1. Walio mkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakawazuilia watu wasiingie katika Uislamu, Mwenyezi Mungu amevivunja vyote walivyo vitenda.
 
2. Na walio amini, na wakatenda mema, na wakasadiki yaliyo teremshwa kwa Muhammad, nayo ni Haki iliyo toka kwa Mola wao Mlezi, atawafutia makosa yao, na atawatengenezea hali yao ya Dini na dunia.
 
3. Hayo ni kwa sababu walio kufuru wamefuata njia ya upotovu, na kwamba walio amini wamefuata njia ya Haki iliyo toka kwa Mola wao Mlezi. Kwa mfano kama huu wa kubainisha kwa uwazi ndio Mwenyezi Mungu anawaeleza watu hali zao ili wapate kuzingatia.
 
4,5,6. Mtapo kutana na walio kufuru katika vita basi wapigeni kwenye shingo zao, mpaka mtakapo wadhoofisha kwa wingi wa kuwauwa, basi tena wafungeni mateka. Tena ama waachilieni wende zao kwa wema na ihsani, baada ya kwisha vita, kwa kuwaachia bila ya fidia, au kwa fidia ya kutoa mali au kubadilishana kwa mateka wa Kiislamu. Inakuwa mmewaachilia kwa badali. Huu ndio uwe mwendo wenu na makafiri mpaka vita vimalizike kabisa. Mwenyezi Mungu anawahukumieni hivyo. Na lau angeli taka bila ya shaka angeli washinda bila ya vita, lakini haya ni ili awajaribu Waumini kwa makafiri kama mtihani ndio ameamrisha Jihadi. Na walio uwawa katika njia ya Mwenyezi Mungu kabisa hatoacha vitendo vyao vipotee. (1) Atawahidi, na azitengeneze nyoyo zao, na awatie katika Pepo aliyo kwisha wajuulisha.
(1) Katika Aya hii tukufu zimetajwa "shingo" khasa, kwa sababu kuzipiga hizo ndio njia inayo faa mno kummaliza upesi mwenye kupigwa bila ya kumuadhibu na kumtesa. Kwani imethibiti kwa ilimu kuwa shingo ndiyo kiungo baina ya kichwa na kiwiliwili kizima. Basi ukikatika mshipa wa uti wa mgongo wenye kupeleka hisiya zote, basi viungo vyote muhimu vinapooza. Na ikikatika mishipa ya damu, damu inasita kufika kwenye ubongo. Na zikikatika njia za kupitisha hewa, basi pumzi husita. Na katika hali hizi zote uhai unakatika mara moja.
 
7. Enyi mlio amini! Mkiinusuru Dini ya Mwenyezi Mungu, na Yeye atakunusuruni muwashinde maadui zenu, na ayatilie nguvu mambo yenu.
 
8. Na walio kufuru Mwenyezi Mungu atawatia mashakani, na atawapotoa vitendo vyao.
 
9. Mambo yao ni hivyo kwa sababu wao wanakereka na aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, yaani Qur'ani na amri zake. Basi Mwenyezi Mungu amevibat'ilisha vitendo vyao.
 
10. Wameshindwa kutafuta ya kuwazindua, hata hawakutembea katika ardhi wakaangalia hali gani ulikuwa mwisho wa walio wakadhibisha Mitume kabla yao? Mwenyezi Mungu aliwateremshia hilaki katika kila kilicho khusiana nao, nafsi zao, mali yao, na watoto wao. Na wenye kumkataa Mwenyezi Mungu na Mitume wake ndio hupata mwisho mfano wa huo.
 
11. Malipo hayo ndio ushindi wa Waumini na kushindwa nguvu makafiri, ni kwa sababu hakika Mwenyezi Mungu ni rafiki mlinzi wa walio amini na ndiye Mwenye kuwanusuru; na makafiri hawana rafiki mlinzi wa kuwanusuru wala kuwakinga na kuangamia.
 
12. Hakika Mwenyezi Mungu atawatia wenye kuamini na wakatenda mema katika Pepo tukufu zenye kupitiwa ndani yake mito. Na makafiri wanastarehe duniani kidogo, na wanakula kama walavyo wanyama, wamepigwa na mghafala wala hawajifikirii mwisho wao. Hawanalo lao ila matamanio yao. Na kesho Akhera nyumba yao ni Motoni.
 
13. Na wengi katika watu wa miji walio tangulia walio kuwa na nguvu zaidi kushinda watu wa mji wako wa Makka ambao watu wake wamekufukuza, ewe Muhammad, tuliwaangamiza kwa namna mbali mbali za adhabu. Na hakutokea yeyote wa kuwanusuru nasi.
 
14. Je! Wanaweza kuwa sawa makundi mawili haya katika malipo? Mwenye kuwa na ujuzi wazi kumjua Muumba wake na Mlezi wake, naye akawa anamt'ii, atakuwa sawa na mwenye kuwa na vitendo vyake viovu naye akaviona ni vizuri, na akafuata hayo ayatendayo na akaeneza pumbao lake la upotovu.
 
15. Sifa ya Pepo walio ahidiwa wachamngu ni kama hivi: ndani yake imo mito ya maji yasiyo chafuka, na mito ya maziwa yasiyo haribika utamu wake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyo safishwa na takataka zote. Na humo watakuwa na kila namna ya matunda, na msamaha mkubwa kutokana na Mola wao Mlezi. Je! Sifa za Pepo ya hawa ni kama sifa itayo kuwa ni malipo ya mwenye kudumu milele Motoni, na akanyweshwa maji yaliyo tokota ya kukata matumbo? Aya hii tukufu inataka tuzingatie kuwa maji yaliyo vunda, yaliyo tuama, yenye kutaghayari, ni maji yenye madhara. Na Aya hii tukufu imesema hayo kabla ya kuvumbuliwa darubini za kutazamia vijidudu (Microscope) kwa makarne ya miaka, ndipo ilipo juulikana kuwa maji yaliyo tuama yaliyo taghayari yanakuwamo ndani yake mamilioni ya vijidudu vyenye madhara ya kuwasibu watu na wanyama kwa namna mbali mbali ya magonjwa.
 
16. Na miongoni mwa makafiri kipo kikundi cha watu wanao kusikiliza wewe, Muhammad. Hawakuamini wewe, wala hawanafiiki na maneno yako. Mpaka wakisha ondoka kwenye baraza yako husema kwa kejeli kuwaambia walio pewa ujuzi: Kasema nini huyu Muhammad sasa hivi? Watu hao ndio Mwenyezi Mungu amepiga muhuri wa ukafiri juu ya nyoyo zao. Ndio wameiacha kheri wakifuata matamanio yao.
 
17. Na walio ongoka wakashika njia ya Haki, Mwenyezi Mungu huwazidishia uwongofu, na akawapa kinga chao cha kujikingia na Moto.
 
18. Wanao kanusha hawawaidhiki na hali za walio tangulia. Basi je! Wanangojea Saa (ya Kiyama) iwajie kwa ghafla? Kwa hakika alama zake zimekwisha dhihiri, na wao hawajazingatia kuwa inakuja. Basi watakumbuka wapi itapo wajia mara moja kwa ghafla?
 
19. Basi thibiti juu ya ujuzi ya kwamba hakika hapana wa kuabudiwa kwa Haki ila Mwenyezi Mungu tu. Na muombe maghfira Mwenyezi Mungu kwa dhambi yako na madhambi ya Waumini wanaume na Waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu anajua kila lenu, la kupita na la kukaa.
 
20,21,22. Walio amini wanasema: Haiteremki Sura ya kututaka tupigane? Na ikiteremka Sura ambayo haifasiriki vyenginevyo ila ni kulazimisha tu, na ikataja ndani yake kuamrishwa vita, utawaona ambao katika nyoyo zao mna unaafiki wanakuangalia kwa muangalio wa mwenye kuzimia kwa mauti, jinsi ya kuviogopa na kuvichukia vita. Linalo wastahikia kulifanya ni kumt'ii Mwenyezi Mungu na kusema neno linalo kubaliana na sharia. Na mambo yakawa ni kweli, na ikawalazimu kupigana, basi lau kuwa ni kweli wana Imani ya Mwenyezi Mungu na ut'iifu ingeli kuwa bora kwao kuliko huo unaafiki. Basi ndio mnavyo tarajiwa, enyi wanaafiki, kuwa mkipata madaraka ndio mfisidi katika nchi na mkate makhusiano yenu na jamaa zenu?
 
23. Hao ndio alio watenga mbali kabisa Mwenyezi Mungu na rehema yake, na akawatia uziwi wasiisikie Haki, na akawatia upofu wa macho wasiione Njia ya Uwongofu.
 
24. Wameingia upofu hata hawaufahamu uwongofu wa Qur'ani? Bali kwenye nyoyo zao zipo kufuli zinawazuia wasiizingatie.
 
25. Hakika wale walio ritadi, wakarejea nyuma kwenye ukafiri na upotofu walio kuwa nao baada ya kuwadhihirikia njia ya uwongofu, Shetani ndiye aliye wapambia, na akawakunjulia matamanio ya uwongo.
 
26,27. Kurejea huko ukafirini ni kwa kuwa waliwaambia wenye kuchukia aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu: Tutakut'iini katika baadhi ya mambo. Na Mwenyezi Mungu anazijua siri za hawa wanaafiki. Hiyo ndiyo hali katika maisha ya duniani, basi watakuwa katika hali gani Malaika watapo wafisha huku wakiwapiga nyuso zao na migongo yao kwa kuwadhalilisha?
 
28. Kufishwa namna hiyo ya kutisha katika hali hiyo ni kwa kuwa hakika wao waliufuata upotovu ulio mkasirisha Mwenyezi Mungu, na wakaichukia Haki inayo mpendeza Mwenyezi Mungu. Basi akayabat'ilisha waliyo yatenda.
 
29. Hivyo wanadhani hawa wenye unaafiki katika nyoyo zao kwamba Mwenyezi Mungu hatazifichua chuki zao wanazo mchukia Mtume wake na Waumini?
 
30. Tungeli penda bila ya shaka tungeli kuonyesha hao wanaafiki, nawe ungeli wajua kwa alama zao, na ungeli wajua kwa namna yao wanavyo sema. Na Mwenyezi Mungu anajua ukweli wa vitendo vyenu vyote.
 
31. Na ninaapa: Bila ya shaka tutakujaribuni kama kukufanyieni mtihani, mpaka tuwajue Mujaahidina, wanao pigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, katika nyinyi, na wenye kuvumilia wakati wa shida na dhiki, na tuzijue khabari zenu za ut'iifu na maasi katika Jihadi na penginepo.
 
32. Hakika walio kufuru na wakazuia njia ya Mwenyezi Mungu, na wakenda kinyume na Mtume kwa inda na ukaidi, baada ya kwisha wadhihirikia uwongofu, hao hawatamdhuru Mwenyezi Mungu kwa lolote. Na Yeye atayabat'ilisha yote waliyo yatenda.
 
33. Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu katika aliyo kuamrisheni, na mt'iini Mtume kwa hayo anayo kuitieni, wala msivipoteze vitendo vyenu.
 
34. Hakika walio kufuru na wakazuia watu wasiingie katika Uislamu, kisha wakafa nao ni makafiri, basi Mwenyezi Mungu hatawasamehe.
 
35. Basi msijifanye wanyonge mbele ya maadui zenu mnapo kutana nao. Wala msiwatake suluhu kwa kuwaogopa, na hali nyinyi ndio mko juu, na ni wenye kushinda kwa nguvu za Imani. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi kwa nusra yake; na wala hatakupunguzieni malipo ya vitendo vyenu.
 
36,37. Hakika uhai wa dunia ni upotovu na udanganyifu. Na nyinyi mkiamini na mkaacha maasi, na mkafanya kheri, Mwenyezi Mungu atakupeni thawabu ya hayo, wala hakutakini mali yenu. Akikutakeni na akakushikilieni basi nyinyi mtafanya uchoyo, na chuki zenu zitaonekana kwa mnavyo yapenda mali.
 
38. Hivi mnaitwa mtumie katika njia ya Mwenyezi Mungu aliyo iamrisha. Kati yenu wapo wanao fanya ubakhili kutoa. Na mwenye kufanya ubakhili hamdhuru mtu ila nafsi yake. Na Mwenyezi Mungu peke yake ndiye tajiri, hana haja ya mtu, na nyinyi ndio mafakiri wenye kumhitajia Yeye. Na mkiacha kumt'ii Mwenyezi Mungu basi atakubadilisheni pahala penu awalete watu wengine, tena hao hawatakuwa mfano wenu wa kuacha kumt'ii.
 
Copyright � 22 August 1997, Sheikh Ali Muhsin Al Barwani