Assalaamu alaykum Warahmatullaahi Wabarakaatuh'

Waba'd:

Alhamdulillaah wassalaatu wassalaam 'alaa Rasoolillaah wa'alaa aalihi wasahaabatihi ajma'een.

Tunafuraha kuwaletea kwa mara ya kwanza kabisa tarjuma ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya kiswahili iliyo tarjumiwa na Sh. Ali Muhsin Al-Barwani katika muundo wa "HTML HELP". Kwa vile hii ni tarjuma ya kwanza na ya pekee kuweko katika muundo huu, tunajaribu kurekebisha makosa madogo hapa na pale yalio tokamana na ukusanyaji na utengenezaji wa kitabu hiki. Iwapo utapata kuona matego na makosa ya kiherufi, au kuto patikana kwa ayaa ya Qur'ani kwa herufi ya kiarabu, tafadhali tujulishe kwa kutu andikia barua pepe (email) kwa anwani ipatikanayo hapa chini. Tuna endelea kuboresha kitabu hiki na panapo majaaliwa ya Mola tuta wajulisha tutakapo toa toleo la pili insha-Allah.

Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo. Faida ya iliyo yachuma ni yake, na khasara ya iliyo yachuma ni juu yake pia. Mola wetu Mlezi! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. (Surat al-Baqarah 2:286)

Tuna mwomba Mwenyezi Mungu atukubaliye na kuzitakasa amali zetu ziwe ni kwa ajili ya kutaka Radhi na Msamaha kutoka Kwake (ameen).

Barakallah feekum.

Wassalaamu 'alaykum Warahmatullaahi Wabarakatuh

Abu Malaadh Said Awadh Baadel
Qur'an wa Sunnah Society of East Africa (
http://www.qssea.net)
anwani: info@qssea.net au hadhramee@hotmail.com
Tarjuma ya Qur'an Tukufu v.1.0
September 30, 2005 | Sha`ban 26, 1426
image
image

Online version: http://www.qurantukufu.net