani. Na
kwetu Sisi, peke yetu, ndio marejeo Akhera.
44. Siku
itakapo wapasukilia ardhi, na watoke humo mbio mbio wakikimbilia
mkutanoni...Hilo jambo kuu la kuwakusanya wote ni dogo na jepesi kwetu.
45. Sisi
tunajua kuliko yeyote hayo wayasemayo ya uwongo juu yaliyo khusu Utume wako.
Wala wewe hukutumwa uwalazimishe kwa unayo yataka. Ila wewe ni mwonyaji basi
mkumbushe kwa Qur'ani Muumini mwenye kuiogopa adhabu yangu ili ukumbusho umfae..
Rudi kwenye
sura
Copyright � 22 August 1997, Sheikh
Ali Muhsin Al Barwani