Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
0

1. Jua litakapo kunjwa, 1

2. Na nyota zikazimwa, 2

3. Na milima ikaondolewa, 3

4. Na ngamia wenye mimba pevu watakapo achwa
wasishughulikiwe, 41

5. Na wanyama wa mwituni wakakusanywa, 5

6. Na bahari zikawaka moto, 6

7. Na nafsi zikaunganishwa, 7

8. Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa, 8

9. Kwa kosa gani aliuliwa? 9

10. Na madaftari yatakapo enezwa, 10

11 Na mbingu itapo tanduliwa, 11

12. Na Jahannamu itapo chochewa, 12

13. Na Pepo ikasogezwa, 13

14. Kila nafsi itajua ilicho kihudhurisha. 14

15. Naapa kwa nyota zinapo rejea nyuma, 15

16. Zinazo kwenda, kisha zikajificha, 16

17. Na kwa usiku unapo pungua, 17

18. Na kwa asubuhi inapo pambazuka, 18

19. Kwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe
mtukufu, 19

20. Mwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye Kiti
cha Enzi, 20

21. Anaye t'iiwa, tena muaminifu. 21

22. Na wala huyu mwenzenu hana wazimu. 22

23. Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio
safi. 23

24. Wala yeye si bakhili kwa mambo ya ghaibu. 24

25. Wala hii si kauli ya Shetani maluuni. 25

26. Basi mnakwenda wapi? 26

27.
Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote.
27

28. Kwa yule miongoni mwenu anaye taka kwenda sawa.
28

29. Wala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Mwenyezi
Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote. 29
Imetarjumiwa na Sheikh Ali Muhsin
Al-Barwani
Ikiwa
una ushauri au maoni juu ya tarjuma hii, andika kwa anwani hii qurani-tukufu@geocities.com
Copyright � 22 August 1997, Sheikh
Ali Muhsin Al Barwani